LIVE Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

LIVE Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Live coverage on JamiiForums
Aliyekuambiwa Ukraine kuna vita nani, Ukraine kuna operation tu ya kijeshi tu, naweza kusema ni operation ndogo sana. Ulishawahi kuona vitani pande zote wanaomba kusimamisha mapigano kwa ajili ya jambo jingine?
Huna akili pathetic!!
 
Hivi vita haviwezi kudumu kwa muda mrefu kwani Russia na vikwazo vikali walivyowekewa hadi Putin amelalamika kwamba ni "Declaration of War" hawawezi kuendesha vita kwa muda mrefu.

Miezi mitatu tu ijayo tayari uchumi wao utakuwa taabani na wananchi watakuwa wanaandamana kudai majeshi yao yaondoke kwenye ardhi ya Ukraine. Kumbuka asilimia 85 ya warusi wanapinga hivi vita.
 
Makampuni kama Lockheed Martin na Boeing yamekuwa yakipata hela nyingi bila sababu za msingi. Marekani ina warmongers wanatishia serikali kwamba kuna threats hivyo military spending iongezwe na silaha kali zitengenezwe mwishoni wanakuja na vitu kama F-35 Lightning II na F-16V. Wakati Uturuki ina drones na Israel ina loitering munitions zinafanya majukumu effectively dhidi ya silaha za Urusi. Mara ya kwanza Israel iliposhambulia Syria tulisema operators wa Syria wako incompetent na silaha za Syria ni weak sio superior, mara ya pili Libya tukasema waliopewa silaha ni insurgents hawana training nzuri na discipline, ikaja Nagorno Karabakh tukahisi labda walishtukizwa na hawana quantity inayotosheleza, tukaja Uturuki iliposhambulia Syria tukasema vilevile. Sasa Urusi yuko anatumia silaha zake mwenyewe
 
Ila mkuu bado hujajibu swali langu je unadhani kweli mpaka sasa Ukraine imesha zitungua ndege 88 za Urusi? Au ni propaganda.

Sent from my TECNO BB4 using JamiiForums mobile app
Wala hata nusu ya hizo siwezi kubali kama wamezitungua. Napenda nione crash site, rubani au footage. Ukrainians wamejaza smartphones uwanja wa vita wanapiga na kujirekodi, vita haiko baharini kwamba ndege zimeondoka na kupotea. Urusi ndio wamebanwa na mainstream media taarifa zao hazifiki kwa wengi
 
The Ministry of Defense showed Ukrainian military documents that came to the department during a special operation.

They belong to the 4th operational brigade of the National Guard of Ukraine, located in Gostomel, Kiev region. Among the papers are maps and plans for combat use.

In addition, orders were at the disposal of the RF Armed Forces that indicate close cooperation with NATO structures and the practical training of the National Guardsmen by NATO.

IMG_20220306_150147_499.jpg


IMG_20220306_150147_670.jpg


IMG_20220306_150147_056.jpg


IMG_20220306_150146_729.jpg


IMG_20220306_150147_125.jpg
 
Haaaaa wengi humu huwa wana ongelea mambo ya kitaalam kwa Utashi wao na mizaha mingi.
Usiyachukulie maanani.

Katika dunia ya sasa hakuna taifa unalo weza kulishinda kwa siku mbili hata jeshi letu huwezi kulishinda kwa siku mbili.

Sent from my TECNO BB4 using JamiiForums mobile app
Walau wewe Mkuu unasimama katika ukweli,kwa hili nakubaliana na wewe upo sahihi.
 
Nimeshangaa kwa urusi kutuma wanajeshi wasio na uzoefu na wengi wao hawajaambiwa kuwa wanaenda kupigana Ukraine.
Pia sijaona s400 hata moja.
S-400 hazipo kwa ajili ya jeshi kama Ukraine, lile hata S-300 inalizidi uwezo. Ukraine inafanya ambush ya silaha za Urusi hakuna kamanda atafanya mchezo kusogeza S-400 zikamatwe Wamarekani waje mbiombio kuzisoma.

