Wanabodi.
Sasa kwenye hili la Halima Mdee, Chadema, imejikwaa tena pale pale ilipojikwa kwenye issue ya kumtumua Zitto, safari hii Chadema bado haijaanguka na bakora za karma bado hazijaanza kutembea.
Kwa vile Zitto alikimbilia mahakamani akashindwa, Chadema wakashangilia ushindi huo, nashukuru mimi niliwaeleza humu kuwaelimisha kuhusu karma, na nikawaambia the consequences ya matendo, hivyo kwenye hili la Halima Mdee, nae amekimbilia mahakamani, ikitokea na Halima akashindwa kama alivyoshindwa Zitto, hivyo Chadema wakafanikiwa kuwatimua rasmi hao wanaowaita Covid 19, naomba mimi niwe mtu wa kwanza kuwaambia the consequences will be very devastating, kwenye karma ya Zitto, angalau someone survived miraculously, I'm not sure kwenye hili, if anyone will!. Kwa kuchelea this, nimejitolea kuishauri Chadema the right thing to do na kuepuka adhabu ya karma.
Paskali.