LIVE Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

LIVE Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Live coverage on JamiiForums
Leo tarehe 2 march 22 tunamaliza kazi labda tutachelewa kuwatangazia tu ila mchuzi wote tunakunywa leo na bakuli litatupwa leo ila sijajua mlio wa kudondoka kwa bakuli
utachukua mda gani kukufikia hapo ulipo.
Nakukumbusha tu Zelenskyy yupo Poland mafichoni.
Sawa, Ila usilete janja janja la kusema tayari ila hatutangazi tukashangaa siku zinapita tu.
 
Leo tarehe 2 march 22 tunamaliza kazi labda tutachelewa kuwatangazia tu ila mchuzi wote tunakunywa leo na bakuli litatupwa leo ila sijajua mlio wa kudondoka kwa bakuli
utachukua mda gani kukufikia hapo ulipo.
Nakukumbusha tu Zelenskyy yupo Poland mafichoni.
leo sidhani raia ndo siku yao ya kuondoka huko Ukraine baada ya hapo ni booóó
 
Mkuu hebu fikiri kwanza kabla ya kuandika. Unaposema Marekani na NATO washa surrender bila kutuambia wame surrender kivipi ina maana gani? Je kuna mmoja wao alivamiwa kati ya Marekani au NATO? Kama hakuna alievamiwa kati ya hao niliowataja unawezaje kusema wame surrender? Kama ulivyoandika hapo juu kuwa sheria au mkataba wa NATO na baba yao Marekani unaruhusu nchi hizo au umoja huo kuingia vitani pindi tu mmoja wao anaposhambuliwa, je Ukraine ni mmoja wa wanachama wao? Jibu hapana sio mmoja wao, na kama sio mmoja wao, unawezaje kusema kuwa wame surrender? Ukweli ni kwamba Putin mwenyew anaiogopa NATO ndio maana ameacha kuzishambulia nchi za NATO ambazo zingine zipo mlangoni kwake (hapa nazungumzia nchi zile za nato anazopeana nazo mpaka) na badala yake kaenda kuishambulia Ukraine ambayo haina uanachama wa umoja huo. Kama lengo ni kuzuia silaha hatari na upanuzi wa NATO katika eneo hilo, kwann kaishambulia nchi ambayo sio mwanachama, na kuacha kushambulia zile ambazo ni wanachama halisi tena zenye majeshi na silaha hatari za NATO karibu yake? Hii ni sawa na kwenda kumkamata mtoto wa jiran yako, eti kisa rafiki yake (ambae pia ni jirani yako) amekuibia kuku wako. Russia anajua fika kuwa Ukraine sio mwachama wa NATO, kwahiyo uvamizi wake hauwezi kuigusa Marekani moja kwa moja, au kuleta madhara yoyote kwa NATO. Angethubutu kufanya hivyo kwa nchi yoyote ya NATO iliyo jirani yake bila kuchukuliwa hatua, hapo ndo tungesema jamaa kweli ni mwanaume. Nakutupia ramani hapo uangalia nchi ambazo zina jeshi kubwa na silaha hatari za NATO tena zinapeana mpaka kabisa na Russia lkn jamaa hakupima kuzivamia kuharibu silaha zao kama anavyodai kwa upande wa Ukraine.

View attachment 2136053
Estonia wapo jirani kabisa lakini hawezi kugusa moto yeye sio mjinga, hata mabwenyenye wa urusi maarufu kama oligarchy wameanza kumkataa
 
Tatizo ni akili finyu mulizonazo, tunapoongelea maisha mazuri tunaongela kwa kigezo cha HDI human development index, ambayo inahusisha educational systems, healthcare, employment, education nk. Sasa niambie nchi yako imeweza kwenye nini hapo? Kama dishi limeyumba tafadhali usijibu chochote, kama una hoja niambie hapa.
WEWe ndiwe unatembea na dish,halafu matusi ni kiashirio cha kuishiwa hoja,Tanzania ni moja ya nchi zenye maendeleo katika nyanja zote ulizozitaja hapo labda mtu ajifanye haoni ndiye atakaebishana kuhusu Hilo,mfano Marekani standard ya elimu Yao watu wanadhani Iko juu lakini hebu angalia elimu yenyewe kama inawasaidiaje kuondokana na matatizo yao ya mass shooting,racism,matumizi ya madawa ya kulevya n.k.
 
