LIVE Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

LIVE Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Live coverage on JamiiForums
Mtazamo wangu kuhusu huu uvamizi wa Kursk:

1)
Inawezekana wapanga mikakati wa Ukraine waliamua kuuvamia huu mji ili Urusi apunguze wanajeshi kule upande wa Mashariki ambako ameelekeza nguvu kubwa kule na ndiyo kiini cha mgogoro upo kule.Hapa Putin kagoma kula chambo.

Walitumia hii theory ya Sun Tzu:

"You can be sure of succeeding in your attacks if you only attack places which are undefended".

2)
Ukraine waliamua kuuvamia huu mji ili wapate nguvu kwenye mazungumzo ya kumaliza vita.Huu mji una kinu kikubwa cha nyuklia.

Urusi amekikamata kinu cha nyuklia cha Ukraine kwa muda sasa na Ukraine ametulia na hana cha kufanya!.

Kama wakifanikiwa kukikamata hiki kinu basi Urusi hatakuwa na namna zaidi ya kutulia! Hapa unaweza kusema Putin kakubali kumeza chambo!

Hapa walitumia hii theory ya Sun Tzu:

"You can ensure the safety of your defense if you only hold positions that cannot be attacked".

Majibu ya Urusi kuhusu uvamizi wa Kursk:


Wao wenyewe bado wanaendelea na kusonga mbele huko Mashariki mwa Ukraine, kwenye huu mji wamepelekwa askari wasiokuwa na mafunzo makubwa na wasio na uzoefu.

Vyanzo (vya kimagharibi) vinasema Putin katoa amri mpaka mwezi wa kumi Ukraine wawe wameondolewa hapo Kursk. Hapa utaona wanataka wamalize mchezo hapo Mashariki kisha waje nyumbani!

Maamuzi magumu ni haya: Mfumo wa upiganaji wa kirusi ni kuharibu kila kitu halafu tuanze upya! Atafanya hivi nyumbani kwake?? Muda utaamua!

Mpaka sasa Putin kaamua kutumia hii theory ya Sun Tzu:

" Do not swallow bait offered by the enemy"
.

Ni mtazamo wangu!
Mkuu, umeeezea uzuri sana na yaeleweka khasa.
 
Baada ya wiki 2 zijazo mkimuona tena Kipanya44 hapa jukwaani basi mniite Asha mitako 😂😂😂
Mkuu nakushauri tu usifikie huku kipanya huyo yeye kashajitoa ufahamu hata ukraine ikabomolewa yote haelewi we ufikiri mpaka leo anaamin bakhmut haijakombolewa na warusi, sio mtu mzuri huyo.
 
In fact Mkuu hatujui idadi kamili ya wa Ukraine( NATO)(West)walioingia
Lakini kama ni elfu 12 Hadi kuifikia mwezi wa 10 wote watakua wamemalizwa.
Labda wawe lakini na zaidi.
Hata hivyo wanazidi kupoteza vifaa Kila siku ,Sasa sijui watawezaje kujilinda wakiwa ndani ya Kursk.
Na kadri siku zinavyozidi kwenda mbele Urusi wanazidi kuwa dhibiti zaidi na wao wanazidi kupungua nguvu,mwisho wa siku watashindwa TU.
Naongelea huko kursk.
Uko sawa ni zaidi ya 12,000 lakini wote wamekwama yaani wamewekwa kati hawawezi kusonga mbele wala kurudi nyuma.

Pia kazi ya kushughulika nao wamepewa wapiganaji wa Chechen, kumbuka ziara ya kuzuga ya Putin huko Jamhuri ya Chechnya majuzi.

Ramzan Kadyrov akamhakikishia raisi Putin kwamba kuna wapiganaji wapatao 47,000.

Kazi kubwa ya Kadyrov ni kusimamia kituo cha mafunzo ya kijeshi ambacho kipo hapo mjini Chechen na chafundisha wapiganaji wa kujitolea ambao Putin awaita "Invicible".

Hivyo wapiganaji wa Chechen watamegwa kiasi na watatumika muda ukifika maana Chechnya na Kurks si mbali na wana vifaa vya aina zote.

Ndo maana naita fake news kwamba kuna wanajeshi wavutwa kutoka pande ya mashariki au wengine wapelekwa kutokea Burkina Faso.
 
Sema wanajeshi wa Ukraine kuna vitu itakuwa wanalishwa sio bure,yaani wanaivamia Russia kama wanaivamia SOMALI LAND
Lengo kubwa ambalo halisemwi lilikuwa Ukraine wachukue kinu cha nyuklia kilichopo Kursk na hiyo mission wakashindwa.

Wangechukua hicho kinu Ukraine wangekuwa na sauti kubwa na wangewalazimisha Russia waketi kwa mazungumzo.

Hicho kinu chalindwa na majeshi halisi ya Russia na si wapiganaji wa kukodiwa.
 
Kelele za chura hazimzuii ndovu kunywa maji.
Ukraine inateseka na itaendelea kuteseka.
Usidhani Russia atakaa kimya pasi na kulipiza hilo shambulizi.
Tena yeye hulipiza mara dufu.
Kaa mkao wa kula usikimbie Russia akilipiza.
Sawa kabisa, Ukraine anateseka na ktk muktadha wako, Russia atakuwa anateseka zaidi kwani ndo mwenye "shughuli".
....kwamba sasa hivi kaanza kulipia????....elewa neno mwenye shughuli.
 
Lengo kubwa ambalo halisemwi lilikuwa Ukraine wachukue kinu cha nyuklia kilichopo Kursk na hiyo mission wakashindwa.

Wangechukua hicho kinu Ukraine wangekuwa na sauti kubwa na wangewalazimisha Russia waketi kwa mazungumzo.

Hicho kinu chalindwa na majeshi halisi ya Russia na si wapiganaji wa kukodiwa.
Supper power mwenye jeshi kubwa anakodi vipi majeshi?
 
Back
Top Bottom