Spika aagiza mwandishi Pascal Mayalla na Wahariri wa gazeti la Raia Mwema wahojiwe kwa kulidhalilisha Bunge

Spika aagiza mwandishi Pascal Mayalla na Wahariri wa gazeti la Raia Mwema wahojiwe kwa kulidhalilisha Bunge

Ile kamati ishakuwa kamati ya madili..

Siyo ya maadili tena..

Ni kama Kamati ya harusi ..

Alafu uhuru wa kujieleza uko wapi ,Pasko usiwaulize tena ila sasa waeleze bayana wasijipendekeze kwa serikali..
 
Kilichoandikwa na Pascal Mayalla kuhusu waheshimiwa wabunge katika gazeti la Raia mwema ni ukweli wenye uchungu ndani yake. Na kitendo cha spika wa bunge kulifikisha jambo hilo bungeni ni kujidhihirisha madhaifu yao kiuhalisia.
Maswali yangu ni haya.
1. Mara ngapi wamekuwa wakidhalilishwa na Makonda ( mkuu wa mkoa wa Dsm na hawasemi chochote) mfano hili la watoto na madawa ya kulevya mwaka jana.
2. Mbona hawako makini kuyajadili yaliyo muhimu kwa wananchi na mjadala ukaonekana unamatokeo chanya ila mjadala unaowahusu huwa makini kuliko kawaida.
3.Mara ngapi mawaziri wanajibu majibu dhaifu na hakuna utekelezaji wowote sijaona hatua zikichukuliwa zaidi.
.
Ifike pahala hawa wabunge tuwaweke wazi watambue sisi wananchi ndio tunaowaweka bungeni na sio kwa nguvu zao. Hivyo wawe tayari kusemwa wanapopindisha mambo.
.
Nini mtazamo wako.
 
Ilikuwa vyema kama kila wilaya sijui mkoa yenye mbunge wananchi waliowapigia kura waende Dodoma kuwakumbusha ni wananchi wamewaweka hapo sio serikali. Wanalipwa mishahara na malupulupu kwa kodi zetu sio serikali kama wameshindwa kutuwakilisha waachie kazi tubakie na wakuu wa mikoa nchi isonge. Wabunge wa Bunge la Tz wapo kwa maslahi yao kufuja pesa za walipa kodi kujadili upuuzi starehe zilizovuka kiwango uzwazwa na ujinga mwingi.
Hii nchi ilipashwa kufuta kitu inaitwa wabunge hawana faida zaidi ya hasara
 
Huyu Spika ajifunze kwa waliomtangulia, Kama akina Sitta wangekuwa kama huyu spika wa leo uchafu uliofukuliwa kipindi kile wa Richmond na mengine yasingefahamika kamwe, Awamu hii spika amekuwa hapendi kusikia ukweli unaouma wenye kutetea maslahi ya taifa, spika amekuwa mbabe kwa wabunge na kuwafungia kuhudhuria vikao vya bunge, hataki kusikia hoja zenye maslahi ya nchi anataka blah! Blah!, spika amekuwa anawapiga mikwara wabunge wenye kujitambua na wanajitahidi kuja na hoja zenya kujenga, kwa mwendo huu wa kutaka kusikia yanayowafurahisha kamwe nchi hii haitaweza kuendelea baada ya miaka kadhaa mbele tutakuwa tumezidi kurudi nyuma huku wenzetu Kenya wakisonga mbele.

Aibu sana.
 
Ndungai buaaaana unatafuta kudhalilishwa sasa. Umesahau sakata la kutelekeza watoto watu wanasema watakuchambua kama karanga weh haya. Pascal Mayalla nothing to worry about you can do this! come what may, you gonna win big! All the best
 
Sasa mbona spika kamhukumu kabla hajafikishwa huko kwenye kamati? After all makala iko kwa mtindo wa swali hivyo hajahukumu moja kwa moja
 
Zama hizo, wale mwanafunzi 'vichwa' walikuwa wakimuliza mwalimu 'kilaza' swali gumu; mwalimu husika alikuwa anamwadhibu mwanafunzi, si kujibu swali.
 
Lisu alisema kila kitu..kuna mtu wana mcort kila siku kwaambaaaa..walipowashika watu fukani mi sikusema kitu maana sikuwepo huko na walipokwenda kwa watu fulani sijasema lolote maana na huko sikuwepo na walipofika mahali ile huko nako sikusema kitu mana sikuwepo huko..sasa wamekuja kwangu na sioni wa kunitetea..pascal mayala sasa ni zamu yako wakati wwngine wanauliwa hamjasema lolote sasa ni zamu yako jamaa anaongea kwa zereeeeeu kwelikweli yaanu ni kama ile ya mhutu anasema mi naiucheki tu hafu nasema ihiiiiiiiiiiii...bunge likikumaliza na mwakiembe nae anakuita sipati picha tanzania inakoelekea ni wapi..ni full dictatorshipe
 
Back
Top Bottom