Spika Ndugai alikuwa na hoja ya msingi, tatizo sio kukopa bali kukopa wakati kuna tozo za miamala ambazo mlidai zanajenga madarasa na vituo vya afya

Nyankurungu2020

JF-Expert Member
Joined
Oct 2, 2020
Posts
4,170
Reaction score
6,757
Bunge la JMT lilipitisha tozo ambazo ama kwa hakika zilizua tafrani na kuzua kilio kwa wananchi, bila hata aibu Mwigulu Nchemba akainuka na kudai kuwa ambae hataki kulipa tozo basi ahamie Burundi.

Sasa kama mlipitisha tozo na mkadai kuwa zinajenga, shule, madarasa, zahanati na vituo vya afya mkopo wa tril 1.3 ajili ya madarasa wa nini?

Hizi tozo mnazokamua wananchi zinatumika kama kwa nini maana mlisema zitajenga madarasa na vituo vya afya.

Ndugai alimchukia sana Prof Assad alioelezwa kuwa bunge lake ni dhaifu, lakini ukweli ni kuwa ni dhaifu, halima meno kuikabaka serikali kwa makosa inayofanya.

Whether kuna watu wa Ccm wanataka kiti cha urais 2025 au hapana lakini ukweli ni kuwa kuna tozo zinaumiza wananchi ili hali kuna mkopo umejenga madarasa.

Sasa mama Samia mbona hazungumzii kama tozo basi au la?

"Kuna sintofahamu kwamba fedha za tozo zinaenda wapi na za mkopo zinaenda wapi?

Tozo tulizopokea Bil 7 tumekwenda kukamilisha ujenzi wa maboma ya madarasa 560 ili kuwaunga mkono maeneo ambayo wametumia nguvu kazi yao kujenga, yapo zaidi ya 10,000 kwahiyo hata hii fedha ni ndogo" - Mama Samia
 
Hivyo mtoa mada ni kwamba tozo zimejenga vyumba vya madarasa 560 pekee wakati uhitaji ni madarasa 10,000.

Hivyo mkopo umeweza kuharakisha utekelezaji na kuziba gap kwa wakati mfupi.

NB ; Mkopo wa uviko-19 hauna riba kwa miaka 20.
 
Kwa matiki hii unakubali kuwa zifutwe na serikali itumie mkopo kuliko kuumiza wananchi. Hakuna anayepinga kukopa bali kwa nini ukope huku unatoza tozo ambazo hazina manufaa?
 
Naamini ndugai alikuwa sahihi sana,sema amekuwa pia mwoga wa kusimamia hoja yake yenye mashiko.kashauli kama nchi tuone tunaijengaje nchi yetu bila kuendelea na mikopo kwa kila mradi unaotakiwa kufanyika.mawaziri walitakiwa wawe wabunifu kujua wapi,na vyanzo vipi vinaweza kuleta mapato bila kuumiza wananchi wa hali ya chini.
Mawaziri wengi ubongo wao umejengeka kwenye kutoza kodi tu
 
Halafu unalipaje hiyo mikopo ya hiyo miradi na madarasa kama hakuna makusanyo na tozo?
 
Mapendekezo? Huwa wanapita humu embo toa mapendekezo zaidi ya hayo yaliyopo?
 
Halafu unalipaje hiyo mikopo ya hiyo miradi na madarasa kama hakuna makusanyo na tozo?
Sababu ya kuweka tozo ilikuwa ni kujenga madarasa na vituo vya afya.
Unaenda kukopa kufanya vitu vile vile.
Kwanini wasifute baada ya mkopo?
Na simama na Ndugai katika hili japo alitusaliti kwenye bwagamoyo port
sisi Sukuma gang.
 
Kwa matiki hii unakubali kuwa zifutwe na serikali itumie mkopo kuliko kuumiza wananchi. Hakuna anayepinga kukopa bali kwa nini ukope huku unatoza tozo ambazo hazina manufaa?
Zifutwe Tena? Mahitaji ya madarasa elfu 10 ni mahitaji ya leo, baada ya miaka kadhaa mahitaji yataongezeka Kama ambavyo idadi ya watu inaongezeka. Unataka tukakope tena wakati huo ukifika? Jitahidi uelewe suluhisho la muda mfupi na muda mrefu kwa manufaa ya taifa
 
Kwani vyanzo pekee vya mapato ya serikali ni tozo za miamala? Huko nyuma madeni yalilipwa vipi?
Mahitaji yanaongezeka, idadi ya watu inaongezeka ambao hawawezi kulipa tozo au kodi kubwa sababu ni wanyonge, vijiji vinaongezeka na maendeleo yanatakiwa yafike vijijini watu wasijazane dsm.

Embu leta mapendekezo wanasiasa wanapita humu kama yanafaa yatafanyiwa kazi.
 
Acha unafiki wewe kiroboto! Wakati marehemu pombe anakopa zaidi ya Trilion 29 kwanini hukusema chochote zaidi ya kusifia?
 
Kwa matiki hii unakubali kuwa zifutwe na serikali itumie mkopo kuliko kuumiza wananchi. Hakuna anayepinga kukopa bali kwa nini ukope huku unatoza tozo ambazo hazina manufaa?
Mkuu Rais kasema tozo zinatekeleza ila kwa kazi ndogo sana.

Kumbuka January 17 shule zinafunguliwa na ktk demand ya madarasa 10,000 tozo imejenga madarasa 560 pekee hivyo kulikua bado na uhitaji wa madarasa 9440 .

Isitoshe mkopo aliokopa hauna riba kwa miaka 20.
 
Mahitaji yanaongezeka, idadi ya watu inaongezeka ambao hawawezi kulipa tozo au kodi kubwa sababu ni wanyonge, vijiji vinaongezeka na maendeleo yanatakiwa yafike vijijini watu wasijazane dsm.

Embu leta mapendekezo wanasiasa wanapita humu kama yanafaa yatafanyiwa kazi.
Achaneni na akili mfu kama hizo.

Hivi kwa rasilimali na utajiri wa taifa letu ni wa kwenda kuminya tozo kweny miamala?

Mtu wa kawaida ukizidisha matumizi unafiliska Mwanasiasa akizidisha matumizi anaongeza kodi.

Aweke sera nzuri za biashara watu wengi walipe kodi.
 
Back
Top Bottom