''Urusi inapigana na NATO'' umetumia vigezo gani kusema hivyo? Mimi pia sikubaliani na nchi za magharibi kwa vitendo vyao dhidi ya urusi, lakini siwezi kupuuzia nguvu ya NATO kijeshi, NATO Bado haijaingia vitani na Urusi
Dah!
Kuna maswali kabla ya kumjibu mtu hua ni kawaida kumjua mtu Hali yake.
Maana unaweza kua unamjibu mtu ambae ana Hali Fulani ukapata ama urahisi wa kumjibu ama ukapata taabu ya kumjibu.
Maana kuelewa baadhi ya vitu hivi sio lazima uwe umepitia mafunzo ya shule ya sekondari,mgambo,upolisi, jeshi,usalama ama diplomasia.
Ufahamu wa mambo haya inahitaji ufuatiliaji wa mambo yanavyoendelea duniani.
kwa kukufuatilia kidogo michango Yako humu jukwaani nakuona ni mtu muelewa sana wa haya mambo.
Ila kinachonishangaza ni unashindwaje kujua kama Urusi inapigana na NATO.
Tena sio NATO tu,bali ni nchi zote za Magharibi.
Sasa hapa ndio penye utata na nitajatibu kukuelezea Kwa akili ili unielewe.
(Kwanza kabisa naomba ukubali maelezo yangu kua nchi moja inaweza kupigana na nchi nyingine kwa kutumia direct war,semi direct war ama indirect war.
Haya ni maelezo yangu TU wala sijayatoa kitabuni,ukumbuke vitabu vimeandikwa na watu,hata Mimi naweza kuandika).
Kwa vita hii USA NATO na other west wanapigana na Urusi Kwa kutumia semi direct war.
Nikisema semi direct war namaanisha kua NATO wako nyuma ya Ukraine Kwa sababu Kuna wanajeshi wao na wataalamu wao wanashiriki moja Kwa moja katika vita hii ingawa hawajatangaza.
Vigezo nilivyotumia kuona NATO na ninaongezea na west wengine wanapigana na Urusi ni hivi;
Anapigana na Urusi ni Ukraine ambae sio mwanachama wa NATO,
Lakini .
1-nchi zote za NATO ,EU na Ulaya Magharibi zimeiwekea vikwazo Urusi.
*Kumbuka Nia ya vikwazo ni kutaka kidhoofisha uchumi wa Urusi ili ishindwe kugharamia vita.
*Kuwafanya raia wa Urusi walete machafuko kwa sbb ya Hali ngumu.
2-Nchi zote za NATO na west wengine kuchangishana fedha ili kuisaidia Ukraine iweze kumudu gharama za vita ili iishinde Urusi.
3-Nchi zote za NATO na west wengine kuchangisha silaha kwa ajili ya kuipa Ukraine ili iweze kuishinda Urusi.
Katika hili la silaha Kuna mambo ambayo ndio yanathibitisha moja Kwa moja kua NATO na west wengine wanapigana na Urusi Kwa kile Mimi nakiita semi direct war ya NATO dhidi ya Urusi.
Nayo ni hiii.
Ushahidi upo ambao baadhi ya ma Jenerali wa baadhi za nchi za NATO wameshiriki moja Kwa moja katika vita hii na wengine kuuliwa vitani.
Ushahidi upo wanajeshi wa NATO wakishiriki vitani Kwa vivuli vya jina la mamluki ama (mercenaries).
Baadhi ya wataalamu wa nchi za NATO kushiriki kuendesha "(ku operate)" baadhi ya mitambo ya kijeshi au kivita ambayo Ukraine wamepewa na nchi za NATO ,kkn wanakua hawana utaalamu wa kui operate.
Maandishi yapo na Kuna wengine waliuliwa kutokana na mashambulizi ya Urusi wakiwa Wana i operate mitambo hiyo.
NATO inapigana na Urusi Kwa kutoa huduma za mawasilano ya satellite za baadhi ya nchi za NATO kulipa taarifa jeshi la Ukraine juu ya mienendo ya vifaa vya urusi na wanajeshi wa urusi,walipo, wanachofanya na wanachofikiria kufanya na kisha kushambulia.
Sehemu kubwa ya huduma hii Ukraine hana isipokua USA na nchi chache sana za NATO.
Kumbuka kuna makombora aliyopewa Ukraine kutoka USA na UK hayawezi kupiga malengo bila satellite na wenye makombora hayo ndio wenye satellite hizo.
Ushiriki mwingine wa NATO ni kuingilia mawasilano ya jeshi la Urusi na kuwapa jeshi la Ukraine.
Kutafuta taarifa za kiintelijesnsia na kuipa Ukraine.
4-Nchi za NATO kukaa vikao vingi sana na vyote kujadilana kuishinda Urusi.
Moja ya kauli ya katibu Mkuu wa NATO ni kua Urusi lazima ishindwe,kwani kushindwa kwa Ukraine ni kushindwa kwa NATO.
Hebu fikiria Ukraine ndio inapigwa lkn ruhusa ya kupiga maeneo Gani na maeneo Gani asipige inatoka NATO.
Ama ukraine ndio inapigwa lkn ruhusa ya ama kuvamia kursk ama kutovamia inatoka NATO.
Sasa kama Ukraine sio mwanachama wa NATO kwa Nini NATO anakua ana maamuzi kwa jeshi la Ukraine?
Kwa uchache hivyo ndio vigezo vyangu kua NATO inapigana na Urusi ikiwa nyuma ya Ukraine lkn ikiwa na wanajeshi wake wakiwa vitani Kwa Siri.
Natambua kabisa uwezo wa NATO.
NATO ni umoja wa kijeshi wenye nguvu kubwa sana hapa duniani.
NATO wanajua fika kama wakiingiza jeshi lao kwa uwazi kwa kutoa tamko rasmi basi Urusi atapata sababu halisi ya kupiga na kuharibu vifaa vya kijeshi,silaha,maeneo na miji Yao yote ya NATO, akilenga malengo ya kijeshi,kisiasa na kiraia yenye uhusika wa moja Kwa moja na vita.
Russia uwezo huo anao.
Pia marafiki wa Urusi nao watakua na sababu ya kuingilia vita kumsaidia Urusi.
NATO Kwa kuyajua haya wala hawatathubutu kutoa tangazo la kuingiza majeshi rasmi Bali wataendela kupigana na Urusi kiujanja ujanja,kiuwoga na kwa kivuli na wakiwa nyuma ya ukraine.