Kitendo cha Russia kuziponda ponda hizo Patriot Air defense batteries kimewadhalilisha na kuwanyong'onyesha sana US and its allies.
Zile Tambo zote zimekwenda na maji.
Zile tambo zote zimekwenda na maji.
Hakika kabisa Mkuu Nkuba 25.
Watu wasiopenda kujishughulisha kutafuta uelewa wa mambo ya ziada humu walidanganywa,walipotoshwa na waliaminishwa sana kua Urusi ni maskini na dhaifu sana mbele ya west.
Kumbuka nikisema west ndani yake yumo USA,NATO na wasio NATO.
Kuna watu humu Sasa hivi wote wamekimbia walikua wanaandika Kila aina ya mashairi na wengi wakawafuata kua USA ndio Kila kitu.yaani baada ya Mungu wanafuata wao.
Waliandika Kila aina ya udhaifu wa silaha za Urusi na kusifia Kila aina ya ubora wa silaha za west,lakini kwa bahati mbaya uhalisia umetokea kua hauko katika upande wao.
Kuna mtu humu alijaribu hata kuponda jeshi la Urusi eti kua havutiwi kabisa na upiganaji wa jeshi la Urusi,mara wanajeshi wa Urusi hawana nidhamu na Kila aina ya kashfa,utadhani yeye ndio mkadiria ubora wa majeshi yote Duniani.
Lakini pamoja na kashafa zao zote utashangaa majeshi ya Urusi yanaendelea kuteka maeneo na kuangamiza silaha na askari wa NATO.
Kwa kifupi Urusi imewaprove wrong wote waliokua wanaiponda.
Kwa kifupi Urusi imewadhalilisha sana USA na NATO yake,maana USA na wenzake wamepeleka silaha za Kila aina na mashabiki wao wakawa wanaziita game changer,lkn Kila zikija zinazimwa vibaya sana.sasa Urusi wanaisubiri F16.
Kuna watu humu waliamini na kuwaaminisha wafuasi wao kua USA Ina mipango thabiti kabisa,mipango ya kuona miaka 100 mbele,waliamini kua na kijinasibu kua Urusi ilikua inatafutwa sana na safari hii imeingia mtegoni na haitatoka,Kuna watu walisema kwa uhakika kabisa kua Kuna nchi zilikua zinaitamani sana Urusi na Sasa imeingia kichwakichwa,eti ki nchi kama ki Poland kua kinaitamani Urusi.
Maneno mengi sana yalisemwa kuonesha kua Urusi itakoma mwaka huu na kua eti USA imeshapanga mipango yake ya kuiangamiza Urusi,na kua eti USA Ina akili sana Kwa mipango.
Lakini kwa hakika USA imeingia Chaka la kufa mtu, na tayari imeshajichimbia kabiri lake yenyewe.
Kama Kuna kosa kubwa USA amefanya,ni kutengeneza vita hii,alidhani anadili na Libya au Zimbabwe,lakini kwa upofu wake hakujua anadili na taifa lenye akili mara kumi kuliko yeye.
Kosa la kwanza kubwa la USA ni vita hii.
Vita hii imezifanya nchi zote adui na USA kua pamoja na Urusi,
mfano Korea kaskazini,Iran,china n.k.
Ila kosa kubwa kabisa ni Urusi kuangukia mikononi mwa china.Hapa ndio mwisho wa mchezo.Ushirika huu ni janga Kwa USA.
Kosa la pili.
Baada ya smo hii ambayo ni miujiza TU ndio itabadili upepo wa ushindi wa Urusi.
Baada ya vita hii NATO inaenda kupoteza ushawishi.
Kosa la tatu.
USA inaenda kupoteza kuogopwa.
Hapa hata haisubiri kuisha vita,kwani Tayari Niger,Mali na siera Leone wameshaacha kuiogopa USA na hata kufikia kuifukuza nchini mwao.tutarajie wimbi hili kuendela sehemu mbalimbali duniani.
Kosa la nne
Soko la silaha za USA kupungua na soko la silaha za Urusi kupanda.
Hii itaupandisha juu uchumi wa Urusi na kuiongezea konfidensi zaidi Urusi.
Tano
USA haitakaa ivamie nchi yoyote Tena kama ilivyofanya kwa Iraq, Afghanistan,Libya na Yugoslavia kwa sababu Urusi itaisaidia waziwazi nchi hiyo, ili kuiadhibu USA, Kwa ajili ya kulipa kisasi, kwa kile anachokifanya USA Kwa Urusi dhidi ya ukraine.
Kosa la SITA
Uchumi wa Urusi na Dunia.
Kosa la kuchochea vita na kuiwekea vikwazo Urusi litaigharimu sana USA.
Kwa sababu nchi nyingi zimeona kua ukitofautiana na USA atakuwekea vikwazo.hivyo nchi nyingi zitatengeneza uchumi na Mifumo ya kifedha na sarafu isiyotegemea USA Kwa asilimia kubwamfano Dola, ili kuepuka vikwazo vya USA.
Hii itaighalimu Sana USA kiuchumi tofauti na Sasa.
Mambo ni mengi.
Lakini kwa kifupi huyo waliekua wanamsifia eti kua ana mipango sahihi kabisa ya muda mrefu ukweli hayuko hivyo,na Sasa ameingia Chaka la miba.
Kwa kifupi USA na mipango yake safari hii yeye ndio kanasa.
Ili ajinusuru aanzishe vita ya Tatu ya Dunia,lakini hii nayo ni kujitoa mhanga,maana USA nayo itakua magofu,maana wapinzani wake Wana silaha zinazoweza kupiga Hadi kwake na kuchagua wapige mji Gani na wapige Nini.
Maana yake watachagua kupiga kambi za jeshi,viwanda vya kijeshi na kiraia,miundombinu na Kila aina ya sehemu muhimu.
Maana yake USA itarudi zama za mawe.
Hali hiyo itakua kwa pande zote USA nao watafanya kama hivyo.
Ndio maana Kuna mtaalamu alisema vita kuu ya Tatu itakua ni vita vya nyukilia na teknolojia lakini ana uhakika vita kuu ya nne itakua ni ya fimbo na mawe.
Kwa muktadha huo USA Iko njia panda ikubali anguko lake ama ikubali kuanzisha vita kuu ya Tatu.
Kwa kumalizia USA ime "miscalculate" hiyo mipango yake inayosifiwaga.