Spika Ndugai ataka Walimu waongezewe kazi wafundishe masomo kuanzia matatu ili kupunguza uhaba wa Walimu

Spika Ndugai ataka Walimu waongezewe kazi wafundishe masomo kuanzia matatu ili kupunguza uhaba wa Walimu

USSR

JF-Expert Member
Joined
Jul 15, 2015
Posts
10,904
Reaction score
26,184
Akikazia mawazo ya wabunge kama kawaida yake nimemsikia Spika ameitaka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kuwaongezea masomo ya kufundisha walimu kwa maana ya kuwafundisha kuyafundisha tangu wakiwa vyuoni hasa vyuo vikuu ili kupunguza uhaba wa walimu na kuongeza tija kwa Wanafunzi.

Akitolea mfano wa Balozi Mbelwa Kairuki alichomsimulia kule China mwaka jana, Ndugai amesema kuwa kule China vijana wanajua mambo mengi sio kama hapa Tanzania ambapo kijana anajua kazi moja tu kama ni fundi ujenzi ni ujenzi tu na kama ni kuchomelea ni kuchomelea tu.

"Kwanini mwalimu wa high school nafundisha somo moja" eti mmesomea kufundisha somo moja tu ili iweje na uhaba huu wa walimu alihoji speaker Ndugai.

Anatakiwa afundishe masomo matatu, manne au hata kuendelea hali iliyoibua hoja ya mkwamo wa walimu wanaongojea kazi Serikali na kujiuliza watakwenda wapi? Kama wazo la Spika litafanyiwa kazi.
 
Wagogo wanaomba kujengewa maghorofa makubwa makubwa Dodoma!

Yaani kila kitu wanaomba hawajuwagi kujiongeza.

Taratibu wanaondolewa mjini kisayansi watabakia pembezoni tu Kibaigwa, Bahi na Mtera.

Warangi nawakubali sana akina Kimbisa ni watu wa kujiongeza sana!
 
Kuna Uhaba ?, Mbona Waalimu wapo Kitaa ?, Au ndio kuongeza kazi kwa ujira ule ule..., Yaani ni mwendo wa kunyonya watu....

Kwanini wasiwaongezee wabunge kazi wakiwa off waende pia kufanya profession zao ?, hapo kuna madaktari, waalimu, wapiga ramli..., na nadhani hakuna mtu hapo hawezi kufagia, kusafisha vyoo na hata kunyoa nywele na kubrashi viatu tunaweza kuwafundisha..., Pia wanaweza kuanzisha shamba la bunge wapeane zamu kila mwezi waende kupiga jembe...
 
Kuna Uhaba ?, Mbona Waalimu wapo Kitaa ?, Au ndio kuongeza kazi kwa ujira ule ule..., Yaani ni mwendo wa kunyonya watu....

Kwanini wasiwaongezee wabunge kazi wakiwa off waende pia kufanya profession zao ?, hapo kuna madaktari, madokta na nadhani hakuna mtu hapo hawezi kufagia, kusafisha vyoo na hata kunyoa nywele na kubrashi viatu tunaweza kuwafundisha..., Pia wanaweza kuanzisha shamba la bunge wapeane zamu kila mwezi waende kupiga jembe...
Wakoloni walikuwa wakandamizaji saiz hadi sisi kwa sisi tunakandamizana mwanawane. Hukumsikia mkubwa wake alivyoropoka kule tabora???
Ndege wenye manyoya sawa huruka pa1 mkuu.
 
Hayo masomo matatu hadi matano ya kufundishwa na mtu mmoja ni masomo gani hayo?

Yani kwa mfano mwl afundishe masomo yafuatayo:

Physics
Geography
Chemistry
Biology
Kiswahili

[emoji849][emoji849][emoji849][emoji849]

Ndugai BURE kabisa.
 
Uhaba wa walimu hautatuliwi kwa kuongezea walimu masomo huko ni kuwatisha mzigo juu ya mzigo matokeo yake ni kudorola kwa elimu nchini.

Uhaba wa walimu unatatuliwa na kuajiri walimu wengine wapya, lakini ukweli huu hawataki kuusema kwa kuwa wako kutumikia matumbo yao.
 
Back
Top Bottom