LIVE Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Live coverage on JamiiForums
Russia waneomba poo,baada ya jumuiya ya kimataifa kupitisha vikwazo vya uchumi ambavyo Russia hawezi kutoboa.
Pia Russia wamemiscalculate uvamizi wao wa nchi ya Ukraine,walidani operation yao inaweza kufanikiwa kwa mda mfupi,lakini wamekutana na upinzani mkubwa,majeshi na wananchi wa Ukraine wameonyesha uzalendo na mapenzi kwa nchi yao,wamesimama kidete na kupigana dhidi ya majeshi ya wavamizi na kusababisha hasara kubwa kwa Russia,vifo na majeruhi wengi wa wanajeshi wa Russia jumlisha vikwazo vya uchumi,vimempelekea Putin kupeleka wajumbe mezani,
 
Binafsi nimependa utulivu wa MACRON, sambasamba na Rais wa Uturuki, hawa muda wote wanataka kuwe na mazungumzo zaidi ya Vita.
Hawana haraka wala kelele nyingi. UK, GERMAN wao wanawaza sana VITA, hata NATO hao ndio viherehere.
 
Kwanza kbs napenda kutanguliza salam kwa wana JF wenzangu hapa jukwaani, pili naomba mods msiuunganishe huu uzi na uzi wowote unaohusiana na mambo ya Ukraine maana kila mtu ana uwasilishaji wake wa taarifa hapa jukwaani, so kuuchukua uzi wa mtu ambae kila siku anatumia data zake, muda wake, fikra zake na energy yake kuchangia comment mbali mbali au kuandika thread mbali mbali afu kwenda kuunganisha na uzi wa mtu mungine bila taarifa au sababu za msingi ni kuingilia uhuru wa watu kutoa maoni yao hapa jukwaani. Kwahiyo mwisho wa siku mtajenga hofu na uoga kwa wateja wenu, maana mtu atajua akileta uzi hapa kwa ajili ya kuhabarisha umma kuhusu yanayojiri huko duniani mods watauchukua huo uzi wake na kuupeleka sehem wanayojua wao bila idhini yake ili kupoteza maana ya kile alichoandika hapa jukwaani. So nina imani mods mtazingatia ushauri wang huu niliowapa. Tuje kwenye mada husika. Ndugu zangu kitendo cha raisi wa Russia kuomba poo ya mazungumzo ya kumaliza mapigano kati ya jeshi lake linalosifika kuwa na nguvu zaidi duniani baada ya lile la Marekani, kimewashangaza wengi waliokuwa wakimuunga mkono mbabe huyo na jeshi lake. Wakati akijiandaa na uvamizi, wengi wa wapambe wake walitegemea uvamizi wake ungechukua usiku mmoja tu kumaliza kile alichoita safisha safisha ya viongozi vibaraka wa magharibi. Sasa anashangaa pamoja na ukubwa wa jeshi lake, wingi wa silaha zake, na ukubwa wa nchi yake ameshindwa kutwaa hata miji mitatu tu mikubwa, badala yake yeye ndo amekuwa akirudishwa nyuma na kunyang'anywa mji wa pili kwa ukubwa ambapo hapo awali jeshi lake ndo lilikuwa linaumiliki. Bila shaka Putin ashasoma alama za nyakati baada ya kunusa ule mtego wa Marekani ambao waliutega kwa lengo la kupata sababu ya kuingia kijeshi kuiadhibu Russia kupitia katika ardhi ya Ukraine. Ikumbukwe Marekani na genge lake la NATO walisema hawawezi kuingia vitani kuisadia Ukraine kwani sio mwanachama wao kamili wa NATO. Ila nyuma ya pazia Marekani alikuwa anapanga mpango wa kurushwa kombora moja tu la Russia nchini Poland ambae ni mwanachama wa NATO ili watemi hao wa dunia waweze sasa kuingia kazini live bila kujificha kwa kisingizio kuwa Russia ndio ilianza uchokozi wa kumshambulia mwanachama mwenzao wa NATO (Poland) Silaha kubwa kubwa zimekuwa zikitumwa Ukraine usiku na mchana kwa kisingizio cha kuipa msaada wa silaha Ukraine, kumbe wakubwa hawa wanaziandaa kwa ajili ya kwenda kuzitumia wenyewe hapo baadae baada ya mipango kukamilika. Mimi na wewe hatujui hilo kombora lingerushwaje rushwaje ili mission yao ikamilike kuingia mzigoni. Wangesubiri kombora la Russia likosee njia na kuangukia kwa mwanachama wao? au wale wale askari wa Ukraine wangetafuta njia ya kupata kombora la Russia na kulivugumiza nchi yoyote mwanachama kinyemela ili msala umuangukie Putin? Pongeza kwa Putin kwa kuliona hili mapema na kuwahi kuomba poo before mambo hayajaharibika, maana Mmarekani na genge lake sio watu wazuri hata kidogo. Kweli unaweza kujikakamua kupambana nao lkn mwisho wa siku wewe ndo utaanguka miguu juu. Mungu aepushe mbali vitaa hii, ili dunia iwe sehemu salama ya kuishi kwa amani.
Mbn hujui hatakuandika sehem kubwa umeandika kwa mihemko ya bangin, wapi putin kaomba poo nawac wac hata history ya dunia hauijui wewe ndio maana unakuja na bla bla kibao
 
Duuhh hivi Siasa za Putin umeanza kuzifatilia baada ya hii vita kuanza???

Angekua na hayo mawazo, asingeingiza majeshi Ukraine.

Ikama ambavyo Alipeleka Majeshi mipakan mwa Ukraine kisha akataka NATO wakubaliane na matakwa yake, NATO ikagoma, akapata sababu ya kupiga Ukraine.

Na sasa ivoivo, kwenye hayo mazungumzo ,ataendelea kuweka matakwa magum kwa UKRAINE wenyewe , ili wakijifanya wanaamriwa na NATO , jamaa apate sababu nyingine ya kuwapiga mpaka aweke Rais wake anayemtaka.
 
Inshu kama hyo sio lazma serikal ihusike Moja Kwa Moja... Sekta binafsi ipo wangeshirikiana na seeikali tu..
Sekta binafsi ipo profit oriented. Watataka misamaha ya kodi kwenye biashara zao n.k gharama inarudi kule kule tu. Unless useme in time being serikali isikusanye kodi yoyote kwenye mafuta.
 
Back
Top Bottom