SPEEDAF Carrier na uhuni wenu wa kitoto mnaotufanyia

aliewahi kuagiza simu aliexpress through speedaf, naomba kuuliza inafika bila tatizo lolote?maana kibongo bongo mzigo kupotea ni kugusa
Kutoka china mpaka Tz mzigo unafika fresh, Tatizo linaanzia hapa Tanzania
 
Hivi mkuu unafahamu chain ya mzigo jinsi inavyofanya kazi? Kuanzia kununua, kukatiwa tracking number, kusafirishwa, hadi kumfikia mteja?

Usipodai refund ni wewe, 😀 lakini jua kabisa mzigo unaposafirishwa, seller anakuwa tayari nae ameulipia bima kidogo, ukipotea yeye mwenyewe hana hasara na lazima awe refunded pia, wanabaki wanavutana koo couriers, sasa mimi nisitake refund kwa nini? 😳
 
tayari nae ameulipia bima kidogo
Parcels zinazokuwa registered/insured (kwa economy au standard shipping) ni zile zinazoanzia na tracking code R, na shipping fee inalipiwa na mnunuzi.

Parcel imepotelea Tz(na ndicho hasa kinachotokea), ukafungua dispute, muuzaji ana haki za kuambatanisha vielelezo kwamba parcel imekuwa shipped, AI za Aliexpress zikathibitisha hii, refund request yako haikubaliwi.
 
Mm nawaamini zaidi speedaf kuliko posta
Ulishawah agiza kitu kama simu kikakufikia bila tatizo? Mimi pia nawaamini sema nimeagiza vitu vidogo vidogo tu ambavyo havifiki gharama kama laki nne hivi, nilishawahi agiza cha laki tatu na kitu na kikanifikia.
 
ulishawah agiza kitu kama simu kikakufikia bila tatizo? mi pia nawaamin sema nimeagiza vitu vidogo vidogo tu ambavyo havifik gharama kama laki nne hivi, nilishawah agiza cha laki tatu na kitu na kikanifikia
Boss mm naagiza vitu vingi sana, hata zaidi ya 300k. Ujio wa speedaf kwangu ni mkombozi sababu post mizigo inachelewa sana. Mzigo unaweza kufika posta ukakaa hata wik mbili bila kupigiwa simu mpaka uende mwenyewe. Speedaf siku 12 mpaka 15 unapokea tena kwenye address yako.

Mimi kabla ya kulipia kitu namwambia kabisa seller unasafirisha na speedaf? Kama haiwezekani namtafuta mwingine.
 
Msaada wakuu. nimeagiza aliexpress carrier ni cainiao super economy global....Je hawa jamaa si ndo speedaf?

Tracking no imeanza na UV72. Make naona mzigo umefika tar 4 dec ila bado kimya
Mzigo wako uliupata tena maana wangu umeanza na UT leo siku ya 14 sijaupata
 
Na nyumbani kwake ni wapi exactly, kmmk daaah naweza nikaleta noma aisee
 
ulishawah agiza kitu kama simu kikakufikia bila tatizo? mi pia nawaamin sema nimeagiza vitu vidogo vidogo tu ambavyo havifik gharama kama laki nne hivi, nilishawah agiza cha laki tatu na kitu na kikanifikia
Wanakuletea ulipo.

Ova
 
Lols! Hili neno 'jau' ni maarufu sana. Ni kweli, Posta ni jau sana.

Ova
Wewe wa kishua si ulikuwa hujui hadi nilipokufundisha? Lol

Lakini naona bado hujaelewa maana yake vizuri, Posta hakuwezi kuwa na jau. Ngoja niendelee kukufundisha.
 
Dah hawa jamaa Wana shida gani mizigo yangu imefika halafu wamekausha kimya. Mmoja toka mwezi wa saba, ngoja niwaendee hukohuko
Jana nimetoka posta kuna mzigo umefika toka mwezi wa saba lakini naambiwa hakuna mzigo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…