Spika Job Ndugai, amejiuzulu Uspika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Spika Job Ndugai, amejiuzulu Uspika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Amechelewa kuchukua maamuzi, ule msamaha alioomba ilitakiwa uendane na kujiuzulu.
 
Habari njema na Nuru mpya Kwa democrasia , uhuru wa kweli na haki katika taifa letu nauona mwanzo mpya Kwa bunge litakalo tekeleza wajibu wake ipasavyo, Sasa tuhamie Kwa wale wa NEC na wanaokwamisha kupatikana katiba mpya .
Hujui hata unachoandika yaani huoni kama huyo spika ajaye ndio atakuwa meaningless kabisa maana hatosema kitu hata kama ni kibaya kwa kuogopa yaliyomkuta mtangulizi wake, au democracy ni kila asemacho/afanyacho Rais kila mtu lazima aseme YES

Tanzania inapoteana na watanzania wenyewe wapo tu as if kila mtu ameisusa nchi so aliye on top anafanya anachojisikia bila bughuza yoyote. Ila twende tu Time will tell

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Shinikizo la kutaka Spika ajiuzulu ktk nafasi yake limeshikiwa bango zaidi na wafuasi wa Mbowe/Chadema.

Niwazi kabisa Spika alikuwa mwiba mkali sana kwa ktk kusimamia sheria na kanuni za mbunge na haswa kwa wapinzani ambao walitaka kuleta mchezo.

Sasa leo hii hatuwezi kushangaa kuona genge la Mbowe likishangilia na kupiga mayowe eti Spika ajiuzulu.

Kamwe wana CCM Makini wasikubali kuingia ktk mtego huuu.

Inatosha na Inatosha sana kwa kitendo cha kiungwana alicho kifanya Spika cha kuomba radhi.

Kamwe tusikubali kuendelea kumdhalalisha Spika wetu aliye fanya kazi kwa umahiri mkubwa na kuisaidia nchi yetu.

Ni vyema wana CCM wakawa makini ktk kipindi hiki cha upepo mbaya, wapaswa kuwa watulivu na nidhamu ya hali ya juu.
Mungu Ibariki Tanzania.
Kazi iendeleee kama kawaida.
Sukumq gang
 
Hili haliachi alama nzuri kwa Taifa letu! Hata Ndugai awe amekosea kiasi gani lakini ipo mbegu mbaya sana imepandwa ambayo toka uhuru haijawahi kutokea!

Tuna safari ndefu sana na kutokubaliana na Ndugai kwenye mengi hakufanyi nipuuze namna alivyoshughulikiwa pamoja na nafasi yake.
Mbona hajashughulikiwa popote? Yeye aliongea jukwaani na akajibiwa majukwaani! Angeongea kamati kuu angejibiwa huko na tusingesikia hizi chokochoko zote, hata angeongea bungeni angejibiwa huko bungeni, wangebishana, angeweza hata kutoa ufafanuzi. Haya maamuzi mengine aliyofanya ni uoga na ujinga wake
 
Mfungo wa massa 72 Toka kwa mchungaji Gwajima hatimae Mungu amesikia Sala na maombi yake.

Amaleki ndio hivyo Tena. Kaondoka mwenyewe. Keeli Mungu hujibu maombi.
Hakuna lolote hapo maana wote ni sukuma gang
 
Back
Top Bottom