Mwanamkiwi
JF-Expert Member
- Mar 7, 2019
- 2,023
- 2,402
Si vile, mambo ni tofauti kidogo. Kati ya nchi inazouza silaha nyingi duniani kuna ufuatano huu:Yeah Saudi blah blah but US na UK huwezi kuwatoa hapo ndio wasambazaji wakubwa wa silaha na misaada mingine
1. Marekani
2. Urusi
3, China
4. Ufaransa
wanofuata ni Ujerumani, Uingereza, Hispania na Italia.
Si ajabu kwamba nchi zenye nguvu ya kiuchumi na viwanda vingi zinazalisha pia silaha nyingi na kuziuza nje. Urusi iko kidogo nje ya mantiki maana tasnia yake ni dhaifu kiasi kimataifa, ila inauza silaha nyingi kupita cheo chake kati ya wazalishaji bidhaa duniani. (uchumi wa kitaifa wa Urusi hutazamiwa tofauti kadri unavyochagua kipimo gani; lkn. utajiri wake ni zaidi mafuta na gesi, si uzalishaji nje ya hayo)
Kwa nchi ambayo raia wako kwenye nafasi ya 92 tu kimapato duniani, inaweka mkazo mkubwa sana kwenye jeshi na tasnia ya kivita. (yaani nchi 91 raia huwa na mapato mazuri zaidi kwa wastani kuliko Urusi)