Spika Dkt. Tulia Ackson: Mbeya Watanikumbuka Kwa Ujenzi wa Barabara Njia 4

Umejibiwa upotoshaji wako umeamua kubadilisha gia
Hata huo mradi wa kiwira sugu aliongea kipindi magufuli kafanya ziara mkoa mbeya
Sugu alisema suluhisho la maji mbeya ni kuchukua mto kiwira mimi niliona kwenye taarifa ya habari lakin leo unamsifia tulia
Hakuna gia iliyobadilika sana sana naongeza mafuta.

Mipango sio matumizi, maneno hayajengi gorofa
 
Spika wa Bunge mh.Dk.Tulia Ackson Mwansasu(PhD) Akihojiwa na Clouds kwamba anaacha alama gani Mbeya amejibu kwamba ikitokea hajaendelea kuwa mbunge basi Wana Mbeya watamkumbuka Kwa ujenzi wa Barabara ya Njia 4 Kwa miaka yake hii mi 5 ambayo amekuwa mbunge wa Jimbo la Mbeya mjini.

Japo jambo hili ndio linaonekana Kwa haraka lakini Mimi nitamkumbuka Kwa mambo Makuu mengine ma 3 ukiacha Hilo la Barabara ya Nsalaga-Ifisi njia 4. Mambo hayo ni ;
1)-Ujanzi wa Jengo la wodi ya kina Mama pale Meta la gorofa 6 ambalo limeipa hadhi Hospital ya Rufaa ya Kanda Mbeya

2)-Ameacha ujenzi wa mradi mkubwa wa Maji wa kutoka chanzo Cha mto kiwira Wilaya ya Rungwe Hadi Jijini Mbeya na Mbalizi Kwa Zaidi ya Bilioni 160.

3)-Ukamilishaji wa Uwanja wa ndege wa Songwe(Anapigania uitwe Mbeya),ikumbukwe Toka Mwandosya ameasisi ujenzi wake awamu ya Mkapa ,uwanja Imekamilika mwaka huu 2023 baada ya Kubomoa na kuijenga Upya runwaya zake,kufunga taa na jengo la Abiria.

4)-Ujenzi wa Barabara ya Igawa-Uyole-Songwe-Tunduma na Uyole-Mbalizi Bypass Kwa njia 4 Kwa Utaratibu wa EPC+F

5)-Mradi wa Tactic una components za Barabara za mtaani km 20,Masoko 3,Stand 3(Soon unaanza).

Hata kama by 2025 Miradi itakuwa haijakamilika inaendelea ila ni vitu ambavyo vinaonekana unaweza waoneaja watu wakaelewa.

----
"Nikisema Mbeya mjini watanikumbuka kwa jambo gani ni kwamba ujenzi wa barabara ya njia nne umeshaanza maana yake ile barabara itakapokamilika au hata kama haikukamilika mimi nikiwa mbunge imeshaanza hivyo siku zote watajua kwamba ilianza kujengwa wakati Mbunge akiwa fulani.

Lakini pia tunazipigania barabara za mitaa, lami zimeshaanza hapa na pale lakini ni dhahiri nchi ni kubwa hii na fedha zote haziwezi kwenda kufanya kazi Mbeya pekee kwahiyo itatuchukua muda ila tumeshaanza kazi na Wananchi wanaona"

"Watu wa Mbeya ni watu wakarimu, wenye Upendo na hivyo mimi na wao tunapendana.

Mimi kama kiongozi wa kuchaguliwa na watu ni kwamba si wote ni wanasiasa na wengine hata siasa sio wafuatiliaji ila wana mambo yao, hoja zao, changamoto zao, hivyo ukishirikiana nao kwenye zile changamoto zao wala hawasikilizi huyu kapita huku au huku wao wanataka kazi ifanyike" - Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson @TuliaAckson

My Take
Sugu wa Chadema amekuwa Mbunge miaka 10 hana hata kitu Kimoja Cha maana anaweza onesha Wananchi Ili kuja kumkumbuka.

