Kuna kitu wengi hawakijua, haya mabasi mengi vithibiti mwendo kuna ambao wamewekewa kwenye speed 85, 90, 100 mpaka 120. Lakini pale kwenye dash board unaona inalia kwenye 85km lakini uhalisia ni 100 speed. Nilishawahi kufuata Kilimanjaro, NewForce, na Sauli za Mbeya Dar, speed zao ni 100. SO mt asikudangaye kwamba zote zinatembelewa 80 speed
Pili kuna mchezo wa kubeti, dereva anaweza amua anunue tochi au akubali kulipa fine lakini nia yake awe mbeye ya wote na kufika wa kwanza, so huo ni mchezo mwingine
Tatu madereva wanaachana kwenye sehemu zifuatazo, kwenye 50 wenzanko wanapita na 100 speed, kwenye vituo au stand za mabasi wajanja wanafanya fasta kama abiria ana mzigo anapeleka stand, mfano stand pale Uyole mabasi yakisimama muda ni dk3 ishapotea. Vitu vya kula pia wengi wanatoa dk 10-15.