Mko wapi mliokuwa mnabisha mkiambiwa Russian military imeonesha weakness? Mpaka sasa mbwembwe za mashabiki waliosema masaa tu Ukraine inaanguka na leo siku ya tatu bado hamna kitu. Jeshi lililokuwa limebakiza almost 10km kuingia city centre bado halijaingia zaidi ya masaa 20 mengine
Vifaru vya Urusi vinaharibiwa na Javelins za Marekani na NLAWS za UK & Sweden. Bado Ujerumani itatoa aina gani sijui ni Spike. Sitaki kuamini kama Ujerumani silaha zake zinaweza shambuliwa effectively na anti armour weapons za Russia mfano Kornet ATGM.
Stinger MANPADS zitafanya helicopters kuruka iwe ngumu. Ukraine ilinunua Bayraktar TB2 za Uturuki ila mpaka sasa haijaonekana clip hata moja, kuna makisio tofauti either wameamua kufanya kimyakimya zisitoe publicity zisije tafutwa kuharibiwa na zisilete mgogoro haina ya Turkey na Russia. Au zimeharibiwa na airstrikes kwenye base zilipokuwa.
Russia alileta silaha za kawaida na ndizo anazo nyingi kwenye inventory yake. Na wanajeshi wengi alioleta ni conscripts, watu wako kwenye mazoezi ghafla wanaambiwa vamia. Hawajaaga nyumbani, hawajajipanga, hawana utayari, wanapigana bila kujua sababu. Wamekamatwa watu wengine miaka 19 wanapewa simu ambazo Ukraine ndio imeanzisha huo utaratibu, wakipiga kwa mama zao mama wanashangaa watoto wao wameenda lini vitani.
Hakuna kitu alichotegemea Putin kimetimia. Na hakujipanga kupigana mpaka sasa. Majenerali wake wanaweza kuwa walijua si mbinu sahihi ila yeye ana tabia ya kuzungukwa na watu wa ndio mzee ambao hujibu kile anachokipenda. Ukitaka kujua hilo, tafuta video ya kikao cha kwanza anapotangaza anaingia Ukraine pale alipokuwa na Security council akafikia kuhutubia mkuu wa Foreign Intelligence akaongea kitu tofauti Putin akabadilika yule jamaa akababaika akajibu vingine kabisa