msovero
JF-Expert Member
- Jun 30, 2019
- 863
- 1,534
Ikiwa ni wiki chache zimepita tangu serikali iweke marufuku ya wanafunzi kusoma wakati wa likizo ili wapate muda wa kupumzika na kujifunza stadi mbali mbali za maisha wakiwa nyumbani, spika Job Ndugai amepinga vikali zuio hilo akidai kuwa linachelewesha maendeleo.
Spika Ndugai amesema wananchi wa kongwa walikuwa wamejipanga wanafunzi kusoma wakati wa likizo huku wakiwa tayari kujitolea kwa chakula pamoja na motisha kwa walimu ambao wangejitolea kufundisha wanafunzi hao na hivyo amedai kwamba kitendo cha serikali kuweka zuio ni kuchelewesha maendeleo kwani wanafunzi wanaosoma wakati wa likizo ni madarasa ya mitihani pekee.
Katika hatua nyingine, spika Ndugai amedai kuwa watu wanamdharau kwakuwa yeye ni 'mgogo' huku akiwashukia vikali vijana wenye digrii kuwa ndio wanaoongoza kwa kumtukana mitandaoni.