LIVE Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

LIVE Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Live coverage on JamiiForums
URUSI anatembeza kichapo, UZI umekimbiwa na wale PRO-NATO ngozi ya TAKO
Ni Vile tume subiri. 2 powerful military iichukue kiev hadi tume choka bwana putin kasha data
449152199.jpg
 
Urusi kaanza kurusha cluster bomb huko kyim mji utabaki magovu muda mchache ujao
 
Ila katika mazungumzo hayo shurti mabeberu wa ulaya na Amerika washiriki ili wajue kwanini waliemchuuza kapewa kichapo🤔
Unaweza kuta mabeberu hawajali kichapo anachokula ukrane, ukute kuna mambo yao tu wanapima na wasingeweza bila urusi kupigana, sasa wanafanikiwa na wanapata na bonus ya adui yao kupata vikwazo.
 
Hajamaliza kazi tu Putin? Bado yu ngali apiga?
Hii vita ya Russia na Ukraine inanikumbusha lile pambano la Lenox Lewis na Hashim Rahmani lililofanyika Afrika kusini miaka kadhaa iliyopita. Katika pambano lile Lewis alionesha dharau ya hali ya juu kwa Hashim, mpaka akafikia hatua ya kulilaumu shirikisho la ngumi duniani kwa kumpambanisha na chekechea (hashim) ambae angeweza kupambana na watoto wenzake huko mitaani. Wakati wa kuingia ulingoni (kabla ya pambano) Lewis alimsogelea Hashim akamuuliza unataka nikutwange ktk round ya ngapi.. ya kwanza, ya pili au ya tatu? Alipoulizwa swali hilo Hashim hakujibu kitu, basi Lewis akamwambia kwa vile dogo wewe ni jeuri, nakuahidi kukuadhibu katika round ya pili tu ili niwahi kwenda kupumzika na familia yangu. Basi pambano likaanza kila mtu akionesha hofu kwa kipigo kibaya atachopata Hashim kutokwa kwa Lewis. Hee kufumba na kufumbua Lewis akajaa kwenye himaya ya Hashim huku akiwa kasahau kulinda chaga (mbavu), Hashim hakutaka kuipoteza hiyo nafasi, akaingia na left hand kuichokonoa chaga ya adui, Lewis baada ya kuhisi chaga zake zimechokonolewa na dogo ikabidi ashushe gard kulinda chaga huku akiwa kasahau kabisa ulinzi wa sura, dah dogo akapata nafasi ya kucheza na sura ya mtu mzima kama vile achezavyo na panch bag. Mara mtu mzima Lewis chaliii, refa anahesabu mpaka kumi Lewis kalala tu kama gogo, dogo Hashim ikabidi apewe ushindi mnono wa nock out. So hata hii vita isije kuwa kama lile pambano la Lewis (urusi) na Hashim (ukraine) tukaja kusikia mtu mzima kazimishwa ugenini na mdogo wake.
 
Tatizo hawa Euro na west kwa ujumla sitaki kutumia neno unafiki ila kuna kitu wao wanadhani wao ni superior kimawazo kuliko watu wengine wote na wamestaarabika kuliko watu wote hapa ndio tatizo. Maisha yao ni ghali kuliko maisha ya wengine na lazima waungwe mkono hata zile tasisi ambazo kwa miaka hawakutia siasa katika michezo kama FIFA na OIC wamewashurutisha mpaka wamachagua upande. Mtu yoyote akienda kinyume na mawazo yao huyo mbaya wanahubiri democracy lakini ni hawa hawa wakati Hamasi wameshinda vote wakaleteta fitna wakatolewa hapo Egypt alishinda uchaguzi Morsi yaliyotokea tunajuwa. Ok ni kweli Hamasi ni wabaya hilo halina ubishi lakini si wamepigiwa kura? Morsi alishinda lakini kwa kuwa hakubaliki na wao wakamtoa na mwisho kufa. Kama ndio hii safari tumeanza kama yake ya Bush either uko na sisi au na wao hakuna netral ndio tunaambiwa. Uhuru wa kuongea ndio nyimbo zao leo hii wanafunga media mpaka internet ili watu wasiongee. Nadhani uhuru wanaohubiri ni ule wanaoutaka wao kutaka mila zao lazima tuzikubali maana wao ndio civilized sisi wengine mapaka tu hatuna ustaarabu. Hakuna sehemu walitia mguu kukawa na mafanikio sio Libya, Iraq hata Syria wameacha majanga kwa watu.
 
Back
Top Bottom