Spika Job Ndugai, amejiuzulu Uspika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Spika Job Ndugai, amejiuzulu Uspika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Gwajima maombi yake ya kumuondoa amaleki yamefanikiwa. Kwa hakika upepo inapoendelea kuvuma CCM bado yajayo yanafurahisha. Mungu na atupe uzima.
 
Wakiona hii inawagharimu kisiasa, Ndugai anaweza kutakiwa kukanusha na hapo itategemea na msimamo wake. All in all, hali si shwari ndani ya CCM.
 
Shinikizo la kutaka Spika ajiuzulu ktk nafasi yake limeshikiwa bango zaidi na wafuasi wa Mbowe/Chadema.

Niwazi kabisa Spika alikuwa mwiba mkali sana kwa ktk kusimamia sheria na kanuni za mbunge na haswa kwa wapinzani ambao walitaka kuleta mchezo.

Sasa leo hii hatuwezi kushangaa kuona genge la Mbowe likishangilia na kupiga mayowe eti Spika ajiuzulu.

Kamwe wana CCM Makini wasikubali kuingia ktk mtego huuu.

Inatosha na Inatosha sana kwa kitendo cha kiungwana alicho kifanya Spika cha kuomba radhi.

Kamwe tusikubali kuendelea kumdhalalisha Spika wetu aliye fanya kazi kwa umahiri mkubwa na kuisaidia nchi yetu.

Ni vyema wana CCM wakawa makini ktk kipindi hiki cha upepo mbaya, wapaswa kuwa watulivu na nidhamu ya hali ya juu.
Mungu Ibariki Tanzania.
Kazi iendeleee kama kawaida.
Hebu na wewe katafute mavi ya kuku ubanje.
 
Nchi hii bana noma Sasa uhuru wake uko wapi hongera mzee heri nusu Shari kuliko Shari kamili wewe ni shujaa umethubutu Mungu atakuvesha hii ni aibu ya dunuani Kwa Mungu uko salama kwani mang'ung'uniko c mazuri ya wanadamu baki na ubunge wako kwani cheo ni dhamana
 
  • Thanks
Reactions: nao
kitendo cha Muhimili mmoja kuweza kushinikiza mkuu wa Muhimili mwingine kujiuzulu ni hatari kwa nchi.

Ni dalili ya Taifa ambalo limefika mwisho na limekufa.Siyo jambo la kushangilia kwa yeyote yule mwenye akili timamu.
1641469238_1641469238-picsay.jpg
 
Hili haliachi alama nzuri kwa Taifa letu! Hata Ndugai awe amekosea kiasi gani lakini ipo mbegu mbaya sana imepandwa ambayo toka uhuru haijawahi kutokea!

Tuna safari ndefu sana na kutokubaliana na Ndugai kwenye mengi hakufanyi nipuuze namna alivyoshughulikiwa pamoja na nafasi yake.
Hamna lolote,
Mungu yupo kazini kutuondolea mashetani.
Huyu ni shetani wa pili kuondoka kwenye mfumo.
 
Back
Top Bottom