Zile Buk pekee zinatosha kuiweka Ukrainian airforce nje ya anga
 
Marekani walipovamia Somalia, wanajeshi wao waliuawa na kutembezwa mitaani jijini Mogadishu, kwenye vita, hata uwe na nguvu kiasi gani casulties haziepukiki
Marekani alipeleka Blackhawk helicopters sijui mbili na armoured vehicles chache akiwa na kaoperesheni kadogo sana. Russia kaja na misururu ya magari ya jeshi inazidi urefu wa kilomita barabarani. Yani unaenda Maxar unapewa picha za satellite za misururu ya kijeshi ya Russia, kazingira pande tatu za Ukraine
 
Tukiachana na nuclear weapons, siwezi panga majeshi bora ya conventional weapons Urusi ikawepo kwenye top 4. Huwezi kuwa na jeshi la ovyo la ardhini na angani linaposhindwa kupigana na vijeshi vidogo kama Ukraine alafu unataka tukuite superpower kwenye majeshi. Ujerumani kwenye WW2 ilipigana na Poland, Ufaransa, Urusi, Marekani na Uingereza ikiwa pamoja na Commonwealth zake zenye nchi imara kama New Zealand, Australia na Canada, et. Hata South Africa ilishiriki dhidi ya Mjerumani, hao ndio walikuwa na jeshi la kupigana na maadui wengi sio hii Russia.

Huu uzi nimeutelekeza kwa siku tatu hizi baada ya kuona kile ninachokijua kimezidi kupwaya. Jeshi la anga la Urusi ndio la kufanya mashambulizi usiku ili lisidondoshewe ndege zake kweli? Juzi ndege 6 ziko confirmed kuangushwa, source zipo nyingi za kudhitibisha hilo na ndege ambazo hakuna uhakika hazijahesabika. Wiki ya pili sasa bado Ukraine imesimamisha S-300 zinafanya kazi. Ingekuwa Israel siku ya kwanza tu, trust me siku ya kwanza tu hakuna air defence system ungeona iko kazini!

Urusi inashindwa kulinda convoy zake, inapaki magari kibao mpakani kule Belarus ila inaogopa kuingia nayo mengi ziko Bayraktar TB2 zinayasubiri, hawana air cover wanaenda as if tuko 1980s. Urusi wana systems zao kama S-300 (S-400 si rahisi ikaletwa kufanya kazi ndogo hizi) ziko mbali uko kwao ambavyo wala Ukraine hana mpango wa kuishambulia Urusi hivyo zinatoa air cover mpaka pembeni mwa Ukraine ila nao wanaendesha ndege level za chini kukwepa radar.

Russia haina coordination nzuri ya airstrikes, artillery na troops. Hata airforce yao haina uzoefu na combat missions, Urusi wako busy na kuendesha ndege kwenye maonesho na kwenye mazingira rafiki wakati NATO wanakuwa na mazoezi magumu yanayofanyika kwenye maeneo tofauti duniani kama Mediterranean sea, Marekani na maeneo ya Ulaya. Marubani wa UK na US hukutana kufanya mazoezi magumu kila mwaka yanaitwa 'Red flags', hutumia makombora ya kisasa, ndege za kisasa na hutumia hali ya hewa mbovu kwenye mvua kubwa, fog na upepo. Last year mwishoni hapo kuna F-35 mpya ya Uingereza ilidondokea kwenye maji wakiwa kwenye mazoezi makali na Marekani. Marubani wa NATO wana simulation rooms za kisasa zinazofanana na mazingira halisi ya vitani, rubani anapewa simulator inayofanana kila kitu na ndege yenye hata VR anazoea mazingira, buttons, emergencies, maamuzi ya haraka. Hata movements za ndege, acrobatics na mitikisiko anapewa anachokosa ni ile hofu inayotofautisha mazoezi na reality. Russia hana kampuni ya kutengeneza modern simulators marubani wake wana disadvantage hapa. Marubani wa Russia wakifanikiwa sana wanatimiza masaa 100 ya kurusha ndege kwa mwaka wakati Marekani na members wakubwa wa NATO wa kwao wanazidi masaa 200 kwa mwaka.

