Urusi hauwezi mziki wa west. ,nikumbushe pamoja na back up ya north Korea.., Belarus., Iran.,china na wengineo,bado ameshindwa kukatiisha kanchi kadogo tu Tena jirani yake
Katika watu walioamua kuwa wehu kwa makusudi hakuna anayekufikia
Katika hizo nchi zote ulizozitaja unaweza kutuambia zimetumia kiasi cha pesa kuisaidia Russia mpaka sasa? Kama ni silaha mpaka sasa amepatiwa msaada wenye thamani kiasi gani?
Usije na habari za drone za shahed, maana hizo zilinunuliwa. Pia military chips za china zilinunuliwa.
Pia unaposema Ukraine ni taifa dogo unamaanisha nini?
Je, unafahamu kwamba kwa ulaya nzima Ukraine ni taifa la pili kwa ukubwa likitanguliwa na Russia?
Je, unafahamu kwamba Ukraine ndio nchi ya pili kwa jeshi kubwa ulaya ikitanguliwa na Russia?
Je, unafahamu kuwa Ukraine kabla ya hii SMO Jeshi lao lilikuwa la 9 duniani kwa ukubwa wa bajeti, wakati Russia ikiwa ya 3?
Sasa nchi ya 2 kwa ukubwa kieneo, ya 2 kwa ukubwa wa jeshi na ya 9 duniani kwa ukubwa wa bajeti ya kijeshi inapewa msaada wa intelijensia na mataifa 10 bora kiintelijensia, inapewa msaada wa zana za kijeshi na nchi 34 na unategemea iwe ya kinyonge? Unategemea ishindwe kirahisi?
Bila kusahau Ukraine inapigana ikiwa haina vikwazo vyovyote wakati huo huo Russia ikiwa na vikwazo lukuki.
Bila shaka Yoyote ile NATO na mataifa yote yanayoisaidia Ukraine hayakutegemea Russia iwe na uwezo wa kupigana kwa muda mrefu mpaka sasa ndio maana hata Trump amekuja na mpango wa kumaliza vita ili wasiendelee kuingia gharama zaidi.
Ilichokifanya Russia mpaka sasa sidhani kama kuna taifa duniani linaweza kukifanya. Hata wao Russia wanaendelea na vita kwasababu ya Ubishi na ufahari wa kushinda vita