Spika Job Ndugai, amejiuzulu Uspika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Spika Job Ndugai, amejiuzulu Uspika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

hivi wewe hujui ccm ndio kila kitu? kuna katiba nchi hii? mkiambiwa tunataka katiba mpya mnabambkia kesi za ugaidi, wacha waparulane wenyewe kwa wenyewe, Majaliwa kaa mguu sawa
Naona kama anatupiwa virago kwenye listi inayo kuja kesho kutwa
 
Hujui hata unachoandika yaani huoni kama huyo spika ajaye ndio atakuwa meaningless kabisa maana hatosema kitu hata kama ni kibaya kwa kuogopa yaliyomkuta mtangulizi wake, au democracy ni kila asemacho/afanyacho Rais kila mtu lazima aseme YES

Tanzania inapoteana na watanzania wenyewe wapo tu as if kila mtu ameisusa nchi so aliye on top anafanya anachojisikia bila bughuza yoyote. Ila twende tu Time will tell

Sent using Jamii Forums mobile app
Tutamhukumu kama alivyohukumiwa mtangulizi wake.
 
images.jpg
 
Pamoja na elimu yake ya hapa na pale anajua maana na matumizi ya kuwa na mihimili mitatu ya dola,anafahamu kila muhimili uko huru, na anajua kwakuwa maisha ya kila siku yanatawaliwa na muhili wa serikali basi Kuna uwezwkano serikali ikavunja katiba na sheria hivyo mihimili ya bunge na mahakama imepewa mamlaka ya kuisimamia na hata kuizuia serikali isivunje katiba ,sheria na haki za raia.Hayo yote yeye aliyapuuza nadhani kwa kile ambacho late Rev.Christopher Mtikila alikiita ugonjwa wa manyani uiteao Apedomia.Mkuu huyu wa muhimili alisimama udhalilishaji wa wabunge wenzake.Kuna waliofukuzwa bungeni kama mbwa,Kuna waliosimamishwa kuhudhuria viakao,Kuna waliodhalilishwa kwa kuitwa walevi na Kuna waliotolewa mjengoni kwa staili ya Tanganyika jeki.Kibaya zaidi ni pale alipomtaja mbunge aliyeshambuliwa kwa risasi akiwa kazini kwamba yuko kuzurula na akampoka Ubunge wake na stahiki zake,Kuna mwingine alitandikwa rungu kichwani wakati wa kura za maoni ndani ya chama chake.Malipo yamekuja haraka Sana,kwa kuwa watesi walikuwa wengi,je ni nani anafuata?
 
Mimi bado sijaamini.
Ila kwa kauli zile za Mwenye nyumba angwezaje kuendekea kukalia kiti kile?
Kama ni kweli,basi amechukua uamzi sahihi .
 
Kosa la ndugai liko wapi kwa mjibu wa sheria? Je, ndugai kavunja katiba katika kutoa maoni yake...!

Kosa la ndugai, linapaswa liwe la kichama na si kama anavyosakamwa aachie ngazi!

Kwa katiba ipi na sheria ipi inayodai sipika akitoa maoni yake kuhusu jambo la kiserikali atawajibika/wajibishwa?

Chama ndicho chaweza kumwajibisha ikiwa ziko taratibu za aina hiyo ila si kwa kumvua madaraka ya usipika!

Ngoja litokee hili, Tutajiona mapanzi mbele ya dunia kwa jinsi itavyoonyesha katiba yetu isivyiheshimiwa na kujitoshereza!

Sasa nimeelewa kwamba, Tz katiba yetu ni mbovu kuliko chochote!

Kwa nchi zenye watu wenye kupima ukweli wa jambo kupitia katiba walizonazo, Kusingeeleweka ikiwa sipika anashinikizwa kuachia ngazi kwa jambo ambalo halipo kikatiba

Mh Sipika ni mkuu wa mhimili unaojitegemea, lkn pia ni RAIA wa Tz mwenye Uhuru wa kutoa maoni yake katika jambo lolote lile huku akizingatia sheria za nchi

Niko na Ndugai na hana kosa kisheria na kikatiba
Unalia nini? Umeambiwa kajiuzulu, au Kuna mahali wamesema wamemfukuza? Kajiondoa mwenyewe baada ya kujiona ni pumbavu
 
Angalia udhaifu wa katiba, haizungumzii spika kujiuzulu na utaratibu wa kujiuzulu
Kifungu cha 84 cha katiba kiko hivi:
84.-(1) Kutakuwa na Spika wa Bunge ambaye atachaguliwa na

Wabunge kutoka miongoni mwa watu ambao ni Wabunge au

wenye sifa za kuwa Wabunge; atakuwa ndiye kiongozi wa Bunge

na atawakilisha Bunge katika vyombo na vikao vingine vyote nje

ya Bunge.



(7) Spika atakoma kuwa Spika na ataacha kiti cha Spika

litokeapo lolote kati ya mambo yafuatayo -

(a) iwapo mtu huyo alichaguliwa kutoka miongoni mwa

Wabunge, basi ikiwa atakoma kuwa Mbunge kwa

sababu yoyote ambayo haihusiki na kuvunjwa Bunge;

au

(b) ikiwa kutatokea jambo lolote ambalo, kama

asingekuwa Spika, lingemfanya mtu huyo asiwe na

sifa za uchaguzi au apoteze sifa za uchaguzi wa

Spika; au

(c) Bunge litakapokutana kwa mara ya kwanza baada ya

Uchaguzi Mkuu uliofanywa baada ya Bunge kuvunjwa,

lakini masharti ya aya hii yatatumika bila ya kuathiri

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

masharti ya ibara ndogo ya (4) ya ibara ya 90 ya

Katiba hii; au

(d) ikiwa mtu huyo ataondolewa kwenye madaraka ya

Spika kwa azimio la Bunge lililoungwa mkono na

Wabunge amabo idadi yao haipungui theluthi mbili ya

Wabunge wote; au

(e) ikiwa mtu huyo atashindwa kuwasilisha kwa Rais

tamko rasmi kwa mujibu wa masharti ya ibara ndogo

(5) ya ibara hii; au

(f) ikiwa mtu huyo atapatikana na hatia kwa kosa la kutoa

habari za uongo, kwa kiapo kinyume cha sheria ya

Kanuni ya jinai, kuhusu tamko rasmi lolote lililotolewa

kwa mujibu wa masharti ya ibara ndogo ya (3) ya ibara

hii; au

(g) ikiwa mtu huyo atashindwa kuwasilisha kwa Rais

taarifa ya mali kwa mujibu wa masharti ya ibara ndogo

ya (5) ya ibara hii kabla ya kumalizika muda uliowekwa

kwa ajili hiyo kwa mujibu wa sheria iliotungwa na

Bunge;

(h) ikiwa itathibitika kuwa mtu huyo amevunja masharti ya

Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma;
 
Bora kaondoka mnafiki mkubwa Ndugai Ndumila kuwili asiye na haya


wote mliokuwa mkimpigia Magufuli vigelegele na baada ya kufa mkaanza kumponda hadharani achieni ngazi wapuuzi nyie

Mwacheni mana Samia aunde timu yake isiyobeba MI ndumila kuwili kama huyo Ndugai
Yehodawa umeandika jambo kubwa sana, huyu Ndugai kabla hata ya 40 ya Magu akaanza kulilia bandari ya Bagamoyo! Wengi wao misimamo mingi wameibadili, mmojawapo jinsi ya kushughulika na COVID
 
Back
Top Bottom