Ndege za Urusi zingekuwa mbovu India isingekuwa inazitumia vizuri na kushinda angani, tena India iliwahi fanya mazoezi na members wa NATO wakakubali sana uwezo wake. India ndio airforce inayoongoza kupata ajari, wale jamaa hawakai miezi miwili bila ndege ya jeshi kuanguka, kamanda wa jeshi la anga alidai bora wafanye mazoezi kwenye mazingira magumu wafe kwenye wakati wa amani ila vita ikija wawe strong wafanye mission kwenye mazingira yote.

Hapa tatizo ni training mbovu isiyokidhi, na washirika wa Urusi hawafanyi mazoezi pamoja. Russia inafanya mazoezi na India, China kidogo sana na watu wa kawaida kama Belarus. NATO wanaunganisha mbinu za wageni kama South Korea, Japan na Israel which I think ndio airforce inayojua sana air warfare kuliko hapa duniani. Israel imeanza operations Syria miaka zaidi ya 10 na sijawahi sikia imepoteza ndege hata moja. Leo hii Urusi ndani ya wiki mbili ana hasara kibao angani.

Hhahahahah nimecheka sana. Mnamchukulia sana poa russia, endeleeni kudanganyana wengi humu hamumjui russia vizuri na wengi wameanza mjulia kwenye vita na ukraine hamjui historia yake vzr huyu jamaa.
 
Kosa vp ikiwa katengwa na dunia na nani atamwekea vikwazo ikiwa ametengwa
Ni kosa na yeye analijua hilo na hawezi hata kuthubutu kutengeneza Soda akaiita COCA,pamoja na arrogance ya Putin lakini hajawa mjinga wa kufikia kufanya hili.
 
propaganda ni sehemu ya vita kumbuka urusi inapigana na ulimwengu ukiangalia hizo picha unaweza sema urusi haiteka hata kijiji lakin mbona warusi hapig picha wanajeshi wa ukraine walio uwawa mbona madhara ya vita yanatolewa na waukraine hapa wanataka attension ya raia wa urusi waandamane kumpoa putin. Ndo maana putin kacheza game la hio sheria huyu mwamba ni zaid ya genius
yeah ni kweli zile ni propaganda za waukraine but ukweli ni kwamba wanatumia video na picha halisi za russia casualities ambazo ht urusi mwenyew hadispute so hii sheria pia imedhamiria kuzuia watu wa urusi kujua hali halisi ya kinachoendelea ukraine,duh mkuu urusi inapigana na ulimwengu wote??mambo yameshafika huko?
 
sasa kwanini urusi imezidi kusonga mbele wakati ukrein ina zana za kuzuia vifaru ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha
Imesonga mbele wapi zaidi ya ivyo vimji viwili vya mpaka na ule mmoja mlikuwa mmeuteka na ikakombolewa sasa ivi mpaka airport mliyokuwaga mmeiteka ile siku ya kwanza ya vita tayari imeshaa kombolewa na jeshi bora la Ukrain na sasa umerudi kwenye umiliki halali wa serikali ya Ukrain

Kifupi jeshi lenu ni dhaifu sana sana halina ubora wowote ni kaMa majeahi yetu uku Africa jeshi halina nidhamu ata kidogo jeshi halina formula, jeshi liko disorganized kama vile kuku waliokatwa vichwa alafu uje kuniambia kiwa kuna jeshi apo jeshi linaishiwa mafuta , jeshi linaishiwa mpaka chakula , jeshi la hovyo zaidi kuwahi kutokea katika karne hii ovyo kabisa putin na wafuasi wake
 
Back
Top Bottom