The Invincible
JF-Expert Member
- May 6, 2006
- 6,006
- 3,281
😁 😁Sa si umalizie tu kushikishwa nini, mnatutesa kufikiria.
😁 😁Sa si umalizie tu kushikishwa nini, mnatutesa kufikiria.
Jinai haipotei kuna siku hata 2026 mtu atafungua kesiRecords ,historia inaandikwa ili siku moja watu wawajibike kwa udhalimu wao.
Sent using Jamii Forums mobile app
Nyinyi wenye afya ya akili mbona mmefanya ya kijinga?Wahenga walishasema tangu kitambo kwamba kabla hujafa hujaumbika , hii maana yake ni kwamba binadamu anaweza kukumbwa na changamoto yoyote wakati wowote bila kujali madaraka aliyonayo .
Video hii hapa chini inamuonyesha Cecil Mwambe akijivua uanachama wa Chadema na kujiunga na ccm mbele ya Humphrey polepole ambaye ni kiongozi wa ccm , lakini kinachoshangaza ni kuona Ndugai kushindwa kuamini jambo hili as if yeye yuko chama tofauti na ccm !
Swali ni Je Spika wa bunge anayo afya njema ya akili , mbona anashindwa kung'amua mambo mepesi kiasi hiki ? Je kuna haja ya bunge hata kama limebakisha wiki chache kuendelea kuongozwa na mtu mwenye mapungufu kiasi hiki ?
Inawezekana kuna vitu viko ndani yake vinamsumbua na kumpa uchizHatuna uhakika pia kama ana akili timamu
Chadema wamepeleka barua ya kumvua uanachama,spika anataka waambatanishe barua ya mwambe ya kujiuzulu swali kama mwambe hakuandika barua chadema ya kuwaeleza kuwa amejiuzulu je chadema wanaipata wapi mpaka waambatanishe?Spika anasema hajapokea barua ya Mwambe, maana CDM walipaswa kuambatanisha barua ya Mwambe kuhamia chama kingine au la muhtasari wa kikao cha chama kilichomvua uanachama Mwambe.
Lasivyo kuna siku Mwambe Atakana na spika ataoneka alisikiliza maneno ya vijiweni yasiyo na document.
Sent using Jamii Forums mobile app
Kuna mambo mengine hayaitaji barua.yako wazi hebu tazama bhas hata hio video mkuuNyinyi wenye afya ya akili mbona mmefanya ya kijinga?
Suala dogo tu la kuambatanisha nakala za barua moja ya cecil mwambe kujitoa chadema na ya pili nakala ya barua rasmi ya kikao halali kilichomtoa au kumjadili na kuamua rasmi kutomtambua kama mwanachama wenu?
Mnarudia makosa yaleyale mliyoyafanya ya kutomtambua joseph selasini kama mnadhimu wa kambi rasmi ya upinzani bungeni kwa maandishi.
Chadema mnakwama wapi?
Sent using Jamii Forums mobile app
Labda sijaelewa. Huyu si alijivua uanachama hadharani na akajiunga na chama kingine? Kuna haja kweli ya kukaa kikao kumvua uanachama mtu aliyeishajivua mwenyewe? Kwa vile sio wa kwanza kutangaza kujivua uanachama basi itakuwa vyema kama atathibitisha kuwa aliamua kutangaza nafasi zao kuwa wazi baada ya kupokea barua na dondoo za kuwafukuza uanachama kutoka vyama vyao vya awali.Spika anasema hajapokea barua ya Mwambe, maana CDM walipaswa kuambatanisha barua ya Mwambe kuhamia chama kingine au la muhtasari wa kikao cha chama kilichomvua uanachama Mwambe.
Lasivyo kuna siku Mwambe Atakana na spika ataoneka alisikiliza maneno ya vijiweni yasiyo na document.
Sent using Jamii Forums mobile app
Eee bhana eeee !!Ndugai akuza deni la matibabu nje ya nchi. Adaiwa kulamba milioni 500 ndani ya miezi mitano
JOB Ndugai, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, na Rais John Magufuliwamenyoshewa kidole, wakihusishwa na ongezeko kubwa la deni la matibabu nje ya nchi.
