Spika aagiza mwandishi Pascal Mayalla na Wahariri wa gazeti la Raia Mwema wahojiwe kwa kulidhalilisha Bunge

Spika aagiza mwandishi Pascal Mayalla na Wahariri wa gazeti la Raia Mwema wahojiwe kwa kulidhalilisha Bunge

Ushauri wangu kwako Kaka Mayalla

Nenda ukamuombe msamaha Mheshimiwa Spika, usitafute sababu za kwenda kuiambia kamati kwakua kwa lugha uliyoitumia kwenye makala yako ni lugha ya kuudhi, ijapokua ulitaka kuonyesha ufundi wa kujificha chini ya kivuli cha mtindo wa swali.

Kaka Mayalla, napenda watu wenye kuamini na kusimamama katika mitizamo yao juu ya kile wanachokiamini FANATIC, lakini kamwe siko radhi na watu wanao onyesha misimamo yao kwa Matusi na Kejeli.

Kaka Mayalla, kumbuka kwamba hao wabunge uliosema "WAPO KWA AJILI YA KUTOA HUDUMA ZA KIBINADAMU" ambayo itabidi baadae utuambie maana yake, wanao wake/waume, watoto na hata watu ambao wanawaona kama ni miongozo yao katika maisha.

Kaka Mayalla, Mheshimiwa Profesa Palamagamba Aidan Mwaluko Kabudi aliwahi kusema (kama mnashindwa kumuheshimu mimi basi heshimu utu wangu) sasa ndugu yangu umeshindwa hata kuheshimu utu wa Wabunge na Spika wao? hata hilo tu nalo linahitaji tufunzane namna ambavyo tunapaswa kuziwasilisha hisia zetu?

Kaka Mayalla, chonde chonde chonde, omba radhi haya yaishe tuendelee na maisha mengine...

Ahsante
 
Kilichoandikwa na Pascal Mayalla kuhusu waheshimiwa wabunge katika gazeti la Raia mwema ni ukweli wenye uchungu ndani yake. Na kitendo cha spika wa bunge kulifikisha jambo hilo bungeni ni kujidhihirisha madhaifu yao kiuhalisia.
Maswali yangu ni haya.
1. Mara ngapi wamekuwa wakidhalilishwa na Makonda ( mkuu wa mkoa wa Dsm na hawasemi chochote) mfano hili la watoto na madawa ya kulevya mwaka jana.
2. Mbona hawako makini kuyajadili yaliyo muhimu kwa wananchi na mjadala ukaonekana unamatokeo chanya ila mjadala unaowahusu huwa makini kuliko kawaida.
3.Mara ngapi mawaziri wanajibu majibu dhaifu na hakuna utekelezaji wowote sijaona hatua zikichukuliwa zaidi.
.
Ifike pahala hawa wabunge tuwaweke wazi watambue sisi wananchi ndio tunaowaweka bungeni na sio kwa nguvu zao. Hivyo wawe tayari kusemwa wanapopindisha mambo.
.
Nini mtazamo wako.
Oooh niajabu sana
 
Huyu Pascal anaweza kuitwa na Immigration kuhojiwa ni mzaliwa na raia wa nchi gani apeleke vyeti vyake vya kuzaliwa na mababu zake 3 waliotangulia enzi zile
 
Kama siyo kujipendekeza kwa sereli kwanini wasijibu swali lililoulizwa badala ya kuwatisha wauliza swali kwa kuwahoji?.
 
Paschal ana akili nyingi kuzidi spika Ndugai kwahiyo ni swala la muda tu mambo yanaenda sawa
 
Vichwani mwetu WaTz, hasa vijana, tumeingiliwa na MDUDU KUJUA. Tunalaumu pasipo kuwa na ushahidi ila kusukumwa na Rais
 
Back
Top Bottom