Spika Ndugai ataka Walimu waongezewe kazi wafundishe masomo kuanzia matatu ili kupunguza uhaba wa Walimu

Nashukuru Nina uvumilivu wa kusoma kitu mpaka mwisho. Tofauti na hapo ningekutukana. Nisamehe maana nilianza kukutafutia laana ya kukupa.
 
Akili kichwani mwako na future ya mtoto wako. Mwalimu hata ukimpa masomo 13 atafundisha hadi bible ila matokeo yake sasa...
Wao hawana shida na hilo kwasababu hata matokeo siku hizi wanapika kama wali.
 
Kama vipi hayo masomo matano amrundikie yule mwalimu wa kemia na hesabu, maana yeye anajua mambo kibao ikiwemo namna hukumu zinavyotakiwa kuandikwa na majaji...
 
Hakuna cha walimu wa kujitolea, serikali iajiri walimu fullstop... Tunalipa kodi ili zilete hizo huduma za jamii, moja ya huduma za jamii ni elimu, elimu sio kuwa na madarasa na madawati, uwepo wa vitendea kazi na walimu Pia ni muhimu mno.... Watumie kodi zetu kuajiri walimu, sio kununua midege inayoleta hasara tu.
Nafikili kila shule ipate walim wa kujitolea sie mazazi tuwachangie ili kupata ufanisi mzuri , kuliko kulazimisha kuongeza , masomo
 
Na nyie ndio ambao mmepitisha utawala huu wa hovyohovyo
 
For the third time nakubaliana na wewe ...Kuna saa MATAGA wewe unanyoosha maelezo
 
Nawakumbusha tu kwamba spika Ndugai alitumia zaidi ya $10 million kwa matibabu India.
 
Labda sijamwelewa vizuri. Hivi anamaanisha hata kupunguza uhaba wa madaktari. Daktari moja atibu sikio, jicho, figo, ini siyo?
Sasa maswali hayo sijui anamwuliza nani,maana yeye yupo huko bungeni zinakotungwa na kurekebisha Sheria zaidi ya miaka 20 hakulitambua hilo.

Kutokana na Mazingira ya kada ya ualimu iilivyo hakuna mzazi eti mwanae kafaulu PCM, PCB, PGM atameleka ualimu.
 
Bora mbunge mmoja angewakilisha majimbo hata 30.

Ili fedha itumike kuwapa akira walimu wengine.

Walimu wanaumuhimu katika kuendelea nchi kuliko Hawa wabunge
 
Baada ya walimu kukamilisha zoezi la usimamizi wa uchaguzi kwa ufanisi Sana hatimae Ndugai amewalipa walimu stahiki zao kea kuwataka waongezewe masomo ya kufundisha.

Hongera mh Nddugai.
 
Ngazi ya shule ya msingi mwalimu anaweza akafundisha masomo kadhaa. Lakini kuanzia sekondari una-speacialise somo moja tu. Mengine utababaisha tu. Kwa mfano mwalimu wa Fizikia anaweza kushikilia nafasi ya mwalimu wa Hisabati wakati kuna dharura.

Lakini topics nyingi hawezi kuzimudu kwa kiwango anachozimudu mwalimu wa Hisabati. La sivyo tutakuwa tunawadanganya wanafunzi kwamba wamesoma Hisabati wakati wamebabaisha tu. Nasema haya kutokana na uzoefu wangu wa kufundisha wa miaka 35.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…