Spika Bunge la Katiba: Mchuano ni kati ya Sitta na Chenge

Spika Bunge la Katiba: Mchuano ni kati ya Sitta na Chenge


Andrew Chenge


Muhariri Michael Bahati

KAMA Tanzania ingekuwa ni nchi inayofuata maadili ya ukweli ya uongozi, Mtemi Andrew Chenge, ama angekuwa nje ya Bunge la Tanzania au, nikitazama mbali zaidi, pengine angekuwa amefungwa jela. Ndiyo sababu nimepatwa na mshituko wa mwaka baada ya kusikia kwamba Mbunge huyu wa Bariadi Mashariki kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), anatajwa kuwania nafasi ya Spika wa Bunge la Katiba lililoanza wiki hii. Hakuna shaka kwamba Andrew Chenge ni msomi wa kiwango kizuri tu katika taaluma ya sheria. Nilikuwa nafuatilia Bunge la Tanzania wakati yeye akiwa

Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) kwa miaka 10 ya rais Benjamin Mkapa, na bungeni alikuwa mahiri kwa ufafanuzi wa miswada mbalimbali. Wakati nafasi yake ilipochukuliwa na Johnson Mwanyika, niliona wazi Serikali ilikuwa imepata pengo bungeni. Mwanyika mara nyingi alionyesha uso na haiba ya kiongozi asiyejiamini na kitaaluma alionyesha yuko nyuma ya Chenge. Hata Jaji Frederick Werema ambaye anashika nafasi ya AG kwa sasa, naye amekosa ushawishi

kama aliokuwa nao Chenge bungeni. Kimsingi, sina tatizo kabisa na usomi wa mbunge huyu. Tatizo langu kubwa na Chenge ni kwenye uadilifu. Naamini kwamba Katiba ni kitu kilicho kitakatifu na kama kweli Watanzania wanaamini katika utukufu wa Katiba, Chenge hawezi hata kufikiriwa kuwa Spika atayeongoza mchakato huo. Kumpa Chenge uspika wa Bunge hilo ni sawa na kuharibu mchakato mzima wa kutayarisha Katiba mpya. Kwa wasiofahamu vizuri

kuhusu mwanasiasa huyu, Chenge ndiye aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali wakati wa utawala wa Mkapa. Yeye ndiye aliyeishauri serikali kuingia katika mikataba ya madini ambayo tunailalamikia leo, ununuzi wa rada mbovu na ununuzi wa ndege ya rais ambayo ilipigiwa kelele nchi nzima. Wakati wake, kulikuwa na fununu nyingi zikimtaja kunufaika na kila mikataba mibovu na isiyo na maslahi ambayo serikali yetu iliingia kwenye eneo la rasilimali zetu.

Ukweli uliibuka wazi wakati serikali ya Uingereza ilipojitosa kuchunguza kuhusu sakata la rada. Serikali ya Tanzania, kwa ushauri wa Chenge na ilinunua rada hiyo ya mtumba kwa bei inayokaribia mara nne ya bei yake ya soko. Kwa mujibu wa serikali ya Uingereza, Chenge alikuwa na kesi ya kujibu kwenye mauzo ya rada hiyo kutokana na kukosekana kwa maelezo ya kina ya ununuzi huo. Huo ndio wakati ambao Chenge alipachikwa jina la ‘Mzee wa

Vijisenti’ baada ya kubainika kuwa na zaidi ya shilingi bilioni moja za Kitanzania katika mojawapo ya akaunti zake za nje ya nchi zilizo katika Visiwa vya Jersey. Hebu tujiulize swali moja; katika hali ya kawaida, inawezekanaje kwa mtumishi wa serikali ya Tanzania kuwa na akaunti yenye thamani ya shilingi bilioni moja na bado akawa jasiri wa kuita kiwango hicho cha fedha vijisenti? Kwa sababu za wazi kabisa, Chenge hajachukuliwa hatua yoyote na serikali ya