Deni hilo limeongezeka kwa kasi isiyo ya kawaida katika kipindi ambacho watumishi wa serikali wanaotibiwa nje ya nchi wanadhibitiwa na rais, na Ndugai mwenyewe amekuwa “mgonjwa mkuu” aliyetibiwa nje katika kipindi hicho.
Mwaka jana, serikali ililiambia bunge kuwa nchi ilikuwa inadaiwa Sh 28.60 bilioni kwa ajili ya matibabu ya viongozi nje ya nchi, hasa India. Ndani ya miezi sita tu, deni hilo limekua hadi Sh. 45.73 bilioni. Hili ni ongezeko la Sh.17.13 bilioni.
Ongezeko la asilimia 60.71 ya deni ndani ya kipindi kifupi, wakati idadi ya viongozi wanaotibiwa nje imepungua, ni doa kwa dhamira ya Rais John Magufuli ya kupiga vita ufisadi na kudhibiti matibabu ya nje.
Kwa mujibu wa ripoti ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali (CAG), ongezeko hili ni la kati ya tarehe 30 Juni 2017 na tarehe 31 Desemba 2017.
Kwa kuwa limeongezeka katika kipindi ambacho wagonjwa wanaokwenda nje lazima waruhusiwe na rais, na “mgonjwa mkuu” aliyetibiwa nje ni Ndugai, ongezeko la deni la matibabu linahusu wote wawili – rais na spika.
Taarifa zinaonyesha kuwa sehemu kubwa ya deni hili imesababishwa na Job Ndugai. Kwa mujibu wa takwimu za CAG, Ndugai amekaa India kwa takriban miezi mitano, akiwa na wasaidizi wake na familia yake.
Posho ya mbunge anapokuwa nje ya nchi kwa siku moja ni dola 500; mtumishi wa bunge ni dola 450; mwenzi wa ndoa ni dola 300.
Kwa uchambuzi wa ripoti ya CAG, Ndugai amekaa India kwa miezi mitano, ambayo ni siku 150. Kama kwa siku moja alilipwa dola 500, ina maana kuwa kwa miezi mitano alilipwa dola 75,000. Kwa shilingi za Kitanzania, kwa viwango vya ubadilishaji fedha vya Sh. 2,170 kwa dola moja, Ndugai alitumia shilingi 162,750,000 kama posho ya kuishi India.
Akiwa India alikuwa na wasaidizi wawili – maana alihamishia ofisi yake huko huko hotelini. Kwa gharama ya dola 450 kwa siku, mara mbili, watumishi hawa walilipwa dola 900 kwa siku. Kwa siku 150 walizokaa India, maana yake walilipwa dola 135,000, sawa na Sh. 292,950,000.
Chanzo chetu kutoka Bungeni kimeliambia SAUTI KUBWA: “Kwa ujumla, matibabu ya Ndugai kwa miezi mitano yametumia posho za shilingi 455,700,000, na hapo bado gharama za hospitali huko India, na tiketi za ndege kwa watu wote hao, na bado gharama alizokuwa anatumia mkewe.”
Takwimu hizi ni kwa mujibu wa ukaguzi wa CAG katika Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto katika hospitali za India.
Wakati ofisi ya spika inatoa gharama zote hizi kwa ajili ya matibabu ya Ndugai, kuna orodha ndefu ya wabunge ambao wamenyimwa huduma hiyo ambayo ni haki yao kisheria.
SAUTI KUBWA limeelezwa kuwa baadhi ya wabunge walionyimwa huduma hiyo, ni wapinzani, na wamekuwa wakitibiwa ndani na nje ya nchi kwa gharama zao binafsi, mikopo au michango ya ndugu na jamaa zao.
Chanzo kimoja kutoka bungeni kimesema: “Kwa kuanzia na Mheshimiwa Tundu Lissu, ambaye maisha yake yaliokolewa na michango ya watanzania, yupo pia Mheshimiwa Zubeda Sakuru ambaye hadi sasa anajigharamia matibabu, na ofisi ya spika imegoma kutoa chochote. Mheshimiwa James Mbatia alipovunjika mkono, alitibiwa India kwa jitihada binafsi; ofisi ya bunge ikakaa kimya.
