Hakuna video. Hakuna picha ya kusapoti taarifa zao zinazoonyesha hayo yanayofanyika.
Mbona leo walivyowakamata wanajeshi wa Chechen 4 kuwatoa ndani ya gari na kuwapiga risasi na kuwaua wameonyesha video yao. Chechen walitoka jana jeshi la askari 1000. Leo 4 wameuuliwa tena muda huu. Iweje hizo za Urusi washindwe kuonyesha video hao askari waliyo waua kwa kiasi hicho wanachokisema?
Ukraine leo asubuhi wamesema Llyushin ndege ya Urusi yenye uwezo wa kubeba wanajeshi 200 wameilipua. Lakini mpaka sasa hivi hakuna picha, hakuna video.
Jana asubuhi ikatangazwa wamelipua ndege SU-27 ya Mrusi kumbe wametungua ndege ya kwao. Kucheki engine ni ndege ya kwao.
Ukraine walionyesha video wamewakamata askari wa jeshi la Urusi na kuonyesha wanawahoji hao mateka. Kuna kitu kinaitwa accent/lafudhi. Lafudhi yao si ya Warusi wana lafudhi ya Kiukraine. Ni maigizo wanafanya.
Zelensky sasa huko twitter anadai meli ya kivita ya Turkey imeizuia meli ya kivita ya Urusi kupita black sea. Lakini mamlaka ya Turkey kwa haraka imejibu muda huu yaani sasa hivi kuwa hiyo taarifa ni ya uongo.
View attachment 2132037
Ukraine kwa sasa hana airforce. Ukraine kwa sasa hana air defensive system. Ukraine hana drone. Ukraine hao hao wameua wanajeshi 3500 wa Urusi kwa siku 2. Amewaua kwa nini? Kwa vifaru?
Ukraine wanafanya propaganda nyingi sana kwenye mitandao ya kijamii ila siwalaumu kwani ni jambo zuri hususani nyakati za vita. Unabusti morali ya raia na wapambanaji wako. Ni psychological warfare. Ni hizi habari Warusi wakizisoma zinawachanganya maandamano yanazidi Urusi na anapata pressure ndani ya nchi kutoka kwa raia. Hapa wamempiga bao Putin.