URUSI NA UKRAINE;MGOGORO WA MTU NA MDOGO WAKE.
Leo 16:30pm 26/02/2022
Joseph Stalin kiongozi ambae aliifanya Soviet Union(USSR)kuwa na nguvu ya kivita,kiuchumi na kuogopwa duniani,aliunda Warsaw Pact kama muungano wa kiulinzi wa nchi za Ulaya Mashariki mwaka 1955 kama mpinzani wa NATO ambayo iliundwa mwaka 1949 ikiwa ni muungano wa nchi za Ulaya Magharibi .Soviet Union ilijumuisha Russia, Ukraine, Georgia, Belorussia, Uzbekistan, Armenia, Azerbaijan, Kazakhstan, Kyrgyzstan, Moldova, Turkmenistan, Tajikistan, Latvia,Vijana wa miaka ya 80 na 90 mnakumbuka enzi zetu za kupiga charter kwenye kuta "Wasoo" neno hilo lilitokana na nguvu na umaarufu wa iliyokuwa Warsaw Pact.
Warsaw Pact ilijumuisha Soviet Union, Albania, Poland, Czechoslovakia, Hungary, Bulgaria, Romania, and the German Democratic Republic,daima Soviet Union itawakumbuka malegendary V.I Lenin,Joseph Stalin,Nikita Krushchev,Boris Yeltsin na sasa Vladimir Putin,ndani ya Vladimir Putin nayaona mawazo na mitazamo ya Baba wa Soviet Union,Joseph Stalin ambae baada ya kuushinda Ufashisti akawa kiongozi pekee wa watu mwenye kuweza kutatua hatima ya mamilioni ya wananchi,
Kwa muda mfupi aliweza kuigeuza Soviet Union kutoka nchi ya uchumi wa kiwango cha tatu katika nguvu ya viwanda hadi kuwa nchi yenye nguvu kiviwanda,kiuchumi na kivita,
Kwa miongo kadhaa Kremlin imedai mara kwa mara kwamba nchi za Magharibi zilivunja ahadi ya kutopanua Nato. Madai hayo yanarejelea mazungumzo ya mwaka 1990, kati ya aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani James A. Baker na kiongozi wa zamani wa Usovieti Mikhail Gorbachev,Lakini viongozi wa Magharibi hawakubaliani na kusema hakukuwa na mpango wowote rasmi kuhusu kutopanua Nato hadi Ulaya Mashariki zaidi na kwamba muungano huo unashikilia 'sera ya mlango wazi.' kulingana na Rais wa Urusi Vladimir Putin,ikiwa Ukraine itakuwa mwanachama wa Nato (kwa sasa haijatuma maombi ya uanachama), "italeta tishio zaidi kwa Urusi"
uwepo wa Ukraine katika muungano, na uwezekano wa kutumwa kwa makombora yoyote ya masafa marefu yenye uwezo wa kushambulia miji ya Urusi au mifumo ya ulinzi ya makombora, sawa na ile ya Poland na Romania, itakuwa suala la "mstari mwekundu" kwa Moscow.Je unadhani USA yuko tayari kuwekewa silaha nzito nzito na jeshi la kivita la URUSI kwenye nchi jirani kabisa na USA kama Canada,Cuba na Mexico,Ndivyo jinsi ilivyo kidunia kwa Urusi pia yuko sahihi kukataa na kujihami ni mojawapo ya kanuni bora sana za kiuongozi kwa nchi yoyote ile duniani.
Mnamo mwaka 2014, Urusi iliyafadhili kijeshi makundi ya vuguvugu Mashariki mwa Ukraine katika majimbo ya CRIMEA,DONBASS,DONETSK na LUHANSK ambayo wakazi wengi wa majimbo hayo wana asili ya Urusi na wanazungumza Kirusi kwa ufasaha,katika mapambano hayo,Majeshi ya waasi kwa msaada wa Urusi walifanikiwa kuyateka majimbo hayo kutoka kwenye mikono ya Serikali ya Kyiv. Jimbo la CRIMEA liliamua kuitisha kura ya maoni (Referendum) ya kujitenga na Ukraine na kujiunga na Urusi.Majimbo mawili (Donestk na LUHANSK) yaliendeleza mapambano makali dhidi ya Majeshi ya Ukraine na kuchukua udhibiti KAMILI wa majimbo hayo. Katika Jimbo la DONBASS Majeshi ya Ukraine yalipambana Sana na hivyo waasi kushindwa kuliteka Jimbo Hilo kikamilifu.
