Spika Makinda Afafanua mvurugano kwenye mjadala wa Sheria ya Mchakato wa Katiba


Hapa adhabu ya wapiga kura haitoshi. Huwezi kumtreat mtu anayekukosea heshima kwa kumheshimu. CCM wametukosea heshima na 2015 iko mbali sana kusubiri kuwaadhibu. WaTZ wanachemka kwa maghadhabu na madudu ya CCM.

Salama yao ni kufanya ukusanyaji wa maoni nchi nzima, kila kaya, kata, wilaya, mkoa. Katiba ni mali ya WaTZ na sio ya JK na mamluki wake.
 
Na hicho ndicho wanachopaswa kukifanya na hicho hicho ndicho wanachoogopa kukifanya
 
Mkuu asante kwa clarification nzuri
 
Mimi Nasubiri siku mswada utakapopelekwa bungeni niandike jina kwa jina kwa wale wabunge wote watakouunga mkono mswaada huo na majimbo yao. Hii itammanisha kwamba kila mbunge atayeuunga mkono mswada huo atakuwa anawakilisha mawazo ya wapiga kura waliomchagua na siku ya mwisho tutawauliza wapiga kura kama kweli alichokisema mbunge wao ndicho walichomtuma na kama sicho watoe hukumu inayostaili.
 
Ukiwa na spika mbumbu namna hii what do you expect? si kila siku kulalamikia chama fulani....spika anatakiwa awe independent and objective otherwise anakua hana maana yeyote. Afadhali kuwa na bunge la ccm pekee ndo ataweza kuliendesha...otherwise she is a failure!!!
 
mawazo ya kupitia njia ya mkato dhidi ya utawala huu yananijia sana siku hizi.....natamani wapotee ghafla tuanze upya
 


Pasco,

..kwa mtizamo wangu CCM ndiyo wanaojaribu kutumia mswaada wa katiba kutimiza malengo yao ya kuendelea kukaa madarakani na kukandamiza mawazo ya wapenda haki Tanzania.

..pia amani ya nchi hii itakuja kuvurugwa na CCM na serikali yake. mauaji ya Rwanda yalipangwa na kutekelezwa na serikali na chama tawala. hata vurugu zilizotokea Kenya kwa kiasi kikubwa zilichochewa na serikali na chama tawala.

..Watanzania tuwe macho.
 
Na hicho ndicho wanachopaswa kukifanya na hicho hicho ndicho wanachoogopa kukifanya

What a dilemma? inakula kwao kote kote.

Mkuu kuna novel moja inaitwa "The Doomsday Conspiracy" sijui kama uliwahi kuisoma?
 
Chadema wala hawana haja ya kutafuta mtaji wa kisiasa...kizuri kinajiuza na kibaya kinajitembeza....hizo ngonjera za makinda ni kujitembeza kwa CCM na Chadema wanajiuza wenyewe na watu kila siku wanakuja. Wala hawana haja ya kuanza kuwasaka watu. Mambo yao yanaonekana na watu wanayajua ndo maana wanapata kasi nchini na wao wabaki kuugulia maumivu tu....
 
Moja ya mambo aliyosema spika ni kwamba watu waachwe watoe maoni yao bila kuzomewa. Akasisitiza kwamba kuzomea sio utamaduni wa bunge letu. Mmmh! Yaelekea spika wa bunge letu ni msahaulifu. Amesahau wabunge (CCM+CUF+TLP+NCCR+UDP) walivyowazomea wabunge wa CDM wakati wakitoka kwenye ukumbi wa bunge (Rais alipohutubia kwa mara ya kwanza na wakati wa kupitisha sheria ya "kuunganisha" upinzani) Kweli mkuki kwa nguruwe...
 
Lazima CCM(sio serikali) wakubali kuwa approach yao katika hili imekwama...katiba wanayoitaka wao itakuwa ya hovyo kuliko hii ya sasa hivi. Watu waliokaa 1977 ni bora mara milioni kuliko hawa wa 2011. Fikiria Kombani,Werema,Tendwa et al kulinganishwa na akina Warioba?
 
CCM na serikali hawana pa kukwepea wamekamatika kila kona. Kama wangejua wangeacha kupambana na chadema maana hawajui chadema ndo nguvu ya uma. Kama wanataka kumalizia miaaka yao 5 bora wangekaa kimya kama mazuzu maana hakuna mwananchi mwenye akili anayesikiliza upuuzi wa CCM.
Nadhani wabunge wa ccm hawajui kama walko uchi kila mtu akiwachora na kuwasubiria siki ya hukumu yao.

