Huyu Spika ajifunze kwa waliomtangulia, Kama akina Sitta wangekuwa kama huyu spika wa leo uchafu uliofukuliwa kipindi kile wa Richmond na mengine yasingefahamika kamwe, Awamu hii spika amekuwa hapendi kusikia ukweli unaouma wenye kutetea maslahi ya taifa, spika amekuwa mbabe kwa wabunge na kuwafungia kuhudhuria vikao vya bunge, hataki kusikia hoja zenye maslahi ya nchi anataka blah! Blah!, spika amekuwa anawapiga mikwara wabunge wenye kujitambua na wanajitahidi kuja na hoja zenya kujenga, kwa mwendo huu wa kutaka kusikia yanayowafurahisha kamwe nchi hii haitaweza kuendelea baada ya miaka kadhaa mbele tutakuwa tumezidi kurudi nyuma huku wenzetu Kenya wakisonga mbele.
Aibu sana.