Atuambie katoa wapi pesa??? Yaani hizi barabara zinajegwa na kodi na mikopo ya world bank na plan zilikuwepo kwa miaka mingi sasa unasema umejenga wewe!. Hata airport atasema amejenga yeye
 
Zinajengwa Kwa Mkopo upi? Kazi ya mbunge ni kujenga au kuisimamia na kuishawishi Serikali kutimiza wajibu wake Kwa Wananchi?

Mwisho mipango sio matumizi,ukitekeleza Mpango unapongezwa sio kuleta taarabu za sijui mipango ilokuwepo na blaa na.blaa za kijinga hapa.
 
Huo mda mrefu ndio haikutekelezwa Bali imetekeleza Sasa hivi awamu ya Spika Kwa heshima yake na amekuwa anapigia kelele mara nyingi.

Kama ni kupangwa aisee imepangwa miradi Mingi sana ila hakuna kinachoendelea

Kwa hiyo mapovu hayana Cha kukusaidia,ni zamu ya Sugu na Chadema kuonesha Wakifanya nini Mbeya Kwa miaka 15?
Miradi yote ilipangwa enzi za Sugu na fedha zimepatikana sasa, tatizo liko wapi?
 
Zinajengwa Kwa Mkopo upi? Kazi ya mbunge ni kujenga au kuisimamia na kuishawishi Serikali kutimiza wajibu wake Kwa Wananchi?

Mwisho mipango sio matumizi,ukitekeleza Mpango unapongezwa sio kuleta taarabu za sijui mipango ilokuwepo na blaa na.blaa za kijinga hapa.

Aonyeshe wananchi kajengaje barabara. Hizo ramani za barabara zilikuwepo kabla ya huyu tapeli, uchambuzi wa mazingira waliofanya hata hawajui. Yaani ushamba wa watu ni kwamba Mbunge ndiye anajenga!. Serikali ndiyo inajenga na ni mipango ya miaka mingi au Sugu au Tulia. Huyu mbunge kaleta utamaduni wa wizi tu hakuna kitu ni bora Sugu analeta uwekezaji wa wafanyabiashara. Hata Samia rafiki yake ni Sugu kwasababu najua ukweli wa unafiki wa huyu Dada
 
Kwani umeandika nini mbona ni mapovu matupu,vipi Kuna shida mahala?

Mipango sio matumizi unless hujui kazi ya Mbunge vs Serikali.

Uwekezaji wa wafanyabiashara unaletwaje na Mbunge?

Mwisho Sugu aoneshe amefanya nini Kwa miaka 10 aliyokaa Mbeya kama mbunge vinginevyo haya mapovu Yako ni matapishi tuu.
 
Wabunge hawajengi chochote huo ndiyo ukweli awe Sugu au Tulia. Lakini wanataka kuamknisha watu huu uongo mkubwa. Mfano mpango wa hiyo barabara ulikuwepo toka zamani sasa mbunge kaleta nini? Pesa tuonyeshe pesa mbunge kailetaje! . Huu uongo pelekeni kwa wasiojua. Wewe ndiye hujui kazi ya mbunge kasome tena majukumu.
 
Ukiona namfagilia mtu ujue amefanya jambo zuri,Mimi sio mshabiki wa Vyama.

Hata Samia namfagilia Kwa sababu anafanya mambo mazuri ya kuonekana.

Mwisho Kuna ujumbe hapa 👇View attachment 2747976
Kwa Tulia siyo bure, nimefuatilia posts zako nyingi. Hauko fair hata anapokuwa critised kwa vitu vya wazi, wewe utatetea tu. If you are not in her payroll, you are either a family member or very close associate
 
Spika wa Bunge mh.Dk.Tulia Ackson Mwansasu(PhD) Akihojiwa na Clouds kwamba anaacha alama gani Mbeya amejibu kwamba ikitokea hajaendelea kuwa mbunge basi Wana Mbeya watamkumbuka Kwa ujenzi wa Barabara ya Njia 4 Kwa miaka yake hii mi 5 ambayo amekuwa mbunge wa Jimbo la Mbeya mjini.
Hopeless phd ya rushwa ya kuuza bandari
 
Alafu hata kumlaumu sugu ni ujinga wa wazi wazi

halmashauri ya jiji la mbeya ilikua chini ya ccm tokea 2010 mpaka 2015
Wakati chadema wamechukua halmashauri ya jiji la mbeya mwaka 2015 magufuli akasema hapeleki maendeleo kwa majimbo ya upinzani hapo unamlaumuje sugu
Sahihisho: Halmashauri ya Jiji la Mbeya ilikuwa chini ya CCM mwaka 2000-2010. Sugu aliingia 2010- 2015 halafu 2015-20.

