LIVE Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

LIVE Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Live coverage on JamiiForums
Unachokataa ni nini? Hii ni taarifa ya Zelensky.

View attachment 2132087

Hii ni taarifa ya kutoka Uturuki kukanusha hiya taarifa.
View attachment 2132088
Ni juu yako! Kuchagua kuamini au kutoamini. Muda huu An-26 ya Ukraine imelipuliwa.
Wengi hawataki kukubali ukweli huu kwamba hii vita Putin kaingizwa chaka, na ajiandae kwenda kuwa mkimbizi China. Ufaransa ashaanza kutanguliza msaada wa silaha kabisa. Baada ya hilo kombora kuangushwa Poland Kitachofata itakuwa ni jeshi na sio msaada wa silaha peke yake.
 
Hii habari ya zuio la Black Sea ina mkanganyiko kidogo, maana rais wa Ukraine ameisema kama request muda mfupi uliopita. Imezua mjadala maana kuna vyanzo vingine vinadai kuwa Uturuki haijathibitisha kufanya hivyo.
Hii Taarifa inawaumiza Pro Putin sana...

Putin alitarajia vita ingeisha mapema...Sasa wazungu wa Ulaya wamejua udhaifu wake wanamfungia Kila sehemu ili mapambano ya na uwiano kidogo kama Russia katumia 1/3 ya jeshi lake ila Bado
 
Mtanzania wewe anajua kuwa ni propaganda lakini mrusi na ukraine wanajua ni kweli. Waukraine wanapata moyo, warusi habari zinawachanganya wanazidisha maandamano. Hichi ndicho ulichokisema ndugu yangu[emoji2][emoji2]
Jamaa una wivu juu ya kutojua kuelewa kinachoendelea. Yani unaona umepoteza sana ndio maana emoji za kujichekesha haziishi kwako. Kuna mada za ufyatuaji matofali, kilimo cha pilipili, ufugaji wa mabata, n.k zipo unaweza enda kuchangia, humu huna tija unaongeza emoji tu.

Hujui unachopinga, hutoi facts wala huna source za info kazi kubisha. Wenzako wanatoa hoja we unapinga kisa ni "Watanzania"
 
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine amesema Uturuki imekubali kufungia meli za Urusi kupita straits za Black sea. Ikitokea hivyo meli za Urusi hazitapita kwenda kushambulia Ukraine mpaka watumie bandari iliyopo Crimea
SIO KWELI.


Jana Rais Edorgan. Alikataa hilo.
 
Urudi chini ya Putin, wamepigana Vita 7 na zote wameshinda.


In fact kwenye hostoria yote ya vita vya urusi... HAWAJAWAH KUSHINDWA.


Ni suala la muda , serikali ya Kyiv alichofanya ,nikuweka Majeshi mengi kwenye mji mkuu, ndio sababu Urudi wanapata shida .


Ila lazima watoboe..... Urudi keshapigwa vikwazo, hana tena cha kupoteza, ni kupiga tuu.

Yaan nikm Tundu Lissu alivyopigwa Risasi alafu akapona .
 
MilardAyo nae kapost eti Warusi 3500 na nyungo zao 34 wamededishwa
Hao wanasikiliza habari za upande mmoja ambazo vyanzo vyake havina usahihi. Au kwa Nam na nyegine wanajua wanachokifanya.

Kwa mfano wengi walikuwa wanaandika Urusi tangu jana walisema wapo Kieve lakini mbona mpaka muda huu hakuna taarifa yoyote?

Ukweli ni kwamba Zelensky aliomba mapigano ya mji mkuu wa nchi yasimame ili wafanye mazungumzo pande zote 2, yaani Urusi na Ukraine. Urusi ikakubali. Ila mpaka muda huu Zelensky amekataa kufanya mazungumzo. Taarifa waliyoitoa Urusi ni hii:

Screenshot_20220226-164034.png

Kuanzia sasa mapigano yameshaanza.
 
URUSI NA UKRAINE;MGOGORO WA MTU NA MDOGO WAKE.

