Cherenganya
JF-Expert Member
- Jan 21, 2018
- 2,309
- 1,785
Ushauri wangu kwako Kaka Mayalla
Nenda ukamuombe msamaha Mheshimiwa Spika, usitafute sababu za kwenda kuiambia kamati kwakua kwa lugha uliyoitumia kwenye makala yako ni lugha ya kuudhi, ijapokua ulitaka kuonyesha ufundi wa kujificha chini ya kivuli cha mtindo wa swali.
Kaka Mayalla, napenda watu wenye kuamini na kusimamama katika mitizamo yao juu ya kile wanachokiamini FANATIC, lakini kamwe siko radhi na watu wanao onyesha misimamo yao kwa Matusi na Kejeli.
Kaka Mayalla, kumbuka kwamba hao wabunge uliosema "WAPO KWA AJILI YA KUTOA HUDUMA ZA KIBINADAMU" ambayo itabidi baadae utuambie maana yake, wanao wake/waume, watoto na hata watu ambao wanawaona kama ni miongozo yao katika maisha.
Kaka Mayalla, Mheshimiwa Profesa Palamagamba Aidan Mwaluko Kabudi aliwahi kusema (kama mnashindwa kumuheshimu mimi basi heshimu utu wangu) sasa ndugu yangu umeshindwa hata kuheshimu utu wa Wabunge na Spika wao? hata hilo tu nalo linahitaji tufunzane namna ambavyo tunapaswa kuziwasilisha hisia zetu?
Kaka Mayalla, chonde chonde chonde, omba radhi haya yaishe tuendelee na maisha mengine...
Ahsante