Spika Dkt. Tulia Ackson: Mbeya Watanikumbuka Kwa Ujenzi wa Barabara Njia 4

Spika Dkt. Tulia Ackson: Mbeya Watanikumbuka Kwa Ujenzi wa Barabara Njia 4

Rais, wabunge zaidi ya asilimia 80, wakurugenzi wote wanatoka ccm tokea ila huwezi amini lawama anapewa chadema kwa umaskin wa nchi hii baada ya miaka 60+ ya uhuru
Haya ndo maajabu ya Tanzania
Ndio tunataka Kiongozi anaetoa majibu.Chadema Mbeya Kwa miaka 10 mkifanya nini? Lazima muoneshe Ili watu wawaamini.kushika Dola sio mumekalia kula ruzuku tuu.
 
Huu ni wakati wa kuonesha baba yenu Sugu alichofanya ,hizi blaa blaa za hofu hazitakusaidia na bahati mbaya sio mtu wa Mbeya.

Kazi nzuri ya Tulia Ackson nyingine hii hapa 👇

View: https://www.instagram.com/p/CxKtoULNL_I/?igshid=MTc4MmM1YmI2Ng==

Hiyo siyo kazi ya Tulia Ackson bali ni zile fedha za COVID-19 kutoka IMF ambazo hospitali na madarasa zimejengwa nchi nzima. Kama kuna mtu wa kumsifia basi ni Rais Samia.

Hakuna wilaya ambayo imekosa vituo vya afya
 
Ndio tunataka Kiongozi anaetoa majibu.Chadema Mbeya Kwa miaka 10 mkifanya nini? Lazima muoneshe Ili watu wawaamini.kushika Dola sio mumekalia kula ruzuku tuu.
Nimeshakupa majibu
2010 mpaka 2015 halmashauri ilikua chini ya ccm waulize ccm walifanya nini
Na 2015 mpaka 2020 nimekushajibu ila umeamua kuchagua ubishi
 
Nimeshakupa majibu
2010 mpaka 2015 halmashauri ilikua chini ya ccm waulize ccm walifanya nini
Na 2015 mpaka 2020 nimekushajibu ila umeamua kuchagua ubishi
Tuko awamu ya Samia na Tulia hao wengine hawapo saizi,walishasahaulika kama Sugu
 
Hiyo siyo kazi ya Tulia Ackson bali ni zile fedha za COVID-19 kutoka IMF ambazo hospitali na madarasa zimejengwa nchi nzima. Kama kuna mtu wa kumsifia basi ni Rais Samia.

Hakuna wilaya ambayo imekosa vituo vya afya
Tatizo mwamba ana hisi kila mtu ni mpiga debe yaan sio mfuatiliaji
Alafu anafikiri ukiwa tofauti naye basi unashabikia au mwana-chadema
 
Spika wa Bunge mh.Dk.Tulia Ackson Mwansasu(PhD) Akihojiwa na Clouds kwamba anaacha alama gani Mbeya amejibu kwamba ikitokea hajaendelea kuwa mbunge basi Wana Mbeya watamkumbuka Kwa ujenzi wa Barabara ya Njia 4 Kwa miaka yake hii mi 5 ambayo amekuwa mbunge wa Jimbo la Mbeya mjini.

Japo jambo hili ndio linaonekana Kwa haraka lakini Mimi nitamkumbuka Kwa mambo Makuu mengine ma 3 ukiacha Hilo la Barabara ya Nsalaga-Ifisi njia 4. Mambo hayo ni ;
1)-Ujanzi wa Jengo la wodi ya kina Mama pale Meta la gorofa 6 ambalo limeipa hadhi Hospital ya Rufaa ya Kanda Mbeya

2)-Ameacha ujenzi wa mradi mkubwa wa Maji wa kutoka chanzo Cha mto kiwira Wilaya ya Rungwe Hadi Jijini Mbeya na Mbalizi Kwa Zaidi ya Bilioni 160.

3)-Ukamilishaji wa Uwanja wa ndege wa Songwe(Anapigania uitwe Mbeya),ikumbukwe Toka Mwandosya ameasisi ujenzi wake awamu ya Mkapa ,uwanja Imekamilika mwaka huu 2023 baada ya Kubomoa na kuijenga Upya runwaya zake,kufunga taa na jengo la Abiria.

4)-Ujenzi wa Barabara ya Igawa-Uyole-Songwe-Tunduma na Uyole-Mbalizi Bypass Kwa njia 4 Kwa Utaratibu wa EPC+F

5)-Mradi wa Tactic una components za Barabara za mtaani km 20,Masoko 3,Stand 3(Soon unaanza).

Hata kama by 2025 Miradi itakuwa haijakamilika inaendelea ila ni vitu ambavyo vinaonekana unaweza waoneaja watu wakaelewa.

