FaizaFoxy
Platinum Member
- Apr 13, 2011
- 100,246
- 123,145
Hizo zote zingine porojo. Mimi si wa kuamua nani mwenye dhambi na nani hana dhambi.Faiza sijui habari zako unapata wapi.
1. Ni Ukraine walioomba tangu miaka 20 kujiunga na NATO na hawakupokelewa hasi sasa. Je nchi ndogo haina madaraka kuchagua inapopendelea kujiunga (hata kama haapokelewi)?
2. Dhambi za Marekani ni dhahiri. Dhambi za Urusi hupendi kuona? Vita yake dhidi ya Waislamu kwenye Kaukazi (pamoja na Chechniya), kushambulia Afghanistan, zamani Chekoslovakia, Hungaria? Vitisho dhidi ya mataifa ya Ulaya?
3. Putin kusema eti Ukraine si nchi, haistahili kuwa nchi huru - ukimkubali je unaona Tanzania ni nchi? Kwa nini? Ukikubali uhuni wa Putin, basi hakuna nchi ambayo ni salama.
4. Hadi sasa naona hakuna aliyeshambulia Urusi tangu miaka 80, lakini Urusi imeshambulia nchi kadhaa. Sasa Ukraine.
Haiwezi kuwa dhambi kwa mmoja basi kwa mwengine ikawa si dhambi.