Vita haipiganwi kama kula maandazi na chai ya rangi unang'ata andazi popote tu hata umetizama kwingine.
Hapo kuna mission inatakiwa kukamilishwa ikiwemo kuepuka majeruhi na vifo vya raia, uharibifu wa miundo mbinu, kuwakamata walengwa wakiwa hai nk.
Urusi wamejipa saa 72 kukamilisha misheni yao. Leo rais wa Ukrain ndugu Zelesky akiongea toka mafichoni ameaga washirika wake wa NATO kuwa itakuwa mara ya mwisho kuongea nao kwani ndani ya saa 48 zijazo lolote laweza tokea kwake akiwa yeye ni mlengwa wa kwanza. Hizo saa 48 ukiongeza 24 zilizopita ni saa 72 za misheni ya Mrusi.
Vita sio maana wasio na hatia wanaumia kwa maslahi ya wapuuzi wachache