Kama watacheza na mchakato huu wa katiba wakidhani wao ni wajanja, basi wajue hawana maisha marefu.
Waangalie majira na nyakati lasivyo aibu iko mlangoni kwao.
Ninawatakia wapiganaji wetu maisha marefu na wasichoke na wala kuogopa wananchi tupo nyuma yenu na tunawapenda CHADEMA! Hongera Lema kwa kuwa mtu usiyebadilika msimamo! Dr. Slaa na Mbowe nyie ndiyo mmeshika usukani wa Chadema na tunawaamini mtatufikisha tunakotaka kufika!
Mungu awapingania na awape ujasiri mkuu!
 
Muswada huu unaakisi (reflect) jinsi CCM ilivyo kwa sasa. Waliodraft sio kuwa hawana uelewa bali ndiyo malengo yao yalivyo na ndicho wanakusudia.
The extents of support, opposition or arguments mean how Tanzanian consider CCM to be! Wasijidanganye, muda wa HAKI NA KWELI si wao tena labda wajaribu UCHAKACHUAJI.
 
Jaman CCM, huo mswada ni kilemaaaaaaa! na public hearing inatekelezwa kichoyo mnooooo! 2wekeeni hata wilayan, eeeeeeh?!
 
MWOSHA HUOSHWA! Au mkuki kwa nguruwe?
 
Kipindi cha kampen za uchaguzi ccm hupita nyumba kwanyuba, kitanda kwa kitanda wakigawa kofia tishet, vipeperushi na rushwa ya pesa taslim sasa iv waambie kusanya maon kwa mtindo huo huone watakavo kukimbiza!
 
nimemuangalia makinda akiwa anasoma hayo aliyotamka asubuhi. taarifa kama vile kaandaliwa. sasa kuhusu zomea zomea si wabunge wa ccm na kikwete ndo walianza kuzomea pale cdm walipotoka bungeni. sasa anakatazaje leo kuzomea?
 
Serikali ya ccm haina uwezo wa kuratibu maoni juu ya marekebisho ya katiba. serikali hii ndio imetuingiza ktk mikataba mibovu lakini mpaka leo wanaamini kuwa ni mikataba yenye tija kwa taifa. Sasa tunapozungumzia swala la katiba kwa serikali ambayo haishauriki ni kupoteza muda au kuwapa wao kibali cha kuchakachua katiba kwa maslahi yao wenyewe.
 
Watawala wanashindwa kuona mbali.
Kwa hali ilivyo sasa na huko tuendapo inaelekea kujengeka imani kwamba mtu mwenye constructive ideas kwenye jamii ni wa CHADEMA na mwenye destructive ideas ni wa CCM na serikali yake.
Nafikiri makosa yamefanyika huko nyuma namna ya kupata viongozi ambayo athari zake zinajitokeza sasa ambapo viongozi wanaonekana uelewa wao ni mdogo kuliko wanaowaongoza, kwani hata yale ya msingi kwa jamii hawayaoni.
Ukiangalia hata Bungeni, anapochangia mpinzani mara nyingi anagusa jamii moja kwa moja kuliko ilivyo kwa wachangiaji wa CCM.
 
Tanzania kwa michezo ya kuigiza hatujambo, lakini sasa lazima tujiulize ni lini tutayapa uzito unaostahili mambo muhimu ya kitaifa. Je, TBC wanataka kuwaambia wananchi kuwa ufafanuzi wa Makinda ni muhimu kuliko mjadala wenyewe uliobatizwa "public hearing" kama kiini macho ? Je, mijadala kama hii ikirushwa live, haiwezi kusaidia kupunguza misongamano ya wahudhuriaji hasa pale kumbi zinapokuwa hazitoshi ?

Ukweli ni kuwa serikali, pamoja na kukosa uwezo wa kuzuia mjadala wa madai ya katiba mpya, haina nia wala sababu ya kuhakikisha katiba mpya inapatikana. Wasiwasi ni kuwa itakapoanza kuonekana kama nguvu ya Umma inafanikiwa, serikali tayari kwa hila inapanga kuvuruga mambo kwa kisingizio cha kulinda amani na utulivu. Mbinu zinasukwa kunyamazisha Umma kwa kisingizio cha kulinda amani na utulivu.

Makinda, Tendwa, Werema, Tambwe, Bagenda na vyombo kama Polisi, TBC, UVCCM na makundi kama ya dini ni matunda tu ya usanii wa CCM. Lakini kama wasemavyo wengi sidhani kama kuna wakati huko nyuma wananchi wameweza kuwa na mwamko kama walio nao hivi sasa. Hivyo ni vizuri Kikwete na CCM wakasoma alama za nyakati na kutambua hatari itakayoikabili taifa kama watajaribu kuchakachua mjadala kama kawaida yao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…