Spika Bunge la Katiba: Mchuano ni kati ya Sitta na Chenge

Spika Bunge la Katiba: Mchuano ni kati ya Sitta na Chenge

Mbona wote ni ccm? Ina maana cdm hawana watu wenye uzoefu

Tatizo sio kwamba CDM hawana watu wenye sifa za kugombea hizo nafasi. Nadhani wanatumia na kucheza vema karata yao Bungeni.

Ki_namba CDM wapo wachache sana, kuweka mtu wa kugombea na tuseme akapata hicho kiti, idadi yao kwenye kuwasilisha ama kupigilia misumali katika hoja wanazoamini zipo sawa utakuwa mdogo, achilia mbali lawama za watu kusema kwamba kila hoja imepita kwa sababu wao,CDM ndo wana spika hivo kudidimiza hoja mbadala.

Pengine watakosa sehemu ya kulalamika kama ilivo hulka yao "kwasababu flani Flan wamepitisha hoja hii ama kuipa nguvu ama kutunyima nafasi ili atetee maslahi ya chama chake.."
#just saying 🙂
 
tatizo sio kwamba cdm hawana watu wenye sifa za kugombea hizo nafasi. Nadhani wanatumia na kucheza vema karata yao bungeni.

Ki_namba cdm wapo wachache sana, kuweka mtu wa kugombea na tuseme akapata hicho kiti, idadi yao kwenye kuwasilisha ama kupigilia misumali katika hoja wanazoamini zipo sawa utakuwa mdogo, achilia mbali lawama za watu kusema kwamba kila hoja imepita kwa sababu wao,cdm ndo wana spika hivo kudidimiza hoja mbadala.

Pengine watakosa sehemu ya kulalamika kama ilivo hulka yao "kwasababu flani flan wamepitisha hoja hii ama kuipa nguvu ama kutunyima nafasi ili atetee maslahi ya chama chake.."
#just saying 🙂

in chenge we trust...in 3 goverment we trust...sita ataendesha bunge la katba kishabiki na hawezi pitishwa na uwezo wa chenge katka ufahamu wa sheria ni mkubwa kuliko sta ikumbukwe chenge ni mmoja wa genius wa havard universty
 
tungeweza kutofautisha vyama vya siasa na mchakato wa katiba mpya tungefanikiwa sana.
yaani natamani wangejisahaulisha kuhusu siasa nawakajikita katika kutengeneza katiba bora.

Mkuu haujakosea kitu!
Tatizo MACCM watatetea serikali 2 kama agizo la chama!
Na sidhani kama atatokea ccm kupinga hilo!
Huoni huu ni ujinga?
Demokrasia iko wapi?
 
Hivi Chenge ni mtu wa aina gani? He keeps on political arena despite the fact that he is alleged of being corrupt. I don't see any thing potential out of him for the next 50 years of the new constitution. I would rather vote for 6. He did well in 2005-2010 in the parliament.

kama wapiga kura nao ni corrupt au mazoba, acha agombee wala usishangae akishinda.
 
Ikiwezekana kila mkoa huwe na serikali yake...

Hii ndiyo safi sana mkuu, serikali za majimbo ndiyo mpango mzima. Tatizo wanaogopa baadhi ya maeneo kuwa watakuwa strong na hawatapata hela za kuiba ndiyo maana wanataka centralization of resources.
 
Mkuu mimi hata waseme hakuna serikali yaani sifuri sawa tu!

Sure mkuu na wajue kuwa wananchi wamechoka, ninaamini wana watu hao hapa JF ili wawe wanachukua tu haya mawazo ili yawasaidie, wajue hawatakiwi kabisa. Hakuna cha maisha bora kwa kila mtanzania, imejeuka kero na majanga ya watu kunyang'anywa ardhi zao na kupewa wawekezaji uchwara na hakuna maendeleo yoyote. Eti nilisikitika sana eti wananchi wa Liganga na Mchuchuma wao watawezeshwa kufuga nguruwe, kuku na bustani ili eti wazalishe wachina wanunue!!! Je huu ndiyo uwezeshaji?? Nilitegemea kusikia maendeleo ya huduma za jamii kama shule na hospitali, barabara, vyuo vya ufundi, n.k. So sad!!
 
Kama Chenge anaamini serikali tatu, hata kama ni fisadi nitampenda tu.
 
Kutoka na ratiba ya kwanza iliyotolewa na bunge la katiba tulidhani tarehe 26 kungekuwa na uchaguzi wa Sipka (mweyekiti?) wa bunge maalum la katiba na penginge hotuba ya ufunguzi ya Mh Rais. Hivyo bosi wangu alinikurupua na kuniagiza niwe Dodoma kufikia jpili. Nilipofika Dodoma nilipitia viwanja maarufu kwenye mitaa ya Kisasa, Nkuhungu na Kikuyu. Huko nilikutana na wajumbe wengi wanaotokana na Asasi za kiraia maana nafahamiana nao.

Kilichonitisha ni pale ambapo makundi ya Ccm walitufuata na kuanza kutushawishi kila kundi na mgombea wao, walianza kufika watu wa Sitta wakatuambia ubaya wa Chenge kwamba ni fisadi na kwamba anawakilisha kudi la mtandao wa mafisadi ambao wamekuwa wakitafuta madaraka kwa nguvu ya fedha chafu. Wakasema wana mtandao mkubwa wa mafisadi na wauza madawa ya kulevya. Wako tayari kuingiza madarakani watu wa aina yoyote ili mradi aliwasapoti katika juhudi zao. Wakatutaka tuwe makini maana usipika wa bunge hili ni jaribio tu la kuelekea katika nafasi wanayoitafuta!

Baada ya hapo wakaingia kundi linalosemekana la Chenge, wao walikuja na gia ya kwamba Sitta hakubaliki hata kidogo maana amekuwa akiisakama Ccm na serikali katika kujitafutia sifa. Wanasema wamebakiza kazi ndogo ya kuwashawishi wajumbe wasiotokana na Ccm ili kukamilisha kazi ya kumsimika mgombea wao. Wanasema linapokuja suala la kanuni hata Sitta anamkubali Chenge. Kuhusu kwamba mgombea wao ametumwa na kundi la mafisadi, walisema ni kelele za Sitta ambazo zimeshazoeleka, eti yeye mbona aliasisi CCJ hawakusema?

Eti na mimi naombwa kura! Nitasanua mengi maana hapa wajumbe wengi hawafahamiani.
 
Hao wataliangamiza hili taifa-hawaaminiki
 
Sijui niiamini habari yako au lah!!!
 
Habari zilizonifikia hivi punde ni kwamba aliyekuwa mwanasheria mkuu wa serikali mh. Andrew Chenge amejitoa kugombea uenyekiti wa bunge la katiba mpya. Sasa amebakia Asha Rose Migiro na Samweli Sitta.!
 
6 hana mpinzani pale!! huyo mama anajisumbua tu.
 
Back
Top Bottom