SPEEDAF Carrier na uhuni wenu wa kitoto mnaotufanyia

SPEEDAF Carrier na uhuni wenu wa kitoto mnaotufanyia

Kuna mwamba yoyote aliewai kufanya ivi, iyo kutoka Aliexpress, inaitwa china to china
Screenshot_20230725-081514.jpg
 
Wadau wa manunuzi online aliexpress ...ivi nikinunua hii bidhaa [emoji116][emoji116] makadirio ya kodi ya VAT ita vhargiwa kama bei gan ivi.
Bei yake ni kama 122090 Tsh ktk mtandao ..je hesabu za kodi ya VAT yanapigwa vipi hapo
Sio kila mzigobunalipia kodi, ila ukitakiwa kulipa kodi haitakua chini ya 43%. Chukua gharama ya bidhaa bila usafiri alafu zidisha kwa 0.43 utapata kodi ya kulipia.
 
Uzoefu wa utumiaji speedaf Tanzania kwangu uko tofauti sana na watumiaji wengine...maana mimi kwao nimeshapokea parcel zangu zaidi ya 50 bila tatizo lolote..mizigo yote huwa huwa natrack kupitia app yao na ikifika siku 2 sijaona dalili ya kuletewa nafuata mwenyewe..lakini mingi yule distributor wao bonge anafikisha kwangu bila shida...zaidi ya mizigo 50 sijawahi pata challenge...mzigo wangu ukija kupitia speedaf najisikia raha lakini ukienda posta kwanza charges zinaongezeka wakati speedaf sitoi hata kumi na mzigo naletewa kwenye address.. halafu posta inachelewa sana maana mizigo yao mingi kuna nchi inapitia na kukaa siku kadhaa..hapa navoandika hii text mizigo nimenunua last week kabla ya idd now ipo airport inafanyiwa clearance ....mimi sijaona ubaya wa speedaf hata kidogo...ila posta ndio sitaki hata wasikia.....
Mkuu, hivi naweza kuwatumia speedaf kwenye alibaba?
Na wanacharge vipi shipping fees, wanatumia uzito au CBM?
 
Hello habari wadau wa jukwaa la teknolojia na wanajamiiforum kwa ujumla.
Kutoka na kasi ya maendeleo ya kisayansi na kiteknolojia si ajabu tena kwa mtu kufanya manunuzi mitandaoni .

Vivyo hivo hata Tanzania kwa sasa idadi ya watu wanaofanya manunuzi hayo imeongezeka maradufu, hasa masoko ya kutoka Uchina(nduguzetu wa damu).

Zimekuepo njia nyingi zitumikazo kusafirisha mizigo kutoka mataifa hayo (Uchina ikiwemo) kwa mda mrefu sasa .Hivi karibu kampuni ya speedaf ilifungua branch Kenya na kua mkombozi huko kwa huduma yao ya door to door delivery lakini uharaka wa mchakato mzima wa kupata mzigo wako toka siku ya manunuzi ulikua ni wa haraka na kuridhisha
Baada ya ujio wao Tanzania tulifurahi sana na kuamini kua nasi sasa tutaendana na kasi ya wenzetu kwani kampuni ile ile imeingia nchini kwetu kutoa huduma zile zile.

La hasha ,vilio vimeanza kusikika kila kona ya nchi yetu .Mizigo inatoka China vizuri, inafika mpka mkoa mhusika ulipo , maagent wanawakabidhi watu wafanye delivery kwa mteja husika ila kimbembe kinaanzia hapa .

1.Mteja hapokei simu ya wito kwa ajili ya kupokea mzigo wake .

2.Ukifuatilia ofisini speedaf unakuta sometimes mzigo ushasaini kua uliiuchukua ilhali haujauchukua wewe mhusika .Meanz agent wa kuleta anajisainia mwenyewe kua kafanya delivery( Kum make zenu tamaa mbaya). Sasa unapoingia kwa seller kudai refund unakuta seller anaevidence inayoonesha kua mzigo umepokelewa na mhusika alieununua.

Sasa kwa hali hii kweli tutafika .Mnafanya huduma nzuri au makampuni mazuri yasije nchini kwa tamaa ndogo ndogo kabisa .