Tunawasubiri wazee wa 'Putin anakiwasha" walitwambia leo ni deadline kiev inakuwa majivu,naona wanasubiri Putin afanye yake ili waje hapa kama nzige kuvamia
🤣 🤣 🤣. Kwamba wapo chimbo
 
leo sidhani raia ndo siku yao ya kuondoka huko Ukraine baada ya hapo ni booóó
Nimesema leo ndio tunamaliza game ila taarifa watu watazipata kesho. Wanachofanya Ukraine na sengefu wake USA ni kitu cha kitoto sana mfano academy unaifunga goli 10 bila alafu msemaji wao anasema wao walikuwa wanaangalia zaidi pasi na kuonana kwa wachezaji uwanjani na sio kupata goli. Watapata tabu sana mwaka huu na tukiwamaliza hawa tunawaendea nchi zikizotuwekea vikwazo nako moja moja tuna chukua. Kwa sasa tumejua kuwa tunaogopwa hivyo wakimbie mbali sana maana ndio kwanza tumeanza A.
 
Estonia wapo jirani kabisa lakini hawezi kugusa moto yeye sio mjinga, hata mabwenyenye wa urusi maarufu kama oligarchy wameanza kumkataa
Urusi ni sawa sawa na mtu mzima alieibiwa kuku, afu anaenda kumalizia hasira zake kwa mtoto wa jirani yake eti kisa tu huyo mtoto wa jirani ana urafiki wa karibu na dogo alieiba kuku ambae pia ni jirani ya huyo mtu mzima. Sasa hapa mwenye akili utajiuliza ni kwann mtu mzima kaenda kumwadhibu innocent child wa jirani yake na wakati muhusika alieiba kuku wake anamfahamu tena anaishi jirani yake. Jibu ni kwamba mtu mzima kaogopa kum face dogo alieiba kuku eidha kwa kuhofia kipigo toka kwa baba wa huyo dogo, so akaona njia ya kufikisha ujumbe wa kuibiwa kwake ni kum target dogo mungine ambae ni yatima na kumalizia hasira zake zote kwake.
 
NATO wanaogopa sana vita na Urusi, na kwa kuwa Ukraine siyo mwanachama wa NATO basi wamepata kisingizio.
Nimeona eti wanatoa msaada wa MIG 29! huu ni utani wa hali ya juu. Kwa silaha za kisasa ndege hizo zitapigwa zote, ni za kizamani mno. Huwezi kumpatia askari wa kimarekani ndege hiyo airushe kwenye vita - ataona humpendi na unamtafutia kifo.
Bongo sihami jamani kwa ujuaji huu, ungetuletea technical specifications zake angalau tukajua kuwa MIC 26 hazina uwezo wa wakumudu uwanja wa Medani
 
Russian delegation left for meeting point with Ukrainian delegation - BelTA correspondent
SmartSelect_20220301-220358_Gallery.jpg
 
SmartSelect_20220301-220358_Gallery.jpg


The Russian delegation is heading to Belovezhskaya Pushcha for negotiations
 
Karudi kwenye historia yako. Watu kama nyie mnakera sana, yani unadai nisome historia na wewe uliyeisoma unapotosha. Wapi ambapo Russia au USSR aliikomboa England (ambayo sio hiyo, unamaanisha Great Britain or United Kingdom kama umejumuisha Northern Ireland). Hakuna mwanahistoria hata awe anapata zero darasani ataiita GB au UK eti England, huu sio mpira wa FIFA.

At least ukiniambia USA au British waliikomboa Europe nakusikiliza. The British empire na commonwealth zilitangaza vita mwaka 1939 pale Hitler alipoivamia Poland. Hitler hakuwa ametangaza kuivamia Britain mpaka alipovamiwa nao. Hitler alikuwa anashawishiana na Britain iungane na Ujerumani ili baadae aigeuke. Britain siku zote wako next level kwenye matumizi ya akili wao ndio walifanya declaration of war dhidi ya Nazi Germany na wakaiambia.

