Sote tumesikia na kuona katika mitandao mbalimbali ya kijamii na vyombo vya habari kuhusina na mashambulizi makali yaliyoanza mnamo Agosti 6 katika mkoa wa Kursk Oblast na vitongoji vyake baina ya jeshi la Ukraini (Ukraine Armed Forces-UAF) na Urusi (Russia Armed Forces -RAF).
•Mkoa wa Kusrk Oblast ni moja ya maeneo ambayo yametwaliwa au kukombolewa (liberated) na RAF.
Update ya kinachoendelea
•Taarifa zilizopo ni kuwa AFR imepokea kipigo kizito cha kushtukiza kutoka kwa UAF.
•Waziri wa ulinzi wa Urusi amesema jeshi lake linapambana na vikosi vya Ukraini katika mipaka ya mipakani ya Sudzhansky na Korenovsky iliyopo katika mkoa huo wa Kursk Oblast.
•Mpaka sasa, jesi la Urusi (RAF) limesema limefanikiwa kurudisha nyuma vikosi vya AFU vyalivyokuwa vinataka kuingia ndani zaidi mwa mkoa huo.
•Kwa upande wa Ukraini, kwa mujimbu wa chanzo kimoja kiitwacho "Institute for the Study of War" kimeripoti ya kuwa UAF wamefanikiwa kuingia ndani ya mkoa huo kilomita 10 (sawa na maili 6) baada ya kuvunja ng'ome mbili za RAF.
•Hali kadhalika, Urusi imetangaza hali ya dharula Kursk na kuhimiza raia wake waondoke haraka katika maeneo hayo.
Ukweli wa mambo
•Inaaminika ya kuwa wanajeshi na mamluki wa NATO ndio wanaoongoza uvamizi huo wa Kursk Oblast huku wakishirikiana na wanajeshi wa UAF wapatao Elfu kumi.
•Kwa muda mrefu jeshi la NATO lilikuwa likijipanga na operesheni hii ambayo ni muendelezo wa kumchokoza Urusi ili aingie mazima vitani.
•Sasa endapo kama operesheni ya Kursk Oblast itafeli, basi ni dhahiri ndio utakuwa mwisho wa vita hii.