Spika Dkt. Tulia aomba jimbo la Mbeya Mjini kugawanywa

Spika Dkt. Tulia aomba jimbo la Mbeya Mjini kugawanywa

India ina watu 1.4 billon ina wabunge 788 wa upper house na lower house.Tanzania yenye watu 61M ina wabunge 360.
Africa aliye tuloga asha kufa.
Kuna wabunge 120 ambao hawana msaada kwa Tz
Mshahara wao ni Bilioni 93.6

Mafuta kila mwezi lita 120,000 zenye thamani ya Bilioni 29 kwa miaka 5

Kiinua mgongo Zaidi ya Bilioni 15

Bado Ofisi zao

Kwa ufupi hela za wabunge wasio na majimbo zinaweza jenga madarasa ya msingi na upili zaidi ya 7500 ambazo tutapunguza msongamano wa wanafunzi
 
Huyu Nguli wa sheria na Spika wa bunge ameonesha kiwango kidogo cha ufanisi kwenye siasa

Kitendo cha kutoka hadharani na kudai kuwa Jimbo la Mbeya Mjini ligawanywe ni kuonesha namna hofu na mashaka yalivyomjaa kuhusu Uchaguzi ujao.

Mara kadhaa zimetolewa mada humu kuhusu uwezo wake wa kisiasa na kuongoza jimbo la Mbeya.

Hatimaye mmepata majibu.

Kosa kubwa alilofanya ni kutoka hadharani na kuonesha udhaifu huo. Kwanini hakutumia japo Chawa wake wa mbali.

Ndio kusema chawa aliwatuma wamegoma akaamua kujilipua?
Kauli yake inapunguza ari na uaminifu kwa vyombo vya chama vinavyoteua wagombea na hivyo huenda vikambwaga chini

Kuna watu watasema aaah wapi? Spika hawezi kuangushwa jimbo wajiuliza Spika Ndugai leo yuko wapi?
Chini ya Katiba bora na Tume huru ya Uchaguzi hata PM majariwa jawezi kushinda uchaguzi kwenye Jimbo la Ruangwa.
 
Huyu Nguli wa sheria na Spika wa bunge ameonesha kiwango kidogo cha ufanisi kwenye siasa

Kitendo cha kutoka hadharani na kudai kuwa Jimbo la Mbeya Mjini ligawanywe ni kuonesha namna hofu na mashaka yalivyomjaa kuhusu Uchaguzi ujao...
Alijaribu lakini Kila chawa alichomoa
 
Huyu Nguli wa sheria na Spika wa bunge ameonesha kiwango kidogo cha ufanisi kwenye siasa

Kitendo cha kutoka hadharani na kudai kuwa Jimbo la Mbeya Mjini ligawanywe ni kuonesha namna hofu na mashaka yalivyomjaa kuhusu Uchaguzi ujao...
Ngoja tuone hitimisho lake, maana hoja ya msingi HAKUNA!
1683117229445.png
 
Mbona Zanzibar kila baada ya kilometer 2.5 kuna mbunge na kila baada ya kilometer 5 kuna mkoa ?.
Kinachowapa jeuri ni muungano, wana mahali pa kuegemea! Wasomi wao wana nafasi ya kufanya kazi Bara hivyo kuwaongezea fursa ya ajira zaidi kwao tofauti na huku Bara ni kuongeza mzigo kwa serikali.
 
Na mishahara itagawanywa nusu ?

Mimi kama mmoja ya waajiri wa hawa jamaa sioni value for money wanachofanya; Ningependekeza hata hii namba iliyopo ipunguzwe zaidi ya nusu....
 
Kwanza nashangaa hadi leo jiji la Mbeya halijagawanywa. Kwenye kampeni zake za 2020. JPM alipokuwa Mbeya alisema baraza la madiwani likiapishwa tu kikao cha kwanza kiwe kujadili kugawanywa kwa jiji la Mbeya. Naona baraza na huyo Meya wake wamezubaa sana. Huyu Tulia anakumbushia tu ahadi ya Jiwe. Ni vema mchakato ukaanza mapema.
 
Kama wanazingatia ukubwa wa jimbo na wingi wa watu, napendekeza Zanzibar wawe na majimbo matano. Matatu Unguja na mawili Pemba.

Hii ni kwa bunge la muungano; kwenye baraza lao la wawakilishi wanaweza kupanga idadi wanayoona inawafaa.
 
View attachment 2608230
Picha: Spika Dkt. Tulia Akson

Spika wa Bunge, Tulia Ackson ni miongoni wa wabunge waliowasilisha maombi ya kugawa majimbo yao ili kuwa mawili kutokana na ukubwa na wingi wa watu.

Taarifa hiyo imetolewa leo bungeni na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu Ummy Nderiananga wakati akijibu swali la nyongeza la mbunge wa Viti Maalum Sophia Mwakagenda.

Katika swali lake Mwakagenda ameuliza ni lini serikali italigawa jimbo la Mbeya mjini ambalo linaongozwa na Spika wa Bunge Tulia Ackson kutokana na ukubwa wake.

“Mheshimiwa Tulia Ackson alishawasilisha kwenye mamlaka nia ya kuomba jimbo hilo ligawanywe, serikali inatafakari maombi hayo na wakati utakapofika vigezo vitatazamwa,” amesema Ummy.

Katika swali la msingi mbunge wa Kilindi Omari Kigua ameuliza ni lini Serikali italigawa Jimbo la Kilindi kutokana na jiografia yake.

Naibu Waziri amesema kwa sasa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ipo katika maandalizi mbali mbali ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025.

“Hivyo kwa kuzingatia taratibu na vigezo ,muda wa kugawa majimbo utakapofika Tume itatoa tangazo rasmi kwa wadau wote wa uchaguzi juu ya kuanza kwa machakato wa ugawaji wa majimbo ili wadau wawasilishe maoni na maombi yao na hivyo kushughulikiwa kwa mujibu wa vigezo vilivyowekwa kikatiba,”amesema Ummy.

Ummy amesema majimbo mengi yameomba kugawanywa lakini mambo yanayotazamwa ni pamoja na ukubwa wa ukumbi wa bunge, idadi ya wabunge wa viti maalumu na jiongrafia za maeneo yaliyoomba kugawanywa.

Chanzo: Mwananchi
Sugu ngoma nzito
Inaitwa pasu kwa pasu
 
Waweke kabisa vigezo vya Jimbo kugawanywa ili vigezo vikifikiwa automatically Jimbo ligawanyike
 
Back
Top Bottom