Spika Ndugai atangaza kutambua Ubunge wa Cecil Mwambe aliyejiuzulu Ubunge na uanachama CHADEMA

Spika Ndugai atangaza kutambua Ubunge wa Cecil Mwambe aliyejiuzulu Ubunge na uanachama CHADEMA

Kuna mambo mengine wakubwa wanayofanya wanadhani watanzania wamefungwa akili.
Ila historia itawahukumu wengi.

Niishie hapo
 
Pia ni vema kujua mke wa ndugai na watoto wake wanaishi wapi kwa maslahi mapana ya taifa.
 
Ndugai amelifanya bunge kuwa kituko cha moja ya bunge la jabu kabisa duniani! acha tuendelee kudharaulliwa tu duniani kutokana na viongozi wa ajabu kabisa kuwahi kutokea nchi hii!
 
Kuna vitu vingine huwezi kuamini kama vinafanywa kwa utashi au kutumia akili! Ndio maana bunge letu limekuwa dhaifu na mambo ya kiswahili haikuwahi kutokea tangu tupate uhuru na sidhani kama itakaa itokee tena kwa spika mwingine!
 
Ukiendesha shuguli zako za kisiasa na kutengeneza mazingira ya maamuzi kifitna , lazima ujue wale watakao kujibu maamuzi yako watafanya kifitna.Kuna kujiuzuru na kutengenezewa mazingira ambayo unalazimika kujiuzuru. Elimu tosha kwa wapinzani.
 
Hii nchi ina maajabu sana, pamoja na mbunge tajwa hapo juu aliekuwa akiwakilisha jimbo la Ndanda kupitia CHADEMA kutangaza kujiuzulu ubunge na kujivua uanachama wa CHADEMA na kujiunga na CCM lakini bado anaendelea kupata stahiki zote kama mbunge na Ndugai bado anamtambua kuwa Cecil Mwambe ni mbunge wa Bunge la Jamhuri.

Kitendo cha Mwambe kuhamia CCM kilimpotezea sifa ya kuendelea kuwa mbunge, Hili la leo Spika wa Bunge amedhihirisha udhaifu alionao. Spika ni dhaifu na Bunge la 11 ni Bunge dhaifu mno katika historia ya Tanzania.

Ni dhaifu kabisa kwa namna anavyowaburuza! Sijui angekuwa imara ingekuwaje? Nadhani angewachuna ngozi kabisa.
 
Siasa za nchi hii ukifuatilia sana utaumia sana roho mkuu! Tafuta ugali wa kula na watoto wako tu!
Huu ni ushauri mbovu na wa hovyooo kabisa. Angalau piga kelele hapa mitandaoni na ID isiyojulikana, chambua mambo wengine wapate elimu na uelewa. Ipo siku watanzania wataamka na kudai haki zao. Kuna mengi Magufuli kayafanyia kazi kutokana na kelele hizi hizi, pamoja na kiburi na ubabe wake
 
Halafu kuna watu bado wanaamini CCM itatoka madarakani kwenye sanduku la kura
 
Hivi spika ndugai hajui kama anajiaibisha mwenyewe yeye na waziri wa sheria pamoja na serikali yote?hivi yeye anaona anawanyoosha wapinzani au aliekuwa mwenyekiti wake wa chama Mbowe?

Tunakoelekea kuna siku watalala huko huko mbungeni hii ganzi ya chuki inayopandikizwa kwa nguvu iko siku.
 
Ni kama usajili wa mkopo, anachezea timu nyingine analipwa na timu nyingine.
 
Hivi spika ndugai hajui kama anajiaibisha mwenyewe yeye na waziri wa sheria pamoja na serikali yote?hivi yeye anaona anawanyoosha wapinzani au aliekuwa mwenyekiti wake wa chama mbowe?
Tunakoelekea kuna siku watalala huko huko mbungeni hii ganzi ya chuki inayopandikizwa kwa nguvu iko siku.
BBC hawana vipindi vya saa 7 mchana, hiyo DW-Ujerumani!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cdm waliiba sana kura hayo ndo matokeo yake. Kitu kinaondoka jinsi kilivyokuja
 
Back
Top Bottom