Leo 16:30pm 26/02/2022

Joseph Stalin kiongozi ambae aliifanya Soviet Union(USSR)kuwa na nguvu ya kivita,kiuchumi na kuogopwa duniani,aliunda Warsaw Pact kama muungano wa kiulinzi wa nchi za Ulaya Mashariki mwaka 1955 kama mpinzani wa NATO ambayo iliundwa mwaka 1949 ikiwa ni muungano wa nchi za Ulaya Magharibi .Soviet Union ilijumuisha Russia, Ukraine, Georgia, Belorussia, Uzbekistan, Armenia, Azerbaijan, Kazakhstan, Kyrgyzstan, Moldova, Turkmenistan, Tajikistan, Latvia,Vijana wa miaka ya 80 na 90 mnakumbuka enzi zetu za kupiga charter kwenye kuta "Wasoo" neno hilo lilitokana na nguvu na umaarufu wa iliyokuwa Warsaw Pact.

Warsaw Pact ilijumuisha Soviet Union, Albania, Poland, Czechoslovakia, Hungary, Bulgaria, Romania, and the German Democratic Republic,daima Soviet Union itawakumbuka malegendary V.I Lenin,Joseph Stalin,Nikita Krushchev,Boris Yeltsin na sasa Vladimir Putin,ndani ya Vladimir Putin nayaona mawazo na mitazamo ya Baba wa Soviet Union,Joseph Stalin ambae baada ya kuushinda Ufashisti akawa kiongozi pekee wa watu mwenye kuweza kutatua hatima ya mamilioni ya wananchi,
Kwa muda mfupi aliweza kuigeuza Soviet Union kutoka nchi ya uchumi wa kiwango cha tatu katika nguvu ya viwanda hadi kuwa nchi yenye nguvu kiviwanda,kiuchumi na kivita,

Kwa miongo kadhaa Kremlin imedai mara kwa mara kwamba nchi za Magharibi zilivunja ahadi ya kutopanua Nato. Madai hayo yanarejelea mazungumzo ya mwaka 1990, kati ya aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani James A. Baker na kiongozi wa zamani wa Usovieti Mikhail Gorbachev,Lakini viongozi wa Magharibi hawakubaliani na kusema hakukuwa na mpango wowote rasmi kuhusu kutopanua Nato hadi Ulaya Mashariki zaidi na kwamba muungano huo unashikilia 'sera ya mlango wazi.' kulingana na Rais wa Urusi Vladimir Putin,ikiwa Ukraine itakuwa mwanachama wa Nato (kwa sasa haijatuma maombi ya uanachama), "italeta tishio zaidi kwa Urusi"

uwepo wa Ukraine katika muungano, na uwezekano wa kutumwa kwa makombora yoyote ya masafa marefu yenye uwezo wa kushambulia miji ya Urusi au mifumo ya ulinzi ya makombora, sawa na ile ya Poland na Romania, itakuwa suala la "mstari mwekundu" kwa Moscow.Je unadhani USA yuko tayari kuwekewa silaha nzito nzito na jeshi la kivita la URUSI kwenye nchi jirani kabisa na USA kama Canada,Cuba na Mexico,Ndivyo jinsi ilivyo kidunia kwa Urusi pia yuko sahihi kukataa na kujihami ni mojawapo ya kanuni bora sana za kiuongozi kwa nchi yoyote ile duniani.

Mnamo mwaka 2014, Urusi iliyafadhili kijeshi makundi ya vuguvugu Mashariki mwa Ukraine katika majimbo ya CRIMEA,DONBASS,DONETSK na LUHANSK ambayo wakazi wengi wa majimbo hayo wana asili ya Urusi na wanazungumza Kirusi kwa ufasaha,katika mapambano hayo,Majeshi ya waasi kwa msaada wa Urusi walifanikiwa kuyateka majimbo hayo kutoka kwenye mikono ya Serikali ya Kyiv. Jimbo la CRIMEA liliamua kuitisha kura ya maoni (Referendum) ya kujitenga na Ukraine na kujiunga na Urusi.Majimbo mawili (Donestk na LUHANSK) yaliendeleza mapambano makali dhidi ya Majeshi ya Ukraine na kuchukua udhibiti KAMILI wa majimbo hayo. Katika Jimbo la DONBASS Majeshi ya Ukraine yalipambana Sana na hivyo waasi kushindwa kuliteka Jimbo Hilo kikamilifu.

