Spika Dkt. Tulia Ackson: Mbeya Watanikumbuka Kwa Ujenzi wa Barabara Njia 4

Spika wa Bunge mh.Dk.Tulia Ackson Mwansasu(PhD) Akihojiwa na Clouds kwamba anaacha alama gani Mbeya amejibu kwamba ikitokea hajaendelea kuwa mbunge basi Wana Mbeya watamkumbuka Kwa ujenzi wa Barabara ya Njia 4 Kwa miaka yake hii mi 5 ambayo amekuwa mbunge wa Jimbo la Mbeya mjini.

Japo jambo hili ndio linaonekana Kwa haraka lakini Mimi nitamkumbuka Kwa mambo Makuu mengine ma 3 ukiacha Hilo la Barabara ya Nsalaga-Ifisi njia 4. Mambo hayo ni ;
1)-Ujanzi wa Jengo la wodi ya kina Mama pale Meta la gorofa 6 ambalo limeipa hadhi Hospital ya Rufaa ya Kanda Mbeya

2)-Ameacha ujenzi wa mradi mkubwa wa Maji wa kutoka chanzo Cha mto kiwira Wilaya ya Rungwe Hadi Jijini Mbeya na Mbalizi Kwa Zaidi ya Bilioni 160.

3)-Ukamilishaji wa Uwanja wa ndege wa Songwe(Anapigania uitwe Mbeya),ikumbukwe Toka Mwandosya ameasisi ujenzi wake awamu ya Mkapa ,uwanja Imekamilika mwaka huu 2023 baada ya Kubomoa na kuijenga Upya runwaya zake,kufunga taa na jengo la Abiria.

4)-Ujenzi wa Barabara ya Igawa-Uyole-Songwe-Tunduma na Uyole-Mbalizi Bypass Kwa njia 4 Kwa Utaratibu wa EPC+F

5)-Mradi wa Tactic una components za Barabara za mtaani km 20,Masoko 3,Stand 3(Soon unaanza).

Hata kama by 2025 Miradi itakuwa haijakamilika inaendelea ila ni vitu ambavyo vinaonekana unaweza waoneaja watu wakaelewa.

----
"Nikisema Mbeya mjini watanikumbuka kwa jambo gani ni kwamba ujenzi wa barabara ya njia nne umeshaanza maana yake ile barabara itakapokamilika au hata kama haikukamilika mimi nikiwa mbunge imeshaanza hivyo siku zote watajua kwamba ilianza kujengwa wakati Mbunge akiwa fulani.

Lakini pia tunazipigania barabara za mitaa, lami zimeshaanza hapa na pale lakini ni dhahiri nchi ni kubwa hii na fedha zote haziwezi kwenda kufanya kazi Mbeya pekee kwahiyo itatuchukua muda ila tumeshaanza kazi na Wananchi wanaona"

"Watu wa Mbeya ni watu wakarimu, wenye Upendo na hivyo mimi na wao tunapendana.

Mimi kama kiongozi wa kuchaguliwa na watu ni kwamba si wote ni wanasiasa na wengine hata siasa sio wafuatiliaji ila wana mambo yao, hoja zao, changamoto zao, hivyo ukishirikiana nao kwenye zile changamoto zao wala hawasikilizi huyu kapita huku au huku wao wanataka kazi ifanyike" - Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson @TuliaAckson

My Take
Sugu wa Chadema amekuwa Mbunge miaka 10 hana hata kitu Kimoja Cha maana anaweza onesha Wananchi Ili kuja kumkumbuka.
View attachment 2748183
Nani akukumbuke wewe kibaraka wa kuuza bandari zetu. Hata kama barabara zimejengwa kwani ni hela yako? Tulifikiri mwanamapinduzi mtetezi wa umma kumbe mpigaji mchumia tumbo tu.
 
Wana Mbeya ndio watamkumbuka, Bandari Iko Dar nenda utaikuta.

Mwisho ni vyema Sugu akaonesha kazi ya ubunge wake Kwa miaka 10 badala ya kutoa mapovu Kwa Kasi ya Tulia.
 
