Spika: Mazishi ya Mama Rwakatare yatahudhuriwa na watu wasiozidi 10, Serikali itasimamia

Azikwe kwa heshima zake huyo mama, kamaliza safari yake bado mimi na wewe... apumzike kwa amani.
 
1.Waziri Mkuu wa Uingereza ame-test Positive,tukaelezwa
2.Wabunge wengi Iran wamepoteza maisha, tukaelezwa
3.Mwanamfalme Charles wa Uingereza ame-test Positive, tukaelezwa
4.Kuna Kiongozi Mkuu mwingine ktk nchi kubwa ambayo nimeisahau ali-test Positive na akaamua kuji-caranteen mbali na First Lady wake, tukaelezwa
5.Wanajeshi wa Marekani kwenye Manowari na Aircraft carriers wame-test Positive,tukaelezwa
6.Trump alipima na nchi yake ikatutangazia matokeo hadharani (Japo alikuwa Negative)
7.....................(Orodha ni ndefu)
Kwetu ni siri Kuu!!!!
TUNAKWAMA WAPI?????
 
Tigershark,
Hii si lazima iwe ni korona Bali inaonekana ni tahadhari dhidi ya korona. Hivi unadhani kama watu wakiruhusiwa kuhudhuria ni maelfu wangapi watahudhuria? Kwa mazingira ya sasa haiwezekani!!
Katika eneo la kanisa hilo hilo ambako Mama Rwekatale atazikwa na watu kumi tu, kila jumapili kuna maelfu ya watu wanakusanyika kusali. Jumapili iliyopita walifurika kusali na jumapili ijayo watafurika kusali. Hivyo mantiki ya kuepuka watu kupata Corona haipo kwa 100%.

Hivi unajua idadi ya watu 10 wewe?
Yaani hapo hata baadhi ya wanafamilia wenye undugu wa damu na marehemu hawatakuwepo.

Kuna kitu cha hatari tunafichwa.
 
Serikali kuficha ficha ndio wanazidi kuongeza tatizo,wakiweka wazi kwamba amekufa kwa corona waamini wake waliofanya naye ibada j2 wangeanza kujifanyia self isolation ili kujicheck afya kwa muda lakini wakiendeleea kuficha waamini wanazidi kusambaza kitaani.
 
Jana machana maeneo ya Buguruni kituo cha polisi napewa taarifa kuwa askari mmoja alianguka akafia pale pale wakabeba wakapeleka Muhimbili. Sasa sijui wanailinda vipi Muhimbili.
Due,hivi corona inaua hata bila mtu kuugua eee?
 
Nolstagic Casanova,
CCM ni special wanaheshima ya pekee na mwenyekiti wake anatarajiwa kuteuliwa na Mungu awaongoze malaika baada ya kutuongoza watanzania vizuri sana.

Je, wewe umewahi kusikia mtu yeyote hata kule Israel akitamani kuteuliwa na Mungu ili awe kiongozi wa malaika? Ila ccm mtu huyo yupo
 
Tangu lini familia inaomba kuzika mwili sehemu fulani!
Mkuu kwa sheria za mijini huwezi kuzika mtu mahali popote bila kuomba kibali serikalini.
Hata kwenye yale makaburi ya umma lazima uombe kibali tena sehemu nyini unapeleka na kikaratasi cha kutoka hospital.

Sehemu za makazi ndiyo kabisa usithubutu kuzika mu ovyo unaweza kujikuta matatizoni kwa humu miji mikubwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…