Spika Ndugai ahoji shughuli za Serikali kurudi Dar, ataka kujua ni nani anayedhibiti matumizi ya Serikali kwa sasa

Kuna jamaa yangu mmoja yuko hapa Dar wiki hii ya pili sasa, kituo chake na familia yake ni Dom... Chakula malazi na kinywaji vyote ni hotelini.... Najiuliza hizi gharama zina uhalali wowote ?
Tunaibiwa sana sisi watanzania
 
Haya mambo ya kuonesha kwa nini kuhamishia Makao Makuu Dodoma ni makosa niliyasema tangu mpendwa Hayati JPM akiwa hai. Na alipona hoja zinamshinda akapiga mkwara wakati anazindua ujenzi wa fulaiova ya Hayati Kijazi Ubungo akisema, 'kama jambo haulipendi si unyamaze.'

Ukweli utabaki kuwa ukweli siku zote. Kufukia kodi za Watanzania Kwa kigezo cha Makao Makuu Dodoma ni ukengemfu. Ikiamliwa DSM iendelee kubakia kuwa Nakao Makuu ya nchi hii leo. Na kukaingiwa gharama za maboresho, ukajengwa mji mpya wa kiserikali DSM na Ikulu mpya bado gharama hizi hazitafikia nusu ya gharama za kuifanya Dodoma kuwa na hadhi ya Makao Makuu.

Faida yake ni kubwa zaidi, DSM itaendelea kutoa kodi kubwa zaidi. Majengo mengi ya Mifuko ya kijamii yaliyo DSM na ya wadau wengine yatapata wapangaji, yange ongeza ajira, serikali itakusanya kodi kuliko sasa ambapo yako idol tu na ni hasara kwa serikali na walio fanya huu uwekezaji.
Tamisemi ilishahamia Dodoma miaka 20 iliyopita . Je hukuliona hili?
Huna akili kabisa
 
Actually ikifika hatua fulani ya maisha ukaanza kuona wewe unaonewa basi mara nyingi huwa iko shida fulani.

Au wengine utakuta wanasema wanaroho ya kukataliwa!

Roho ya kukataliwa gani?

Imeandikwa; “Je mkitenda mema hamtapata kibali?! “

Kanuni mojawapo ya kukubarika na watu au kupendwa na watu ni pamoja na kutenda mema.

Tendea watu mema, wape watu zilizo haki zao, timiza wajibu wako kwa wakati, jisimamie, uone kama utachikiwa na watu au kuonewa na mtu yeyote!
 
Tamisemi ilishahamia Dodoma miaka 20 iliyopita . Je hukuliona hili?
Huna akili kabisa

Mwenye akili ni wewe ambaye umeacha nyumba za serikali zilizo za idadi ya kuridhisha DSM unaenda Dodoma kupangishia wafanyakazi wa serikali kutapanya kodi kama huu si ujinga tuite nini labda?! Bado institution ya ndoa ambayo imejeruhiwa sana kwa maamuzi haya ya kuwahamishia watumishi wa umma Dodoma kwa kukurupuka. Dodoma ni mradi tu wakuwatafutia wakandarasi artificial soko sasa sijui mlikuwa na intrest gani huko kwenye biashara za ukandarasi.
 
Kweli hii nchi siyo ngumu ila wananchi na viongozi wake ndiyo wagumu...
 
Actually ikifika hatua fulani ya maisha ukaanza kuona wewe unaonewa basi mara nyingi huwa iko shida fulani.

Au wengine utakuta wanasema wanaroho ya kukataliwa!

Roho ya kukataliwa gani?

Imeandikwa; “Je mkitenda mema hamtapata kibali?! “

Kanuni mojawapo ya kukubarika na watu au kupendwa na watu ni pamoja na kutenda mema.

Tendea watu mema, wape watu zilizo haki zao, uone kama utachikiwa na watu au kuonewa na mtu yeyote!

Acha kunukuu Neno la Mungu kwa kuunga unga. Ayubu alisema nilikuwa macho kwa vipofu, mguu na mikono kwa vilema kwa maana ya roho nzuri na kutoa misaada lakini bado alipigika.
 
Narudia tena acheni kumhujumu Rais Samia. Ndugai analalamika Mawaziri na Rais Samia kuonekana DSM lakni wakati JPM alipohamia Chato tena kwenye hoteli yake na convoy kubwa ya wasaidizi wake hakulalamikia hiyo expenditure wala Dodoma kuwa jeopardized. Wanafiki na wasaga sumu wakubwa.
Kutolalamika kipindi kile kwa ufujaji na matumizi ya hovyo ya JPM hakuharalishi ufujaji na matumizi ya hovyo ya SASHA
 
Spika wa bunge mh Job Ndugai leo wakati wa kuahirisha shughuli za Bunge, amewahoji mawaziri ni kwa nini kwa sasa wameamua kufanyia makongamano, warsha na semina nyingi Dar es Salaam na kuacha kufanyia Dodoma ambayo ni makao makuu ya nchi.