Tarehe 24 Desemba 2021, Majeshi ya Urusi yalianza kuingiza mifumo ya Ulinzi wa Anga-ANT AIRCRAFT MISSILES (S-300 na S-400). Ujio wa Mifumo hiyo ya Ulinzi wa Anga ulisababisha DRONES za Ukraine kushindwa kufanya mashambulizi ya Anga. Hali hiyo ilitoa upenyo wa Majeshi ya Urusi na waasi kuchukua udhibiti upya wa majimbo ya DONBASS na LUHANSK,kutokana na Ukraine kutokuwa na Mifumo ya Ulinzi wa Anga (ANT-AIRCRAFT MISSILES) ya Uhakika, Basi Urusi ana nafasi ya kutumia ndege za kivita kushambulia Mifumo yote ya Ukraine ya kulipulia Vifaru Kabla ya vifaru hivyo kuanza kuingia kwenye Ardhi ya Ukraine kwa Urahisi zaidi,kutokana na Ukraine kulijua hili,imeamua kupeleka Mifumo yake ya kulipulia Vifaru karibu na mpaka wa Poland upande wa Magharibi. Makombora haya yanaweza kushambulia vifaru vyote vya Urusi ambavyo vitaingia Ukraine upande wa kaskazini wa Ukraine kutokea Belarus. Je,Urusi ataweza kushambulia kwa ndege za kivita Mifumo hii ya Ukraine ya kulipulia Vifaru ambavyo viko kwenye mpaka wa Poland? Jibu ni Hapana.

Kwasababu Marekani imeonya kwamba, endapo ndege za kivita za Urusi zitakaribia kwenye mipaka ya NATO(Poland ni Mwanachama wa NATO) Basi Marekani hatasita kuzitungua ndege Hizo. Ikumbukwe kuwa, Mwaka 2017, ndege ya Kivita Ya Urusi iliyokuwa inafanya mission ya kuwashambulia waasi wa ISLAMIC STATE ilitunguliwa na Mifumo ya Anga ya Uturuki ilipokaribia Anga la Uturuki kwenye Mpaka wa Uturuki na Syria. Hili tukio liliharibu uhusiano wa kidiplomasia Kati ya Uturuki na Urusi.

Kutokana na Uwezo mkubwa wa kijeshi wa Urusi ukilinganisha na Ukraine,bila Shaka Urusi itaibuka kidedea na kuyateka maeneo mengi ya Ukraine Kama itataka hivyo. Ushindi huo wa Urusi hautakuja kwa urahisi,Urusi inaweza kushuhudia kulipuliwa kwa vifaru vyake vingi ambavyo vitaingia kwenye ardhi ya Ukraine kuliko vifaru 140 ambavyo Urusi alivipoteza wakati wa Uvamizi wa nchi ya GEORGIA. Hii ni kutokana na Ukraine kupokea msaada wa Siraha za kulipua vifaru (ANT-TANK MISSILES) Zaidi ya Tani 80 kutoka Uingereza. Mwaka 2014 Ukraine haikuwa na Siraha hizi.

Urusi ilishaonya toka kitambo kwamba haitaruhusu kuona nguvu na ushawishi wa jumuia ya NATO inasogea karibu na mipaka yake,tujipe chemsha bongo kidogo,hivi Cuba pia si ni nchi huru ndugu zangu!?Je nini kilitokea pale Cuba alipotaka kumkaribisha Mrusi kujenga base ya kivita nyumbani kwake kwenye mji wake Mkuu wa Havana,Rais Kennedy akaenda Havana akabomoa kila kitu.
Huwezi ruhusu jirani yako awe na zana kali za kivita tena akisaidiwa na mpinzani wake mkuu kuzikusanya pamoja,Ukraine aondoe wazo lake la kujitanua kijeshi kwa mgongo wa NATO akisaidiwa na USA
La sivyo kaka ake wa Kwanza Russia atampiga kila siku.