----
"Nikisema Mbeya mjini watanikumbuka kwa jambo gani ni kwamba ujenzi wa barabara ya njia nne umeshaanza maana yake ile barabara itakapokamilika au hata kama haikukamilika mimi nikiwa mbunge imeshaanza hivyo siku zote watajua kwamba ilianza kujengwa wakati Mbunge akiwa fulani.

Lakini pia tunazipigania barabara za mitaa, lami zimeshaanza hapa na pale lakini ni dhahiri nchi ni kubwa hii na fedha zote haziwezi kwenda kufanya kazi Mbeya pekee kwahiyo itatuchukua muda ila tumeshaanza kazi na Wananchi wanaona"

"Watu wa Mbeya ni watu wakarimu, wenye Upendo na hivyo mimi na wao tunapendana.

Mimi kama kiongozi wa kuchaguliwa na watu ni kwamba si wote ni wanasiasa na wengine hata siasa sio wafuatiliaji ila wana mambo yao, hoja zao, changamoto zao, hivyo ukishirikiana nao kwenye zile changamoto zao wala hawasikilizi huyu kapita huku au huku wao wanataka kazi ifanyike" - Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson @TuliaAckson

My Take
Sugu wa Chadema amekuwa Mbunge miaka 10 hana hata kitu Kimoja Cha maana anaweza onesha Wananchi Ili kuja kumkumbuka.
View attachment 2748183
Huo ujenzi wa barabara si mpango wake, ulisnzishwa na serikali kabla hajawa mbunge ili kupunguza ajali zilizokuwa zikitokea, mpango wa mradi wa maji ulianza wakati Kikwete akiwa rais, alipoingia Magufuli alizuia miradi ya maendeleo majimbo yote ya wapinzani, huyu mama anapenda kudandia na uongo juu.
 
Mpango ni Toka Uhuru ,ila ushawishi wake ndio umefanya ianze kujengwa Sasa.

Onyesha alichofanya Sugu sitaki blaa blaa
 
Mpango ni Toka Uhuru ,ila ushawishi wake ndio umefanya ianze kujengwa Sasa.

Onyesha alichofanya Sugu sitaki blaa blaa
Toka uhuru! Wewe ulikuwa hajazaliwa na hata Dar haikuwa na njia nne, pia hiyo Mbeya yenyewe hauijui ila uchawa unakusumbua.
 
Toa shobo na upumbavu wako hapa,asingeisimamia hiyo Serikali ingeleta pesa za kujenga Barabara na miradi mingine Mbeya?

Kama hakuna alichofanya huko Jimboni haya niliyoandika ulifanya wewe na Sugu?

Mwisho ni wakati wa Sugu kuonesha alichofanya Mbeya Kwa

Basi nabishana na mtoto ina maana na hili hulijui ambalo lilitokea mwaka 2015

ana ubishi wa kitoto na wakati mambo yalikua wazi nimeshangaa hadi hilo alikua halijui

Magufuli alichukua mamlaka za halmashauri na hiki kitendo wadau wengi wa maendeleo walikipinga sana na baada ya kuchukua hizo mamlaka akawa na ujasiri wa kusema hapeleki maendeleo kwa majimbo ya wapinzani sababu hata wakiomba hela za maendeleo anapiga chini hilo ombi
Maendeleo ya vitu (majengo na Barabara) ni lazima yafanyike tu maadamu kodi za wananchi zinaendelea kukusanywa, tusipoona maendeleo ya vitu basi tunatakiwa tuweke mgomo wa kulipa kodi, sasa mtuambie kipindi hicho magufuli ameitupa mbeya pesa zetu alimoatia nani maana alifanya makusudi ili tuchukie wapinzani, na kama maendeleo ya vitu yataendelea kuja bila kujali kiongozi ni msomi au si msomi basi kiongozi bora hawezi kupimwa kwa hivi vitu bali atapimwa kwa ubunifu mwingine wa kuwapa watu furaha pasipo kuhitaji matumizi ya pesa mfano kutunga sheria nzuri, mikataba mizuri, kupinga ufisadi, kuondoa ukabila, na mambo mengine mengi mfano nyerere mpaka leo anakumbukwa kwa kuondoa ukabila na sio kwa kujenga Barabara na shule (maana hivi ni wajibu maadamu kodi ipo inatozwa) kwa maana hiyo hatuwezi kumkumbuka tulia kwa mabarabara bali tutamkumbuka kwa ubaya wa kutusaliti bungeni na kuuza bandari zetu na kutunga sheria za tozo kwa watanzania,nk. Kwa maana hiyo hafai kuwa mbunge anatupunguzia raha duniani
 
Samia na Tulia wanapiga kote kote vitu na Ustawi wa jamii.
 
Back
Top Bottom