Ndugai ametaka kujua ni nani anayecontrol expanditure za serikali kwa sasa kwani kila mawaziri wanapofanya hizo safari za Dar wanalipana posho za kutisha pamoja na wasaidizi wao huku wakiwaacha wananchi masikini wakiwa hoi hoe hae bila huduma muhimu za jamii.

View attachment 1932327
Watanzania siyo mbumbumbu. Tunaona yanayotendeka. RIP Magu
 
Kuna jamaa yangu mmoja yuko hapa Dar wiki hii ya pili sasa, kituo chake na familia yake ni Dom... Chakula malazi na kinywaji vyote ni hotelini.... Najiuliza hizi gharama zina uhalali wowote ?

Hizi sio halali. Baadhi ya wafanyakazi wa serkali wanaona kama ni sehemu ya kujiongezea kipato.
 
Acha kunukuu Neno la Mungu kwa kuunga unga. Ayubu alisema nilikuwa macho kwa vipofu, mguu na mikono kwa vilema kwa maana ya roho nzuri na kutoa misaada lakini bado alipigika.

Mmnh!

Kwa hiyo unataka kuandikaje kwa mfano?!
 
Kutolalamika kipindi kile kwa ufujaji na matumizi ya hovyo ya JPM hakuharalishi ufujaji na matumizi ya hovyo ya SASHA
Ok! Kinachoshangaza kundi lilelile kilichokuwa kinadai Rais ni Taasisi na Ikulu ni popote nchini Tanzania leo inalalamikiaje jambo lilelile? Hapo ndo tunapoona figisu za Ndugai na kundi lake against Rais SSH
 
Kwani yeye ghaama za matibabu India nani aliidhinisha!?
 
Spika wa bunge mh Job Ndugai leo wakati wa kuahirisha shughuli za Bunge, amewahoji mawaziri ni kwa nini kwa sasa wameamua kufanyia makongamano, warsha na semina nyingi Dar es Salaam na kuacha kufanyia Dodoma ambayo ni makao makuu ya nchi.

Ndugai ametaka kujua ni nani anayecontrol expanditure za serikali kwa sasa kwani kila mawaziri wanapofanya hizo safari za Dar wanalipana posho za kutisha pamoja na wasaidizi wao huku wakiwaacha wananchi masikini wakiwa hoi hoe hae bila huduma muhimu za jamii.

View attachment 1932327
tatizo mama naye analegeza jicho mno, hivyo wanamchukulia poa.
 
Spika wa bunge mh Job Ndugai leo wakati wa kuahirisha shughuli za Bunge, amewahoji mawaziri ni kwa nini kwa sasa wameamua kufanyia makongamano, warsha na semina nyingi Dar es Salaam na kuacha kufanyia Dodoma ambayo ni makao makuu ya nchi.

Ndugai ametaka kujua ni nani anayecontrol expanditure za serikali kwa sasa kwani kila mawaziri wanapofanya hizo safari za Dar wanalipana posho za kutisha pamoja na wasaidizi wao huku wakiwaacha wananchi masikini wakiwa hoi hoe hae bila huduma muhimu za jamii.

View attachment 1932327
Contradiction is the CCM's order of the day. Fund embezzlement on the expense of its citizens. "Tozo kwenye kila aina ya huduma ili wakubwa waendelee kutumbua".
 
Nini maana ya makao makuu ya serikali kuwa Dodoma? na hiyo siyo maneno ya blah blah ni sheria......Dar ni commercial capital kama ilivyo Lagos kule Nigeria kadri watu wanavyoendelea kukamuliwa tozo ndo na safari za vigogo Dar-Dom, Dom-Dar zinavyoongezeka. Swali lililoulizwa hapa ni nani ana control government expenditure?
Jibu la swali Ndugai analijua Rais ndiyo anatoa pesa. Bunge lake limepuuzwa.
 
Spika wa bunge mh Job Ndugai leo wakati wa kuahirisha shughuli za Bunge, amewahoji mawaziri ni kwa nini kwa sasa wameamua kufanyia makongamano, warsha na semina nyingi Dar es Salaam na kuacha kufanyia Dodoma ambayo ni makao makuu ya nchi.

Ndugai ametaka kujua ni nani anayecontrol expanditure za serikali kwa sasa kwani kila mawaziri wanapofanya hizo safari za Dar wanalipana posho za kutisha pamoja na wasaidizi wao huku wakiwaacha wananchi masikini wakiwa hoi hoe hae bila huduma muhimu za jamii.

View attachment 1932327
Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo,
 
Back
Top Bottom