LIMBOMAMBOMA
JF-Expert Member
- Oct 3, 2017
- 11,788
- 15,406
Hivi mwambe kuhama chama ilikuwa Ni siri?Shida barua ya Mnyika ndo ina mapungufu...!ivi CDM hakuna wasomi wabobezi kama alivyokuwa Slaa na Mashinji? Maana vile viatu vishakua oversize
Hivi mwambe kuhama chama ilikuwa Ni siri?Shida barua ya Mnyika ndo ina mapungufu...!ivi CDM hakuna wasomi wabobezi kama alivyokuwa Slaa na Mashinji? Maana vile viatu vishakua oversize
Ni spika mbovu kuwah kutokea akiendesha bunge Kwa chuk na kukomoa watu
Its not over until its over...[emoji769]
Hoja ya ndugai Ni pumbaSpeaker kafafanua kwamba barua aliyopokea toka kwa Katibu Mkuu wa CHADEMA ina mapungufu ya kisheria, kwa hiyo 'haina maana'. Nadhani ujumbe wake hapa ni kwamba CHADEMA kikimulikwa vizuri kina mapungufu mengi ya kiuongozi. Kama katibu mkuu wa chama ameshindwa kugundua kwamba barua yake haikidhi 'vigezo' kisheria huo ni upungufu mkubwa.
Wanajua hakuna wa kuwauliza ila siku watu wakipandisha mashetan itakua balaa maana uoga una mwishoAnamuiga jiwe. Walianza kunajisi chaguzi za marudio watu wakakaa kimya, wakanajisi uchaguzi SM bado watu wako kimya. Katika mazingira hayo sioni wakiacha kufanya lolote watakalo.
Wakuteuliwa na ndu gayIbara ya 66 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania ieainisha wabunge.
http://juakatibatanzania.com/assets/images/katiba.pdf
66.-(1) Bila ya kuathiri masharti mengine ya ibara hii, kutakuwa na aina zifuatazo za Wabunge, yaani-
(a) Wabunge waliochaguliwa kuwakilisha majimbo ya uchaguzi;
(b) Wabunge wanawake wa idadi inayoongezeka, kuanzia asilimia ishirini ya Wabunge waliotajwa katika aya ya (a), (c ) na (d), itakayotajwa mara kwa mara na Tume ya Uchaguzi kwa taarifa iliyochapishwa katika Gazeti la Serikali baada ya kupata kibali cha Rais, watakaochaguliwa na vyama vya siasa vinavyowakilishwa Bungeni, kwa mujibu wa ibara ya 78, na kwa kuzingatia masharti ya uwiano wa uwakilishi baina ya vyama hivyo;
(c) Wabunge watano waliochaguliwa na Baraza la Wawakilishi kutoka miongoni mwa wajumbe wake;
(d) Mwanasheria Mkuu;
(e) Wabunge wasiozidi kumi walioteuliwa na Rais kutoka miongoni mwa watu wenye sifa kwa mujibu wa ibara ya 67, isipokuwa sifa iliyotajwa katika ibara ya 67(1)(b).
Sasa huyu mbunge aliyejiuzulu uanachama wa chama kilichopmpa tiketi ya kugombea ubunge, akapigiwa kura kwa sera za chama hicho, alipojiuzulu uanachama, automatically alijiuzulu na ubunge.
Sasa hivi amekuwa mbunge wa aina gani kati ya hizo hapo juu?
Maanaubunge wa kuchaguliwa na wananchi ameshajiuzulu, si mmoja wa wabunge wa viti maalum vya wanawake, si mbunge wa baraza la wawakilishi, si mwanasheria mkuu, si mbunge wa kuteuliwa na rais.
Ni mbunge wa aina gani huyu Frankenstein?
We nae! Kuna kujiuzuru ubunge na kuna kujivua uanachama, mtu anaweza kujiuzuru ubunge na akaendelea kuwa mwanachama Kama alivyofanya Rostam Aziz, hivyo basi kile tu kitendo cha mwambe cha kujiuzuru ubunge tena kwa kupitia spika tayari ubunge wake ulikoma, yaani hata asingejivua uanachama na kuendelea kubaki chadema lakin tayari kashajivua ubunge. Suala barua kutoka chamani ni kwa wale wabunge wanaofuzwa au kujivua uanachama bila kujiuzuru ubunge, Sasa huyu mwambe alijiuzuru ubunge Kama Rostam ingawa Rostam hakujivua uanachama.Inawezekana chama husika lazima kimwandikie Spika kukoma kwa uanachama wa mbunge husika (wanaojua hili wanaweza kutuambia) ndiyo maana pia nimehoji utaratibu wa mtu kuhama chama mara baada ya bunge kuisha umetokea wapi?
Tumia akili kwa mfano mwambe wewe Tume inajuaje kama jimbo fulani liko wazi? Mbunge akijiuzulu ,spika anaanza kujua kisha anaiandikia barua tume tume inatangaza uchaguziKwani sheria inasemaje?
Spika hawezi kuchukua hatua mpaka tume ya uchaguzi iwe imemtaarifu kwamba jimbo fulani liko wazi kutokana na sababu tajwa.
Je, Kuna mtu ana ushahidi kwamba spika kesha taarifiwa na Tume?
Acha tu ndio maana ni mbabembabe sn na yuko mstali wa mbele kutetea serikali badala ya wananchi maana anajua ccm wanachoweza kumfanya km SittaEee bhana eeee !!
OkMwandishi amewaorodhesha wote hawa kutoka upinzani, ingekuwa vyema akaorodhesha wabunge kadhaa wa CCM waliohudumiwa tofauti mbali ya huyo spika.
Hii nchi ina maajabu sana, pamoja na mbunge tajwa hapo juu aliekuwa akiwakilisha jimbo la Ndanda kupitia CHADEMA kutangaza kujiuzulu ubunge na kujivua uanachama wa CHADEMA na kujiunga na CCM lakini bado anaendelea kupata stahiki zote kama mbunge na Ndugai bado anamtambua kuwa Cecil Mwambe ni mbunge wa Bunge la Jamhuri.
Kitendo cha Mwambe kuhamia CCM kilimpotezea sifa ya kuendelea kuwa mbunge, Hili la leo Spika wa Bunge amedhihirisha udhaifu alionao. Spika ni dhaifu na Bunge la 11 ni Bunge dhaifu mno katika historia ya Tanzania.