Spika aagiza mwandishi Pascal Mayalla na Wahariri wa gazeti la Raia Mwema wahojiwe kwa kulidhalilisha Bunge

Spika aagiza mwandishi Pascal Mayalla na Wahariri wa gazeti la Raia Mwema wahojiwe kwa kulidhalilisha Bunge

FB_IMG_1523524974138.jpg


My Take
Naomba na mimi kuunganishwa kwenye kesi ya Pasco kwa kusema bunge hili ni bunge la hovyo kabisa
 
ONA AIBU WASI.....wewe nae ni mwanahabari UNAEJIELEWA KWELI????
kila mtu anafahamu kabsa wewe ni kamradi maalumu ka hapo UFIPA.....zero brain kabsa MUANDIKA UMBEA, unaekopi mada fb na kutuletea hapa...wakati unanijibu hii comment uje utuonyeshe ANDIKO LOLOTE ULILO WAHI KUANDIKA HAPA JF la kutoka kichwani kwako mwenyewe kama afanyavyo PASCHAL
Akileta unitag!!
 
View attachment 742226

My Take
Naomba na mimi kuunganishwa kwenye kesi ya Pasco kwa kusema bunge hili ni bunge la hovyo kabisa
CHEKI ULIVYO BHANGI......hivi hapa UNATUDHIRISHIAJE wewe kweli ni mwanaume wa SHOKA kwa ulichokiandika nyuma YA KEYBOARD????.....Utaunganishwaje NA JASIRI KAMA PASCHAL ili hali upo nyuma ya keyboard?
 
Sasa hawa wanataka wasifiwe kwa lipi? Kuwa kitengo cha jiwe? Kuwa Bunge uchwara au kuchukua rushwa ya milioni 10 kutoka kwa jiwe ili waminye uhuru wa habari nchini!?
 
Tatizo wewe Ulitaka awe Ukawa?
Paschal Mayalla ni Mwanahabari huru...
Hafungamani na Upande wowote na Huwa analiweka wazi hilo....Tatizo Inategemea na Uelewa wa Kichwa chako...spoon Feeding!
Yeye kila Upande Kukosoa na Kusifia pale inapostahili....Tatizo wewe Umezoea 1+1=2
naona hata nikikuelewesha taaluma ya uwandishi wa habari baado itakuwia vigumu sana kuelewa wewe
 
Spika Job Ndugai ametoa maagizo kwa Kamati ya Maadili ya Bunge, kumhoji Mwanahabari Pascal Mayalla na Wahariri wa gazeti la Raia Mwema kwa kuandika makala ikiwa na kichwa "Bunge linajipendekeza?"Taarifa zaidi zinafuata...

Kina Pascal waliuliza swali, hawakutoa kauli; Bunge linajipendekeza kwa serikali? Sasa utamshitakije mtu anayeuliza swali? Kuuliza si ujinga. Kama Bunge sio la kujipendekeza kwa serikali basi Ndugai ajibu na kufafanua kwa nini Bunge sio la kujipendekeza. Sio sahihi kumfuatilia mtu aliyeuliza swali kwa kutaka kujibiwa.

Na mimi nitamuuliza Ndugai; hivi amesoma fasihi? Ni yupi kati ya watu watakaotoa matamshi haya wanatakiwa kuhojiwa;

1. Raisi Magufuli ni dikteta?
2. Raisi Magufuli ni dikteta.

3. Bunge linajipendekeza kwa serikali?
4. Bunge linajipendekeza kwa serikali.
 
Back
Top Bottom