Tanzania hadi sasa. Anakula kuku kwa mrija na imefikia wakati sasa watu wanamuona kuwa anafaa kuwa Spika wa Bunge la Katiba?! Itafikia wakati, wengine watasema anafaa hata kuwa Rais wa Tanzania?! Nimesikia majina mengine yakitajwa kuwania wadhifa huo wa Spika na sina matatizo nao isipokuwa jina la huyu Chenge. Kama Chenge atachukua fomu na hatimaye kuwania nafasi hiyo na kisha kushinda, huo utakuwa mwisho wangu wa kufuatilia kutazama Bunge

hilo. Nitatazamaje Bunge hilo na kulifuatilia ilhali anayeliongoza ana tuhuma ambazo hajazikanusha hadi leo? Nani kawahi kumsikia Chenge akisema ni wapi alipozipata fedha zile? Nimekuwa nikisoma kitabu cha Power, Politics and Death cha aliyekuwa Msemaji wa Serikali ya Nigeria, Olusegun Adeniyi, kinachozungumzia maisha ndani ya serikali ya marehemu Rais Umaru Mussa Yar’Adua. Miongoni mwa watu wanaotajwa sana katika kitabu hicho ni waziri wa sheria na mwanasheria mkuu wa Serikali ya Shirikisho la Nigeria, Michael Kaase Aondoakaa. Huyu bwana alikuwa

mwanasheria mahiri sana lakini tatizo lake alikuwa kibaraka wa mafisadi. Huyu ndiye aliyefanikisha kuachiwa huru kwa Gavana Fisadi wa Jimbo la Delta, James Ibori. Si huyo pekee lakini enzi yake bwana huyu Aondoakaa, Nigeria iliingia katika mikataba tata na kufanya maamuzi tata kuhusu ufisadi na mafisadi. Ni huyuhuyu ndiye aliyefanya kazi ya Mkuu wa Taasisi ya Kupambana na Rushwa ya Nigeria, Nuhu Ribadu, iote nyasi na akaishi maisha magumu kwa sababu ya kutaka kupambana na rushwa. Kwangu, sioni tofauti kubwa kati ya Chenge na Aondoakaa. Majirani zetu

hawatatuelewa endapo watamsikia Chenge akiwa ndiye Spika wa Bunge la Katiba. Serikali ya Uingereza itatushangaa endapo tutamchagua Chenge kwenye shughuli hii. Kazi ya kutengeneza Rasimu ya Katiba ilifanywa na watu ambao wana sifa ya usafi kwenye jamii ya Watanzania. Ndiyo maana Mwenyekiti wake alikuwa Jaji Joseph Warioba, akiwa anasikindikizwa na watu kama Profesa Mwesiga Baregu, Profesa Palamagamba Kabudi, Dk. Salim Ahmed Salim na

wengineo. Ombi langu kwa wajumbe wa Bunge la Katiba ni kwamba wasiharibu kazi hii ya kukumbukwa ya tume hii kwa kumpa Chenge fursa ya kutia mguu wake. Kama Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, alivyopata kusema katika siku za nyuma; “Katiba ni Kitu Kitakatifu na Hakitakiwi Kuchezewachezewa.” - See more at:


Raia Mwema - Spika Chenge, tumekwisha
mawazo yako ni tofauti kabisa na kinacho endelea kule ccm.Kule wana shindana kwa uhodari wa ufisadi.Fisadi zaidi wao ndiyo jembe.Pole sana lakini!
 
Hapa si pahala pa mchezo nikimaanisha huko kwenye bunge, hakuna magamba wala magome ,bunge hili si la kucheka na CCM kwani halihusiani na chama chaowala chama kingine ,hivyo na wao wanatakiwa wawe na heshima la si hivyo patachimbika.

Pachimbike wapi, nchi hii hii iliyojaa mataahira kibao? Mangapi yamefanyika lkn wadanganyika wako kimya tu utadhani mazezeta?! Thubutu!
 
ngoja nikueleweshe ndugu yangu;bunge la katiba siyo la kisiasa ndiyo maana kutakuwa na wajumbe 166 kutoka nje ya bunge hivyo hakutakuwa na kambi rasmi ya serikali au kambi rasmi ya upinzani.

210,hao 166 umetoa wapi, be serious
 
Mbowe pia ni mgombea usisahau hilo nalo.
Kingereza kitasemeka mno, je! atakuwa na uwezo kumudu?
Lissu alidai kuwa Hana elimu ya chuo kikuu wala hawezi kuongea kingereza, kazi hipo!!!
 
