Wana Nzengo,naombeni kuanzia Leo tuanze kumuombea kwa mungu wetu,Muandishi nguli,Ndg Paschal Mayala,aepushwe na mabaya yote yanayoweza kumtokea,baada ya kuonyesha kutoyumbishwa na wito wa Speaker.Pamoja na speaker kushikiria msimamo kwamba lazima Paschal aitwe kwenye kamati ya maadili,bado paschal hajaogopa na ameendelea kushikiria imani ya tulio wengi kuhusu bunge letu.
Kwa nini aombewe,.Kama tujuavyo hali ilivyo sasa,ukionekana unakosoa mihimili ya nchi na ukajulikana,basi jiandae kwa kinachoweza kukutokea.Hebu tuombe lisitokee kwa mwandishi huyu mahili aliyebakia ambaye angalau anauthubutu wa kusema na kutusemea sisi tuliogeuka kuwa kunguru.Mungu mlinde na kumsimamia shujaa wetu Paschal,kwa mabaya yote yanayoweza kumpata.