Tulia ameingia 2020 baada ya Magufuli kumpa ubunge wa bila kupigiwa kura
 
Mzee unafeli sana,tatizo sio mipango Wala mikakati Bali ni mtu wa ku push utekelezwaji wa Mipango.

Hata bwawa la Nyerere lilikuwepo kwenye Mpango lakini anasifiwa Mwendazake aliyeamua kutekeleza.

12 September 2022
Mbeya, Tanzania

ENEO LA AJILI ILIYOUA WATU 25 / MAKAMU WA RAIS ATEMBELEA NA KUZUNGUMZA HAYA MBEYA/ATOA MAAGIZO POLISI

View: https://m.youtube.com/watch?v=xrNYtEJcZjs&pp=ygUkTWFrYW11IHdhIFJhaXMgTXBhbmdvIGFqYWxpIHphIG1iZXlh

Makamu wa Rais Philip Mpango tarehe 12 September 2022 akazia mkazo suala la barabara zijengwe kupunguza ajali Mbeya
 
Jengo la hospital ya meta limeanza kujengwa lini???yaani kisa uchawa unataka kuleta upimbi wako hapa???? Tuambie jengo limeanza kujengwa mwaka gani
 
12 September 2022
Mbeya, Tanzania

ENEO LA AJALI ILIYOUA WATU 25 / MAKAMU WA RAIS ATEMBELEA NA KUZUNGUMZA HAYA MBEYA/ATOA MAAGIZO POLISI

View: https://m.youtube.com/watch?v=xrNYtEJcZjs&pp=ygUkTWFrYW11IHdhIFJhaXMgTXBhbmdvIGFqYWxpIHphIG1iZXlh

Makamu wa Rais Philip Mpango tarehe 12 September 2022 akazia mkazo suala la barabara zijengwe kupunguza ajali Mbeya

01 August 2023​

MAKAMU WA RAIS DR. MPANGO ATEMBELEA TENA BARABARA YA INYALA MBEYA, KUKAZIA KAZI IISHE​

View: https://m.youtube.com/watch?v=1eZ1uKKxNQc
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango ameupongeza uongozi wa Wakala ya Barabara nchini (TANROAD) pamoja na Mkoa wa Mbeya kwa usimamizi mzuri na kukamilisha ujenzi wa barabara ya mchepuko katika eneo la mlima wa Inyala mkoani Mbeya.

Makamu wa Rais amesema hayo wakati akikagua barabara ya mchepuko katika Mlima Inyala iliogharimu shilingi bilioni 6.9 leo tarehe 01 Agosti 2023.

Amesema eneo hilo lilikuwa likikabiliwa na ajali nyingi zilizogharimu Maisha ya watu hivyo kukamilika kwa ujenzi wa barabara hiyo utasaidia katika kukabiliana na adha hiyo.

Makamu wa Rais ametoa rai kwa madereva na watumiaji wa vyombo vya moto nchini kuwa waangalifu na kufuata sheria za usalama barabarani ili kunusuru Maisha ya watumiaji wa barabara.

Ametoa wito kwa madereva kujenga utaratibu wa kukagua magari mara kwa mara ili kuepusha ajali zinazoweza kujitokeza kutokana na ubovu wa vyombo vya moto.

Aidha Makamu wa Rais amewataka askari wa usalama barabarani kufanya kazi kwa uadilifu kwa kusimamia sheria za usalama barabarani ili kulinda Maisha ya wananchi wanaotumia barabara hizo.

