Spika Ndugai asema Tume ya Taifa ya Uchaguzi na Mahakama pekee wanaweza kumuambia kuwaondoa Bungeni Wabunge 19 wa Viti Maalum CHADEMA

Spika Ndugai asema Tume ya Taifa ya Uchaguzi na Mahakama pekee wanaweza kumuambia kuwaondoa Bungeni Wabunge 19 wa Viti Maalum CHADEMA

Spika anachagua vifungu vya kufuata.Huyu spika angekuwa nchi za wenzetu angeshafukuziliwa mbali
 
Kwanza; Kwa upande mmoja yuko sahihi kuwa yeye hahusiki na uteuzi wa wabunge, yeye kazi yake ni moja tu, kuwa, ni kujiridhisha kuwa wanaokuja na kuingia ktk chombo hicho cha kutunga sheria (anachokiongoza yeye) ni wabunge halali waliokidhi vigezo vya kisheria na kikatiba waliopita katika michakato halali kwa mujibu wa sheria na katiba ya nchi yetu...

Kwa hili amesema mwenyewe kwa kinywa chake kuwa amejiridhisha na kuona kuwa hao ni wabunge halali. Hilo ni jema na ni kweli kabisa na binafsi nakubaliana naye...

Ni kweli hawezi kuanza kuhoji uhalali wa kila mbunge hata pale anapokuwa ana cheti cha utambulisho toka Time ya Uchaguzi - NEC...

Pili; Amesema, baada ya hatua hizo jukumu lake jingine ni kuwapokea, kuwatambua na kisha kuwaapisha rasmi ili waanze majukumu yao...

Mpaka hapo sina hakika kama kuna tatizo na kuwa kuna mtu hakubaliani na hayo kwa sbb ni kweli hajavunja wala kukiuka sheria yoyote wala katiba ya nchi yetu...

Hata hivyo; Nadhani binafsi tatizo liko hapa. Kwamba, Spika Ndugai anadhani watu wote ni wajinga. Kwa sababu ya ulevi wa madaraka tu anashindwa kujua kuwa watu tunafahamu na pengine kuelewa zaidi kuliko yeye anavyoelewa. Anasahau kuwa sheria ni msumeno na inakata pande zote..

Kwamba, kama ambavyo katika hatua zote hizo nilizoeleza hapo juu amefuata utaratibu, sheria na katiba inavyotaka (kama anavyodai), basi anapaswa kutenda hivyo hivyo kwa kina mama hawa 19 baada ya chama chao (CHADEMA) kutowatambua (kwa sababu ya ishu zilizo ndani ya chama chao)...

Wao CHADEMA wanadai utaratibu wa uteuzi wao ndani ya chama ili kuupata ubunge huo haukufuatwa na kwa sababu hiyo kimewafutia uanachama wao...

Wametendewa haki ama hawakutendewa haki na chama chao? Hili siyo jukumu la Spika Ndugai kulijua. Anapaswa kufanya wajibu wake kwa nyaraka halali na rasmi. Kama Chadema, wameshamtaarifu rasmi basi, hana choice ila kuwaelekeza hao kinamama yawapasayo kufanya...!

Aidha, wote tunaelewa kuwa, kwa mujibu wa sheria mama (katiba) ya nchi yetu, mtu hawezi kuwa mbunge iwapo hana udhamini wa chama halali cha siasa chenye usajili wa kudumu...!!

Sasa basi; Taratibu, sheria na katiba hiyohiyo iliyompa mamlaka ta kuwatambua na kisha kuwaapisha kabla ya hili la pili kuibuka, ndiyo taratibu na sheria na katiba hiyo hiyo tena imewaondolea sifa ya ubunge wao...

Sasa Spika Ndugai atuambie anaona shida gani kuliweka hilo wazi ili watu wamuelewe badala ya kupiga siasa ambazo hazina manufaa yoyote kwake na kwa nchi..?

Binafsi namshauri Spika Ndugai aheshimu taratibu, sheria na katiba ya nchi yetu....

Tunatambua na kujua kuwa wabunge hawa CCM na serikali yao inawahitaji sana kwa manufaa ya kisiasa...

Na amesema vizuri sana kwamba chombo pekee kilichobaki cha kurudisha sifa ya ubunge wa hawa kinamama 19 waliokuwa wanachama wa CHADEMA infact siyo Tume ya Uchaguzi bali ni mahakama pekee unless chama cha hawa kinamama kilichowafutia uanachama wao kibadili maamuzi yake...

There's no way around ku - bypass sheria na katiba ya nchi. Tutajizungusha weee lakini ukweli ni huu..

Na hapa siyo ishu ya kuwa hawa ni wanawake ndiyo maana wanatendewa hivi. Hapana, hii siyo kweli hata kidogo bali Taratibu na katiba yetu zinataka iwe hivyo..!!

Spika Ndugai huu ni ushauri wa bure kabisa; Jitenge na hili. Wewe ni kiongozi wa muhimili muhimu sana. Waache hawa kinamama warudi na kupatana na chama chao. Ama wakiona hawatendewi haki, waende mahakamani labda watapata haki yao huko...!!
Fact Sana mkuu.
 
View attachment 1645026
Kwa kumbukumbu tu...
Njia moja ni tume ya uchaguzi kuniandikia na kusema hawa wanastahili kuwa wabunge, mheshimiwa Spika waapishe na huo ndio utaratibu na utaratibu huo ulifuatwa nikawaapisha.

Upande wa pili ni kwamba majina ya wanaoapishwa hapa kwa njia hiyo huwa yanakuwa yamepita kwa kutangazwa kwenye gazeti la serikali. Gazeti la serikali lilikwisha watangaza kwa kuwaorodhesha kwa majina mmoja mmoja katika hao 19, kwakua hayo yametekelezwa ipasavyo na spika nae kawaapisha alafu mtu mwingine anasema kosa la hao ni wewe kuwaita na kuwaapisha kwa hiyo wafukuze, hivi na mimi si nitaingie kwenye Guiness book spika wa ajabu kabisa ambae hajawahi kutokea dunia kuwafukuza wabunge kwa kosa la kuwaapisha.

Kwa kweli tunaongozwa na vichaa kama wanavyodai wao wenyewe...

Huu ni ushahidii tosha kuwa nchi inaongozwa na watu wasiokuwa na uwezo na busara ya kuwa viongozi wa Taifa letu. Jiwe na Ndugai wake are just PRETENDERS!!!!!
 
Back
Top Bottom