Kuna wabunge 120 ambao hawana msaada kwa TzIndia ina watu 1.4 billon ina wabunge 788 wa upper house na lower house.Tanzania yenye watu 61M ina wabunge 360.
Africa aliye tuloga asha kufa.
Alijaribu lakini Kila chawa alichomoaHuyu Nguli wa sheria na Spika wa bunge ameonesha kiwango kidogo cha ufanisi kwenye siasa
Kitendo cha kutoka hadharani na kudai kuwa Jimbo la Mbeya Mjini ligawanywe ni kuonesha namna hofu na mashaka yalivyomjaa kuhusu Uchaguzi ujao...
Ngoja tuone hitimisho lake, maana hoja ya msingi HAKUNA!Huyu Nguli wa sheria na Spika wa bunge ameonesha kiwango kidogo cha ufanisi kwenye siasa
Kitendo cha kutoka hadharani na kudai kuwa Jimbo la Mbeya Mjini ligawanywe ni kuonesha namna hofu na mashaka yalivyomjaa kuhusu Uchaguzi ujao...
Weka benchi hapo hapo tukae soteNgoja tuone hitimisho lake...
View attachment 2608487
Chawa bila kuwalipa huwaoni 😅😅Alijaribu lakini Kila chawa alichomoa
Yeye hata hela zake wamekulaChawa bila kuwalipa huwaoni [emoji28][emoji28]
Umemaliza kazimjinha ni wewe na familia yako pamoja na hao ccm wenzako mashoga kama tulivyotaarifiwa na masaburi kule bungeni.
Tulia kashatulizwaSugu moto chini
Kinachowapa jeuri ni muungano, wana mahali pa kuegemea! Wasomi wao wana nafasi ya kufanya kazi Bara hivyo kuwaongezea fursa ya ajira zaidi kwao tofauti na huku Bara ni kuongeza mzigo kwa serikali.Mbona Zanzibar kila baada ya kilometer 2.5 kuna mbunge na kila baada ya kilometer 5 kuna mkoa ?.
wataisoma namba 2025 kaona mbeleko limekatikakaona kuwa hatoboiiii famasiala nini
You're the next John[emoji23][emoji23][emoji23] Ufipa st wanaoshangilia
Watu wanajimilikisha Majimbo
Na sisi Iringa tunataka Jimbo la Ipogolo
Aende akagombee ChatoAmeshaona hatoboi kwa Sugu..
Kivuli tu kinafanya anastukastuka..
Sugu ngoma nzitoView attachment 2608230
Picha: Spika Dkt. Tulia Akson
Spika wa Bunge, Tulia Ackson ni miongoni wa wabunge waliowasilisha maombi ya kugawa majimbo yao ili kuwa mawili kutokana na ukubwa na wingi wa watu.
Taarifa hiyo imetolewa leo bungeni na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu Ummy Nderiananga wakati akijibu swali la nyongeza la mbunge wa Viti Maalum Sophia Mwakagenda.
Katika swali lake Mwakagenda ameuliza ni lini serikali italigawa jimbo la Mbeya mjini ambalo linaongozwa na Spika wa Bunge Tulia Ackson kutokana na ukubwa wake.
“Mheshimiwa Tulia Ackson alishawasilisha kwenye mamlaka nia ya kuomba jimbo hilo ligawanywe, serikali inatafakari maombi hayo na wakati utakapofika vigezo vitatazamwa,” amesema Ummy.
Katika swali la msingi mbunge wa Kilindi Omari Kigua ameuliza ni lini Serikali italigawa Jimbo la Kilindi kutokana na jiografia yake.
Naibu Waziri amesema kwa sasa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ipo katika maandalizi mbali mbali ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025.
“Hivyo kwa kuzingatia taratibu na vigezo ,muda wa kugawa majimbo utakapofika Tume itatoa tangazo rasmi kwa wadau wote wa uchaguzi juu ya kuanza kwa machakato wa ugawaji wa majimbo ili wadau wawasilishe maoni na maombi yao na hivyo kushughulikiwa kwa mujibu wa vigezo vilivyowekwa kikatiba,”amesema Ummy.
Ummy amesema majimbo mengi yameomba kugawanywa lakini mambo yanayotazamwa ni pamoja na ukubwa wa ukumbi wa bunge, idadi ya wabunge wa viti maalumu na jiongrafia za maeneo yaliyoomba kugawanywa.
Chanzo: Mwananchi