Spika Ndugai awataka wabunge wajenge nyumba Dodoma kwani hata wabunge wa Kenya wote wana nyumba Nairobi

Kwani ubunge unapewa hatimiliki??ukijenga usipo chaguliwa na wananchi inakuaje sasa??halafu economically hotel lodge hotel wata survive vipi??serekali itakosa mapato kiasi gani?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
KUMBE!
 
Kwanza ubunge ni miaka mitano na siku za kukaa bungeni kwa Mwaka hazizidi siku 120
Hivyo sio afya kujenga nyumba utakayoishi siku 120 kwa Mwaka

Pili miji huendelea kutokana na shughuli za biashara malazi, chakula, starehe, n.k pale mbunge anakuwa na nyumba in amaana atakula nyumbani, atalala nyumbani hivyo mahoteli na migahawa haitapata walaji hivyo Kodi Ajira zitapungua.

Unapowashawishi wajenge maana yakeunataka wahamie Dodoma hata baada ya kustaafu ubunge kitu ambacho sio afya kwa maendeleo ya miji na majiji. Watu warudi kwao baada ya kipindi Cha ubunge na utumishi kuisha.

Bank zimeruhusiwa kujenga jengo la makao makuu tu huko kwengine wanatakiwa kupanga, unafiriki bank wangepewa mwanya wajenge wenyewe nini kingetokea?
 
Kwa Wabunge hubadilika, mimi ningeshauri kila Halmashauri / Jimbo la uchaguzi lipewe kiwanja lijenge nyumba kwa ajili ya kumpangishia Mbunge wake na hiki kitakuwa ni chanzo cha mapato cha kudumua kwa halmashauri husika,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…