Kazi ipi aonyeshe na wakati umeshapewa sababu
Ila ujinga mda mwingine ni tabia

2010-2015 halmashauri ya jiji la mbeya ilikua chini ya ccm nkimaanisha meya alikua wa ccm na kipindi hiki mapato ya halmashauri walikua wanaweka bank wanayotaka yaana sehemu yeyote ile wanayotaka

2015-2020
Halmashauri zikaambiwa ziwe zinaweka mapata yao hazina na sio kwenye bank za biashara tena na wawe wanaomba kama wanahitaji
Lakin bado unashupaza shingo hutaki kukubali ukweli

Tokea 2015 kurudi nyuma hadi uhuru 1961 halmashauri ya mbeya mjini ilikua chini ya ccm wamefanya nini yaani miaka 56 hakuna cha maana walichofanya unakuja mlaumu chama kilichotawala kwa miaka 5 tena kwa figusu nyingi na ukahakikisha hela zake hakai nazo
Huo ni ujinga
 
Spika wa Bunge mh.Dk.Tulia Ackson Mwansasu(PhD) Akihojiwa na Clouds kwamba anaacha alama gani Mbeya amejibu kwamba ikitokea hajaendelea kuwa mbunge basi Wana Mbeya watamkumbuka Kwa ujenzi wa Barabara ya Njia 4 Kwa miaka yake hii mi 5 ambayo amekuwa mbunge wa Jimbo la Mbeya mjini.
Kazi ya mbunge sio kujenga Barabara ila ni kuisimamia serikali na kutunga sheria. Sasa asisahau hiyo part ya 2 ambayo yeye kama Spika amesimamia sheria mbovu kutungwa na amefeli kabisa kuhakikisha bunge linaitumia ripoti ya CAG kuinyoosha serikali.

Sitta hakuna alichofanya jimboni kwake ila ana legacy kubwa mnoo sababu ya jinsi bunge lilifanya kisawasawa kazi ya kuisimamia serikali
 
Toa shobo na upumbavu wako hapa,asingeisimamia hiyo Serikali ingeleta pesa za kujenga Barabara na miradi mingine Mbeya?

Kama hakuna alichofanya huko Jimboni haya niliyoandika ulifanya wewe na Sugu?

Mwisho ni wakati wa Sugu kuonesha alichofanya Mbeya Kwa miaka 10.
 
Wana Mbeya ndio watamkumbuka, Bandari Iko Dar nenda utaikuta.

Mwisho ni vyema Sugu akaonesha kazi ya ubunge wake Kwa miaka 10 badala ya kutoa mapovu Kwa Kasi ya Tulia.
Kwani miradi mingapi mlikua mnaipiga chenga kisa kuogopa kumpa sugu credit? Na hii tabia hata Dar mlifanya, Kuna mradi wa Maji ulichepushwa usipite ubungo kisa kuogopa kumpa Mnyika credit!! Alafu mkibaki wenyewe ndio mnafanya eti ionekane mbunge wa CCM ndio kafanya!!

Mbeya sio mbumbumbu hivyo na Tulia anajua hilo so ajiandae kisaikolojia 2025 unless Jimbo ligawanywe.
 
Chadema iliongoza Jiji la Mbeya, onyesheni miradi mliyobuni na kutekeleza badala ya kutafuta excuses za kijinga.

Na kama Mbeya haipati miradi Kwa Ajili ya Chadema,Kwa nini kuchagua chama kinacholeta hasara?
 
Mradi wa kiwira kupeleka maji mbeya mjini sugu aliuongelea mara nyingi sana ila kwa sababu ni mpinzani haukutekelezwa

Tulia alichofanya ni kuchukua idea ya sugu na kuitekeleza ndo maana hakuna mtu mwenye akili anakubaliana na ujinga wa mleta uzi
 
Chadema iliongoza Jiji la Mbeya, onyesheni miradi mliyobuni na kutekeleza badala ya kutafuta excuses za kijinga.