Tarehe 24 Desemba 2021, Majeshi ya Urusi yalianza kuingiza mifumo ya Ulinzi wa Anga-ANT AIRCRAFT MISSILES (S-300 na S-400). Ujio wa Mifumo hiyo ya Ulinzi wa Anga ulisababisha DRONES za Ukraine kushindwa kufanya mashambulizi ya Anga. Hali hiyo ilitoa upenyo wa Majeshi ya Urusi na waasi kuchukua udhibiti upya wa majimbo ya DONBASS na LUHANSK,kutokana na Ukraine kutokuwa na Mifumo ya Ulinzi wa Anga (ANT-AIRCRAFT MISSILES) ya Uhakika, Basi Urusi ana nafasi ya kutumia ndege za kivita kushambulia Mifumo yote ya Ukraine ya kulipulia Vifaru Kabla ya vifaru hivyo kuanza kuingia kwenye Ardhi ya Ukraine kwa Urahisi zaidi,kutokana na Ukraine kulijua hili,imeamua kupeleka Mifumo yake ya kulipulia Vifaru karibu na mpaka wa Poland upande wa Magharibi. Makombora haya yanaweza kushambulia vifaru vyote vya Urusi ambavyo vitaingia Ukraine upande wa kaskazini wa Ukraine kutokea Belarus. Je,Urusi ataweza kushambulia kwa ndege za kivita Mifumo hii ya Ukraine ya kulipulia Vifaru ambavyo viko kwenye mpaka wa Poland? Jibu ni Hapana.
Kwasababu Marekani imeonya kwamba, endapo ndege za kivita za Urusi zitakaribia kwenye mipaka ya NATO(Poland ni Mwanachama wa NATO) Basi Marekani hatasita kuzitungua ndege Hizo. Ikumbukwe kuwa, Mwaka 2017, ndege ya Kivita Ya Urusi iliyokuwa inafanya mission ya kuwashambulia waasi wa ISLAMIC STATE ilitunguliwa na Mifumo ya Anga ya Uturuki ilipokaribia Anga la Uturuki kwenye Mpaka wa Uturuki na Syria. Hili tukio liliharibu uhusiano wa kidiplomasia Kati ya Uturuki na Urusi.
Kutokana na Uwezo mkubwa wa kijeshi wa Urusi ukilinganisha na Ukraine,bila Shaka Urusi itaibuka kidedea na kuyateka maeneo mengi ya Ukraine Kama itataka hivyo. Ushindi huo wa Urusi hautakuja kwa urahisi,Urusi inaweza kushuhudia kulipuliwa kwa vifaru vyake vingi ambavyo vitaingia kwenye ardhi ya Ukraine kuliko vifaru 140 ambavyo Urusi alivipoteza wakati wa Uvamizi wa nchi ya GEORGIA. Hii ni kutokana na Ukraine kupokea msaada wa Siraha za kulipua vifaru (ANT-TANK MISSILES) Zaidi ya Tani 80 kutoka Uingereza. Mwaka 2014 Ukraine haikuwa na Siraha hizi.
Urusi ilishaonya toka kitambo kwamba haitaruhusu kuona nguvu na ushawishi wa jumuia ya NATO inasogea karibu na mipaka yake,tujipe chemsha bongo kidogo,hivi Cuba pia si ni nchi huru ndugu zangu!?Je nini kilitokea pale Cuba alipotaka kumkaribisha Mrusi kujenga base ya kivita nyumbani kwake kwenye mji wake Mkuu wa Havana,Rais Kennedy akaenda Havana akabomoa kila kitu.
Huwezi ruhusu jirani yako awe na zana kali za kivita tena akisaidiwa na mpinzani wake mkuu kuzikusanya pamoja,Ukraine aondoe wazo lake la kujitanua kijeshi kwa mgongo wa NATO akisaidiwa na USA
La sivyo kaka ake wa Kwanza Russia atampiga kila siku.
Nikiishia hapa,Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078854
-Bachelor of Business Administration in International Business.
-Master of Leadership and Management.
Recent Publication;
-Assessment on the Effects of Micro-Financing on Poverty Reduction.