Spika Ndugai atangaza kutambua Ubunge wa Cecil Mwambe aliyejiuzulu Ubunge na uanachama CHADEMA

Spika Ndugai atangaza kutambua Ubunge wa Cecil Mwambe aliyejiuzulu Ubunge na uanachama CHADEMA

Chadema mmeambiwa hamjatimiza vigezo vya kumuondoa jamaa,hivyo mpaka hapo maamuzi ya Spika ni sahihi.

Mihemko imezidi, inshangaza sana mnavyojitanabaisha kuwahuko kumejaa vichwa kumbe ugoro mtupu.
FB_IMG_1588805454050.jpg
 
Hapa ndo nimeelewa mabeberu huwa wanamaanisha nini wakisema "WE GOT YOUR BACK SON". And they got his back for real!
 
Kama bunge lake job ndugai sio dhaifu basi amtambue Joshua nassari nae ni mbunge pia kupitia utaratibu wake huo vinginevyo naye pia ni dhaifu ila sisi walipa Kodi ndio wajinga wa kutupwa tuendelee kulipa kodi hakuna shida
 
Atawajibishwa na nani na kwa sheria ipi?
Uhujumu uchumi
Unampaje mshahara na posho mtu asiyestahili
Unamuingizaje bungeni mtu asiyestahili kuwa sehemu ya bunge..
Huyu mbilikimo ndugai ana laana huyu
Soon ataokota makopo
 
Ha ha ha ha ha ha ha ha ha wacheni nicheke, maajabu hayaishi hapa bongo.

Taa za mkono wa chuma zimewashwa rasmi.

Mwenye macho haambiwi tazama, ni maandalizi kabambe, pia kuwaonesha Wabunge wengine wa CHADEMA kuwa waende wasiogope hakuna kinachoshindikana.

Kuna uwezekano kuwa wanapima upepo endapo ata declare kuongoza maisha itakuwaje.

Dahh ha ha ha ha ha, kuna shida kubwa sana kwenye hii ardhi.
 
..Je, Cecil Mwambe anautaka ubunge wa aina hii?

..ccm inafanya mambo ya hovyo, lakini sidhani kama wanaweza kushiriki kulinajisi bunge kama anavyotaka kufanya Spika Ndugai.
 
..Je, Cecil Mwambe anautaka ubunge wa aina hii?

..ccm inafanya mambo ya hovyo, lakini sidhani kama wanaweza kushiriki kulinajisi bunge kama anavyotaka kufanya Spika Ndugai.
CCM wenzako wanaona sawa muulize bashiru na elimu yake Kama atapingana na ndgy
 
Anamuiga jiwe. Walianza kunajisi chaguzi za marudio watu wakakaa kimya, wakanajisi uchaguzi SM bado watu wako kimya. Katika mazingira hayo sioni wakiacha kufanya lolote watakalo.
Nchi ya wapumbavu hii na wanajua wanaweza fanya lolote kwa yeyote na wakati wowote sanasana ukiwapinga unapotezwa kivyovyote...!

Chuki wanayoijenga sijui..... Mungu tupe uvumilivu.
 
Cecil Mwambe alijiondoa Chadema kwenda CCM hivyo sio Mbunge halali kwa Mujibu wa Ibara ya 71(1)(e) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


IMG_20200507_235229.png
 
CCM wenzako wanaona sawa muulize bashiru na elimu yake Kama atapingana na ndgy

..Dah!!

..katika MATUSI mabaya unayoweza kunitukana ni hili la kuniita mwana-CCM.

..hivi nimekukosea nini mpaka uniite mwana-CCM?
 
Hivi bado munaendelea kumshangaa Nini, endeleeni na ujenzi wa taifa. Bunge la CCM liko vizuri tu nadhani Kila mmoja anaona maendeleo mlangoni kwake

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwani sheria inasemaje?
Spika hawezi kuchukua hatua mpaka tume ya uchaguzi iwe imemtaarifu kwamba jimbo fulani liko wazi kutokana na sababu tajwa.

Je, Kuna mtu ana ushahidi kwamba spika kesha taarifiwa na Tume?
kisheria hiyo ndiyo point
 
Back
Top Bottom