On the other hand, USSR chini ya Stalin Ilikuwa na mkataba na Ujerumani ulioitwa Molotov-Ribbentrop Pact wa mwaka 1939. Vyacheslav Molotov huyu huyu wa Molotov cocktails alikuwa Foreign Minister wa USSR. Hiyo non-aggression pact ilisema wasiingizane vitani. Germany ikapiga Poland KWA KUSHIRIKIANA na USSR, USSR walidai eti wanaisaidia hii Ukraine na Belarus eti walikuwa wanaonewa na Poland. USSR iliua maofisa wa Poland maelfu wa kijeshi kwenye Katyn masacre ambapo maofisa wa kijeshi na wanausalama 22,000 waliuwawa na USSR.
Britain ikatangaza vita dhidi ya Germany. Germany ikapiga France kwa kuwa Britain iko karibu nao basi watatumia Ufaransa watume ndege zao na meli kuvamia Uingereza.

Ufaransa ikaanguka kwa haraka hata mwezi haikukaa, walikuwa na maofisa wajinga sana hasa ndio tatizo. Uingereza ikawa yenyewe tu hapo Ujerumani ina Italy kwa Mussolin. Mwaka 1941 Hitler akaona Uingereza haijajipanga sana na haiwezekani ijipange akaamua aivamie USSR kwa haraka, hapo ni baada ya USSR kuonesha udhaifu ilipovamia Finland wabishi sana hawa. USSR iliamini mkataba ule na ikashtukizwa. Marekani kutokana na Pearl Harbor attack ndio akatoa supplies na nguvu dhidi ya Ujerumani.

Nimezunguka sana kukwambia hivi: Russia/USSR hakuisaidia Europe, alijitetea mwenyewe maana mwanzo tu alikuwa ashakubaliana na Ujerumani. Kama Hitler angesikiliza majenerali wake asingevamia two fronts at the same time na Russia isingepigana kukomboa Ulaya. USSR asingepigana na Ujerumani angepotezwa, walifikia hatua ya kubakiza 20km kuifikia Moscow, walipigana battles kama Stalingrad na Kursk mamilioni ya vifo yakatokea.

Na hatua ya mwisho kulikuwa na scramble nani afike Berlin wa kwanza aitwae nchi. Washindi waligawana nusu ya Ujerumani kisa hawakuwa wanaaminiana hata pale Yalta conference. USSR iliitaka Kaliningrad enclave kwa sababu hizi hizi za kushtukiana. Wote walikuwa washajipanga kwa possibility ya kuendelea na vita nyingine baada ya Ujerumani.
Hongera unaijua history vizuri, USSR hatasahau alichofanyiwa na Finland
 
Kama nilivyowahi kusema katika mada na michango yangu ya huko nyuma, lengo la Russia ni kuiondoa madarakani serikali ya Zelenskyy na kuirudisha serikali itakayosikiliza Russia.

Russia yaandaa mazingira ya kumrudisha alekuwa raisi wa Ukraine ambae aliondolewa kwenye mapinduzi ya 2014.

Kiongozi huyo wa zamani wa Ukraine wana Vicktor Yanukovych kwa sasa yupo nchini Belarus akisubiria "go ahead" baada ya Ukraine kuwa chini ya majeshi ya Russia.

Ili Ukraine iwe chini ya majeshi ya russia kikamilifu ni pale majeshi hayo ya Russia yawe huru kutembea mitaani, kurudisha huduma zote muhimu, kuongoza vituo vya mawasiliano, kijeshi na pia kuongoza magari mabarabarani.
Daah hatari sana
 
News from the world of gaming:

Users from Russia report problems paying for purchases on Steam and the Playstation Store.

Also, from insider Tom Henderson, information appeared that EA Sports plans to remove the Russian national teams from FIFA and the NHL.
SmartSelect_20220301-220358_Gallery.jpg
 
Back
Top Bottom