WADAU KAMA SPEEDAF HAWALETI MAREKEBISHO HARAKA,tuanzeni napema kampeni ya kufosi seller kutokutumia hawa speedaf kwani ni hasara kubwa mno tuipatayo wote mnunuzi na muuzaji. Hapa chini naweka ushahidi wa item nisioipokea ila agent uchawara kasign kua umefika na kapita nao kaenda kuhonga kwa demu wake manina
View attachment 2434527View attachment 2434883
Tatizo watu wote wanalalamika kuhusu kupotea mizigo yao ila hakuna aliewahi shtaki mahakamani ili upate hela ndefu, tatizo Nini haswa?
 
Mimi miaka mitano na ushee kidogo, tokea nianze hizi mishe naishia kupokea tu kupitia posta.. Na nachagua shipping method zaidi ya moja, sometimes free cainiao, standard shipping lakini chaa ajabu ndio hivyo sina maajabu.

Sijawahi kuletewa na spidaf hata siku moja... Siku moja nikaja kulizua nikaona labda kwenye address lile box la posta linaniponza, nikaamua kulitoa/kulifuta ili nije kutarajia niletewe na spidafuu.. Kilichonikuta mzigo niliufatia makao makuu posta pale kuna kitengo cha TRA nikakandamizwa na kodi. Sasa nimeona nitulie tu niangalie chochoro zengine.
 
Screenshot_20230812-203006_1.png

Mzigo toka tarehe 4 upo ofisini kwao mpaka tarehe 11 ndio umetoka, na hio Tarehe 11 jamaa katulia sehemu hajaleta mzigo, ukimpigia hapokei, then kaurudisha na sababu imeandikwa mpokeaji ameomba uletwe siku nyengine. Hawa jamaa wanawaharibia wenzao biashara.

Mzigo toka China hadi Tanzania unatumia muda mchache kuliko toka Ofisi zao hadi kwa mteja, hivi hakuna pa kuwaripoti?
 
View attachment 2715653
Mzigo toka tarehe 4 upo ofisini kwao mpaka tarehe 11 ndio umetoka, na hio Tarehe 11 jamaa katulia sehemu hajaleta mzigo, ukimpigia hapokei, then kaurudisha na sababu imeandikwa mpokeaji ameomba uletwe siku nyengine. Hawa jamaa wanawaharibia wenzao biashara.

Mzigo toka China hadi Tanzania unatumia mda mchache kuliko toka Ofisi zao hadi kwa mteja,, hivi hakuna pa kuwaripoti?
Speedaf wana official website unaweza pia kuripoti huko kuhusu huyu wakala wao wa Tanzania.
 
Sasa hapo mbona simple?

Aliye confirm as received by me huyo ndiye atajua hajui maana for now inakuletea mpaka namba ya muhusika aliye confirm sasa hapo tunaachanaje kwa mfano?

Kuwa na amani ndugu, hakuna kupoteza kitu hata kama ni cha buku.
 
Refund unapewa depending na fault ipo wapi hata kama ulishapokea mzigo

Nimepata Refund Juzi kati Hapo..nilipokea mzigo lakini product haifanyi kazi nikadai refund na evidence nikawapa wakarudisha pesa yangu kiroho safi
Naomba kufahamu....Hivi hapo kwenye refund manake unapiga picha bidhaa kuwa ni fake(Tafsiri kama haifanyi kazi vizuri) kwa huyo muuzaji atakurudishia hela au product mpya
 
Kwa mara ya kwanza nashangaa mzigo wangu umekuja na speedaf afu nimepokea ofisi za kikuu AliExpress ziko sehemu Moja

Kikweli sijapenda taratibu zao mizigo ipo ovyo ovyo Ni rahisi mzigo potea Sana ,,

Imagine watu tofauti wanaingia ofisini kupiga stori

Bora posta mizigo inakaa ofisini unatumiwa no ya mzigo unaenda na ID yako unapewa control number unalipa Yani Ni safe Sana
Samahani naomba kufahamu mambo haya mawili
1.Mzigo posta mda maximum wakukaa ni muda ganii????
2.Waweza mtuma mtu akuchukulie mzigo posta
 
Wazee mpaka hapo kuna ulazima wa kusubiri tena nipigiwe simu au niwafate huko huko mwenyewe nikajichukulie changu mapema?
Screenshot_20231027-101322.jpg
Screenshot_20231027-091053.jpg
 
Back
Top Bottom