Nikiishia hapa,Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078854

-Bachelor of Business Administration in International Business.
-Master of Leadership and Management.

Recent Publication;
-Assessment on the Effects of Micro-Financing on Poverty Reduction.
 
1645887463517.png

Mwaka 1955 Wakati Congo ipo Chini ya Ubeligiji
-Baba mmoja wa kizungu Alinunua mtt wa kiafrika na kumuweka kwenye wavu kwajili ya watoto wake kuchezea kama mdoli,.
[emoji26][emoji26] wazungu ni [emoji706][emoji706] View attachment 2131661

Sent from my SM-A022F using JamiiForums mobile app
Maelezo hayo huwezi kuamini mwenyewe. Ni watoto wanaocheza kati yake. Kitu hicho cha waya ni kwa ajili ya ndege, inaonekana waliwahi kuwa na ndege kama kasuku aliyefungwa ndani yake. Sasa ni watoto wanaocheza. Kama ni Kongo la 1955, basi uwezekano mkubwa huyu mdogo ni mtoto wa wafanyakazi wa nyumba wa familia ya kizungu, na watoto wanacheza pamoja. Labda kwa kufurahia, labda kwa kuchokoza (maana mdogo hacheki...)
 
Urudi chini ya Putin, wamepigana Vita 7 na zote wameshinda.


In fact kwenye hostoria yote ya vita vya urusi... HAWAJAWAH KUSHINDWA.


Ni suala la muda , serikali ya Kyiv alichofanya ,nikuweka Majeshi mengi kwenye mji mkuu, ndio sababu Urudi wanapata shida .


Ila lazima watoboe..... Urudi keshapigwa vikwazo, hana tena cha kupoteza, ni kupiga tuu.

Yaan nikm Tundu Lissu alivyopigwa Risasi alafu akapona .
Hungary uprising nayo walishinda ya mwaka 1956...Warusi hawaji kurudia upuuzi wao kama huu huko Hungary wakichapika mno mno...
 
Tuseme chanzo ni Marekani na washirika wake kutaka kuweka silaha zao za Nuke Ukraine kwa kupitia mgongo wa Ukraine kujiunga na NATO.

Mkataba wa Minsk uliosainiwa sijui miaka mingapi iliweka wazi kwamba NATO haitaendelea kujitanua kuelekea upande wa Urusi hivyo kitendo cha NATO kutaka kupokea Ukraine ni kuvunja mkataba huo.

Hii ndiyo maana Putin amezionya Finland na Sweden nao wakijifanya kutaka kujiunga na NATO watapigwa vibaya.
Yaani nyie mnamlaumu victim badala ya aggressor?

Ukraine ni nchi huru na ina haki ya kuchagua marafiki zake.

Ukraine ilitaka sana kuwa Karibu na Russia Lakini Russia ni bullies na hawaaminiki. Mwanzoni walisema wataheshimu Uhuru wa nchi zote zilizokuwa Soviet Union. Lakini baadaye wakaivamia Georgia.

Mwaka 2014 wakaivamia Ukraine na kuteka baadhi ya maeneo. Na sasa wanawaunga mkono waasi wa Ukraine wanaotaka kujitenga.

Tokea hapo Ukraine ikaaamua kufungamana na EU na kutaka kujiunga na NATO Kama njia ya kujilinda na Urusi. Pia Urusi ni maskini hawana uwezo wa kuisaidia Ukraine. Hivyo baada ya miaka zaidi ya 30 ya Uhuru, Ukraine wameamua kuwa future yao itakuwa nzuri wakiungana na EU.

Urusi wamechukia kuona koloni lao la Ukraine linawakimbia. Wanaamua kuwalazimisha kwa kipigo.
 
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine amesema Uturuki imekubali kufungia meli za Urusi kupita straits za Black sea. Ikitokea hivyo meli za Urusi hazitapita kwenda kushambulia Ukraine mpaka watumie bandari iliyopo Crimea
Acha kuchujua habari toka kwa Comedian Rais wa Ukraine a.k.a. Masanja muigizaji

 
Back
Top Bottom