“Mheshimiwa Ester Bulaya amegharamia matibabu yake mwenyewe, na Mheshimiwa Conchesta Rwamlaza amejilipia gharama za kwenda Muhimbili, Nairobi na India, na hadi sasa ofisi ya spika inapiga danadana. Majuzi tu, tulimpoteza Mheshimiwa Kasuku Bilago, ambaye hadi anaaga dunia kwa kukosa matibabu ya uhakika, alikuwa anahangaika kujilipia, huku ofisi ya spika ikiwa imegoma kugharamia matibabu yake.
“Hii yote ni kujaribu kuonesha ni jinsi gani gharama za matibabu zinavyotolewa kwa upendeleo wakati wabunge wote kwa mujibu wa sheria wana haki sawa ya kupatiwa matibabu.”
Kwa mujibu wa Sheria ya Uendeshaji wa Bunge ya mwaka 2008, katika kifungu cha 24(1), “matibabu ya mbunge yatagharamiwa na Bunge ndani na nje ya Tanzania.”
Bunge limekuwa linatumia kifungu hiki kuidhinisha malipo ya matibabu ya Ndugai na baadhi ya wabunge, hasa wa CCM, lakini limekataa kutumia kifungu hicho hicho kutibu wabunge wengine, hasa wanaotokana na vyama vya upinzani
Mwandishi amewaorodhesha wote hawa kutoka upinzani, ingekuwa vyema akaorodhesha wabunge kadhaa wa CCM waliohudumiwa tofauti mbali ya huyo spika.Chanzo kimoja kutoka bungeni kimesema: “Kwa kuanzia na Mheshimiwa Tundu Lissu, ambaye maisha yake yaliokolewa na michango ya watanzania, yupo pia Mheshimiwa Zubeda Sakuru ambaye hadi sasa anajigharamia matibabu, na ofisi ya spika imegoma kutoa chochote. Mheshimiwa James Mbatia alipovunjika mkono, alitibiwa India kwa jitihada binafsi; ofisi ya bunge ikakaa kimya.
“Mheshimiwa Ester Bulaya amegharamia matibabu yake mwenyewe, na Mheshimiwa Conchesta Rwamlaza amejilipia gharama za kwenda Muhimbili, Nairobi na India, na hadi sasa ofisi ya spika inapiga danadana. Majuzi tu, tulimpoteza Mheshimiwa Kasuku Bilago, ambaye hadi anaaga dunia kwa kukosa matibabu ya uhakika, alikuwa anahangaika kujilipia, huku ofisi ya spika ikiwa imegoma kugharamia matibabu yake.
Hii nchi ina maajabu sana, pamoja na mbunge tajwa hapo juu aliekuwa akiwakilisha jimbo la Ndanda kupitia CHADEMA kutangaza kujiuzulu ubunge na kujivua uanachama wa CHADEMA na kujiunga na CCM lakini bado anaendelea kupata stahiki zote kama mbunge na Ndugai bado anamtambua kuwa Cecil Mwambe ni mbunge wa Bunge la Jamhuri.
Kitendo cha Mwambe kuhamia CCM kilimpotezea sifa ya kuendelea kuwa mbunge, Hili la leo Spika wa Bunge amedhihirisha udhaifu alionao. Spika ni dhaifu na Bunge la 11 ni Bunge dhaifu mno katika historia ya Tanzania.
Kweli bwana. Eti Ndugai anasema haitambui barua ya katibu mkuu wa Chadema. Mwambe si alihama chama kwa hiari na barua aliyoandika ndiyo inatumika kama kielelezo ambayo spika analetewa nakala na Mwambe mwenyewe? Hili lizee kweli ni zero!
Kwani Cecilia mwenyewe anahudhuria bungeni au mpunga unaflow tu amelala.?
Ndugai amethibitisha kupokea barua ya kutaarifiwa toka kwa katibu mkuu wa Chadema JJ Mnyika na kaitupilia mbali na kusema kuwa haina maana
Sent from my iPhone using JamiiForums
Na hilo ndiyo tatizo kuu, linalofanya vitanda visilalike huko Chato!Hivi quorum imetimia kule bungeni?? Nina wasiwasi Budget Kuu ya serikali haiwezi kupita bila wabunge hawa!!!!!!
Sent using Jamii Forums mobile app