Na hawa wabunge wengine wasio na vyama vya siasa watagombea kwa namna gani sasa?

Na ndo maana panahitajika mchakato huru usiotegemea wala kujihusisha na chama, hata asiye mbunge kwa tiketi ya chama naye aweze kugombea.
 
Kutoka na ratiba ya kwanza iliyotolewa na bunge la katiba tulidhani tarehe 26 kungekuwa na uchaguzi wa Sipka (mweyekiti?) wa bunge maalum la katiba na penginge hotuba ya ufunguzi ya Mh Rais. Hivyo bosi wangu alinikurupua na kuniagiza niwe Dodoma kufikia jpili. Nilipofika Dodoma nilipitia viwanja maarufu kwenye mitaa ya Kisasa, Nkuhungu na Kikuyu. Huko nilikutana na wajumbe wengi wanaotokana na Asasi za kiraia maana nafahamiana nao.

Kilichonitisha ni pale ambapo makundi ya Ccm walitufuata na kuanza kutushawishi kila kundi na mgombea wao, walianza kufika watu wa Sitta wakatuambia ubaya wa Chenge kwamba ni fisadi na kwamba anawakilisha kudi la mtandao wa mafisadi ambao wamekuwa wakitafuta madaraka kwa nguvu ya fedha chafu. Wakasema wana mtandao mkubwa wa mafisadi na wauza madawa ya kulevya. Wako tayari kuingiza madarakani watu wa aina yoyote ili mradi aliwasapoti katika juhudi zao. Wakatutaka tuwe makini maana usipika wa bunge hili ni jaribio tu la kuelekea katika nafasi wanayoitafuta!

Baada ya hapo wakaingia kundi linalosemekana la Chenge, wao walikuja na gia ya kwamba Sitta hakubaliki hata kidogo maana amekuwa akiisakama Ccm na serikali katika kujitafutia sifa. Wanasema wamebakiza kazi ndogo ya kuwashawishi wajumbe wasiotokana na Ccm ili kukamilisha kazi ya kumsimika mgombea wao. Wanasema linapokuja suala la kanuni hata Sitta anamkubali Chenge. Kuhusu kwamba mgombea wao ametumwa na kundi la mafisadi, walisema ni kelele za Sitta ambazo zimeshazoeleka, eti yeye mbona aliasisi CCJ hawakusema?

Eti na mimi naombwa kura! Nitasanua mengi maana hapa wajumbe wengi hawafahamiani.

Basi ngoja wahuni waje wametinga kaunda suti na kubeba vi diary na ipad kuchukua mlungula kama wabunge wa katiba hawafamiani vizuri
 
mawazo yako ni tofauti kabisa na kinacho endelea kule ccm.Kule wana shindana kwa uhodari wa ufisadi.Fisadi zaidi wao ndiyo jembe.Pole sana lakini!

Ninyi wahariri Wa Raia Mwema na RAIA Tanzania mtaacha kupokea hongo za sitta na membe? Nyie mawakala Wa kagame hebu kuweni waandishi sio wadaku
 
Hayo majina yamekuwa yakitajwa wapi?
Na ukisema vijana ambao sio wavurugaji ambao ni wavurugaji ni wakina nani? Acha kukurupuka njoo na taarifa kamili,kama huna unaweza kuchangia posts nyingine sio lazima uanzishe na wewe.

Eti zzk!huyu si wa mahakama.
 
ccm wengi wenye akili baada ya kupigwa chenga na muungwana wameshtukia haya mashirikiano yao ambayo huwezi kukumbushia kisheria, wajinga waache wampitishe huyo chaguo la chama, lakini ukweli wa mambo 2015 takrima hiyo haitarejeshwa.
 
in chenge we trust...in 3 goverment we trust...sita ataendesha bunge la katba kishabiki na hawezi pitishwa na uwezo wa chenge katka ufahamu wa sheria ni mkubwa kuliko sta ikumbukwe chenge ni mmoja wa genius wa havard universty

nn amelifanyia taifa licha ya kuwa genius?
 
Back
Top Bottom