Spika Ndugai ataka Walimu waongezewe kazi wafundishe masomo kuanzia matatu ili kupunguza uhaba wa Walimu

Spika Ndugai ataka Walimu waongezewe kazi wafundishe masomo kuanzia matatu ili kupunguza uhaba wa Walimu

Wala hautakiwi kuumiza kichwa. Unaburuza tu bora liende. Watajijua wenyewe. Wanafikiri kufundisha ni kazi nyepesi.
Fikiria unaambiwa ufundishe Physics, Chemistry, Biology na Mathematics A-level.
Mziki wake unauonaje?
 
Hayo masomo matatu hadi matano ya kufundishwa na mtu mmoja ni masomo gani hayo?

Yani kwa mfano mwl afundishe masomo yafuatayo:

Physics
Geography
Chemistry
Biology
Kiswahili

[emoji849][emoji849][emoji849][emoji849]

Ndugai BURE kabisa.
Kuna kusahihisha madftari ya watoto, na madarasa ndio yamejazwa watoto 100 - 400 kwa darasa.
DHAIFU wa AKILI na kinga za mwili anavimbiwa kodi zetu anajiona mzima na timamu. Bure kabisa.
 
Hayo masomo matatu hadi matano ya kufundishwa na mtu mmoja ni masomo gani hayo?

Yani kwa mfano mwl afundishe masomo yafuatayo:

Physics
Geography
Chemistry
Biology
Kiswahili

[emoji849][emoji849][emoji849][emoji849]

Ndugai BURE kabisa.
Hii nchi inatawaliwa na viongozi wenye uwezo mdogo wa kufikiri kiasi cha kushangaza wameingiaje madarakani! Kila siku wanatoa matamko yaliyojaa mkanganganyiko mpaka inashangaza.
 
Speaker
Ndiyo Ukweli Wenyewe
Nasema Uongo Ndugu Zangu
Ccm Hoyee!😂😁
 
Akikazia mawazo ya wabunge kama kawaida yake nimemsikia Mh Speaker ameitaka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kuwaongezea masomo ya kufundisha walimu kwa maana ya kuwafundisha kuyafundisha tangu wakiwa vyuoni hasa vyuo vikuu ili kupunguza uhaba wa walimu na kuongeza tija kwa wanafunzi.

Akitolea mfano wa Balozi Mbelwa Kairuki alichomsimulia kule China mwaka jana, Ndugai amesema kuwa kule China vijana wanajua mambo mengi sio kama hapa Tanzania ambapo kijana anajua kazi moja tu kama ni fundi ujenzi ni ujenzi tu na kama ni kuchomelea ni kuchomelea tu.

"Kwanini mwalimu wa high school nafundisha somo moja" eti mmesomea kufundisha somo moja tu ili iweje na uhaba huu wa walimu alihoji speaker Ndugai.

Anatakiwa afundishe masomo matatu, manne au hata kuendelea .hali iliyoibua hoja ya mkwamo wa walimu wanaongojea kazi serkalini na kujiuliza watakwenda wapi? Kama wazo la speaker litafanyiwa kazi.
Hilo somo moja wanafunzi wangapi? Tuanzie hapo.
Tatizo sio idadi ya ya masomo anayofundisha mwalimu bali uwiano wa wanafunzi na walimu.
Shule za msingi mwalimu anaweza kufundisha karibu masomo yote na hii haijaweza kutatua tatizo la walimu
 
Mfano mimi mwalimu, nafundisha somo X kidoto Y wanafunzi 400 na kidato S wanafunzi 350. Jumla ni wanafunzi 750 nikiongezewa somo moja kwa vidato vilevile jumla itakuwa 1500. Nikitoa kazi, zoezi au jaribio itabidi nisahihishe wanafunzi 1500.
Huku ni kufikiri au kubashiri

Shida ya watu wa CCM huwa wanajiona wazalendo na wana uwezo mkubwa wa kufikiri kuliko watu wengine wote.
 
Hivi huyu mtu ana elimu gani(amesomea nini??) ningependa kujua maana katika empty set ninazozijua huyu ni wa kwanza yaan katika sector ya poor reasoning nampa cheo cha brigedia general
 
Wakiongezewa masomo ya kufundisha pia waongezewe mishahara,anayepokea 800,000 akiongezewa masomo mawili alipwe 2,400,000 kila somo na mshahara wake,kama wao wanavyopata posho kila kikao
 
Huyu spika ni boya tu.
Huwezi kuongeza tija kwa mwanafunzi kwa kumuongezea mzigo wa masomo mwalimu.Halafu masomo matano chuo kikuu mtu atayasomaje? Lazima mwalimu afundishwe partially sana.
 
Back
Top Bottom