Septemba 11 mwaka 2022 Makamu wa Rais alitembelea eneo la Inyala na kuagiza mambo mbalimbali ili kukabiliana na ajali zilizokuwa zinajitokeza katika eneo hilo ikiwemo kujenga kwa kiwango cha lami barabara ya mchepuko katika mlima Inyala, kupanua ukubwa wa barabara kutoka mita 6.7 hadi mita 10.5 pamoja na kuweka taa za barabarani katika eneo la kukagulia magari
 
Spika wa Bunge mh.Dk.Tulia Ackson Mwansasu(PhD) Akihojiwa na Clouds kwamba anaacha alama gani Mbeya amejibu kwamba ikitokea hajaendelea kuwa mbunge basi Wana Mbeya watamkumbuka Kwa ujenzi wa Barabara ya Njia 4 Kwa miaka yake hii mi 5 ambayo amekuwa mbunge wa Jimbo la Mbeya mjini.

Japo jambo hili ndio linaonekana Kwa haraka lakini Mimi nitamkumbuka Kwa mambo Makuu mengine ma 3 ukiacha Hilo la Barabara ya Nsalaga-Ifisi njia 4. Mambo hayo ni ;
1)-Ujanzi wa Jengo la wodi ya kina Mama pale Meta la gorofa 6 ambalo limeipa hadhi Hospital ya Rufaa ya Kanda Mbeya

2)-Ameacha ujenzi wa mradi mkubwa wa Maji wa kutoka chanzo Cha mto kiwira Wilaya ya Rungwe Hadi Jijini Mbeya na Mbalizi Kwa Zaidi ya Bilioni 160.

3)-Ukamilishaji wa Uwanja wa ndege wa Songwe(Anapigania uitwe Mbeya),ikumbukwe Toka Mwandosya ameasisi ujenzi wake awamu ya Mkapa ,uwanja Imekamilika mwaka huu 2023 baada ya Kubomoa na kuijenga Upya runwaya zake,kufunga taa na jengo la Abiria.

4)-Ujenzi wa Barabara ya Igawa-Uyole-Songwe-Tunduma na Uyole-Mbalizi Bypass Kwa njia 4 Kwa Utaratibu wa EPC+F

5)-Mradi wa Tactic una components za Barabara za mtaani km 20,Masoko 3,Stand 3(Soon unaanza).

Hata kama by 2025 Miradi itakuwa haijakamilika inaendelea ila ni vitu ambavyo vinaonekana unaweza waoneaja watu wakaelewa.

----
"Nikisema Mbeya mjini watanikumbuka kwa jambo gani ni kwamba ujenzi wa barabara ya njia nne umeshaanza maana yake ile barabara itakapokamilika au hata kama haikukamilika mimi nikiwa mbunge imeshaanza hivyo siku zote watajua kwamba ilianza kujengwa wakati Mbunge akiwa fulani.

Lakini pia tunazipigania barabara za mitaa, lami zimeshaanza hapa na pale lakini ni dhahiri nchi ni kubwa hii na fedha zote haziwezi kwenda kufanya kazi Mbeya pekee kwahiyo itatuchukua muda ila tumeshaanza kazi na Wananchi wanaona"

"Watu wa Mbeya ni watu wakarimu, wenye Upendo na hivyo mimi na wao tunapendana.

Mimi kama kiongozi wa kuchaguliwa na watu ni kwamba si wote ni wanasiasa na wengine hata siasa sio wafuatiliaji ila wana mambo yao, hoja zao, changamoto zao, hivyo ukishirikiana nao kwenye zile changamoto zao wala hawasikilizi huyu kapita huku au huku wao wanataka kazi ifanyike" - Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson @TuliaAckson

My Take
Sugu wa Chadema amekuwa Mbunge miaka 10 hana hata kitu Kimoja Cha maana anaweza onesha Wananchi Ili kuja kumkumbuka.
View attachment 2748183
Haijalishi! 2025 tunasimama na mwenye jimbo lake, barabara huo ni wajibu wenu na sio hisani!!
 
Kwa Tulia siyo bure, nimefuatilia posts zako nyingi. Hauko fair hata anapokuwa critised kwa vitu vya wazi, wewe utatetea tu. If you are not in her payroll, you are either a family member or very close associate
Sina u close wowote na simjui na yeye hanijui
 
Back
Top Bottom