Na kama Mbeya haipati miradi Kwa Ajili ya Chadema,Kwa nini kuchagua chama kinacholeta hasara?
2015-2020
Halmashauri zikaambiwa ziwe zinaweka mapata yao hazina na sio kwenye bank za biashara tena na wawe wanaomba kama wanahitaji
Lakin bado unashupaza shingo hutaki kukubali ukweli
 
Mwisho ni wakati wa Sugu kuonesha alichofanya Mbeya Kwa miaka 10.
Mbona ameeleza siku anaaga mwezi wa 7 Ile 2020.... Au unajitoa ufahamu.
shobo na upumbavu wako hapa,asingeisimamia hiyo Serikali ingeleta pesa za kujenga Barabara na miradi mingine Mbeya?
Huelewi maana ya oversight mfano serikali imejenga barabara ni kazi ya bunge kuhakikisha hakukuwa na ufisadi, quality ni sawa na hakuna unnecessary delays. Sasa huyo Dr Tulia anajua Kuna zaidi ya billion 400 ilitafunwa kwenye ripoti ya CAG amefanya Nini so far?? Hiyo ndio primary kazi ya mbunge.

Kingine kwenye utungaji sheria, hapo ndio Kuna sheria mbovu kama zile za tozo kwenye miamala ya kielektroniki, kupandisha bei ya bundles, tozo kwenye miamala ya benki, sheria mbovu za uwekezaji, bajeti hewa, alafu unakuja kuongelea Barabara ndio kipimo Cha utendaji wa SPIKA??

You can't be serious
 
Mbona ameeleza siku anaaga mwezi wa 7 Ile 2020.... Au unajitoa ufahamu.

Huelewi maana ya oversight mfano serikali imejenga barabara ni kazi ya bunge kuhakikisha hakukuwa na ufisadi, quality ni sawa na hakuna unnecessary delays. Sasa huyo Dr Tulia anajua Kuna zaidi ya billion 400 ilitafunwa kwenye ripoti ya CAG amefanya Nini so far?? Hiyo ndio primary kazi ya mbunge.

Kingine kwenye utungaji sheria, hapo ndio Kuna sheria mbovu kama zile za tozo kwenye miamala ya kielektroniki, kupandisha bei ya bundles, tozo kwenye miamala ya benki, sheria mbovu za uwekezaji, bajeti hewa, alafu unakuja kuongelea Barabara ndio kipimo Cha utendaji wa SPIKA??

You can't be serious
Nataka wewe hapo unitajie Ili tuweke kumbuka
 
Na kama Mbeya haipati miradi Kwa Ajili ya Chadema,Kwa nini kuchagua chama kinacholeta hasara?
Na ndio maana wanataka kumuadhibu Dr Tulia maana haiwezekani mnahujumu mkoa mzima kisa tu umewakataa kwenye sanduku la kura.

Kodi inalipwa na Kila mtu wakiwemo CHADEMA Sasa wewe unaona ni sawa mkoa uhujumiwe kisa chama? Basi msikusanye Kodi za wanachadema.
 
Mtu mwenye akili timamu hawezi mchagua kiasi kama Sugu labda uwe dishi.
 
Na ndio maana wanataka kumuadhibu Dr Tulia maana haiwezekani mnahujumu mkoa mzima kisa tu umewakataa kwenye sanduku la kura.

Kodi inalipwa na Kila mtu wakiwemo CHADEMA Sasa wewe unaona ni sawa mkoa uhujumiwe kisa chama? Basi msikusanye Kodi za wanachadema.
Rais, wabunge zaidi ya asilimia 80, wakurugenzi wote wanatoka ccm tokea ila huwezi amini lawama anapewa chadema kwa umaskin wa nchi hii baada ya miaka 60+ ya uhuru
 
Ulitaka nionekane mpuuzi kama wewe chawa wa Sugu?
Unaona ulivyo na akili fupi sasa. Yan mnadhani kila anayekuja kuongelea siasa basi ni chawa wa chama fulani. Wengine tunatumia elimu zetu sawasawa hatuna huo utopolo wa uchawa. Msingi wa swali langu ulikua direct kukufirisha lakini kwa bahati mbaya akili kisoda ukakurupuka kunijibu tofauti.

Rudia kusoma halafu kaa chini utafakari nilitaka kumaanisha nini? Am not too old but also not that young for this
 
Wewe chawa wa Sugu,onesheni mlichofanya miaka 10,blaa blaa hapana.
 
Back
Top Bottom